Athumani Idd'Chuji' na Haruna Moshi'Boban' kujitoa stars

Athumani Idd'Chuji' na Haruna Moshi'Boban' kujitoa stars

Marcimo is na everage coach, amekuwa overated na media ile mbaya! Sidhani kama uwezo wake unafikia hata wa Silversaid Mziray!! Mnakumbuka timu alipewa ikishindia chipsi dume na maji lakini tukachukua kombe la challenge...all the supports angepewa Mziray timu ingeenda kombe la dunia. Sitetei tabia za kuvuta bangi za Chuji na Boban ni wakati wa wadau kumuona Maximo uwezo umefikia pomoni aende zake wazalendo wachukue timu..Brazilian coach hawana mafanikio zaidi ya nchini kwao

Masa
 
Sitetei tabia za kuvuta bangi za Chuji na Boban ni wakati wa wadau kumuona Maximo uwezo umefikia pomoni aende zake wazalendo wachukue timu.

Sasa mbona hatuweki wazi kama hawa jamaa wanavuta Bangi?Si angesema tumwelewe si wadau wa soka la hapa Bongo...
Ni kweli ualimu wake sasa umefika kikomo inamlazimu aachie ngazi tu kama anasoma alama za nyakati.
 
Katika historia sijawahi kusikia jeshi lenye askari wasio na nidhamu, likapata mafanikio makubwa vitani.Shuleni walimu walituhimiza kuwa na nidhamu kama kuwahi shule, kuhudhuria vipindi, kuheshimu sheria na taratibu and all those have made the students become good and organized people...team, as an army contigent, must have displined soldiers. kama General, ningejisikia vibaya kama nikisema geuka kushoto halafu kila mtu anafanya anachojisikia kufanya.
Kama issue ni displine basi Maximo yuko sahihi..tusidaganyane hapa Chuji na Boban sio mastaa kiasi hicho labda kibongo bongo. Hawataweza kufika popote kwenye professional football kama hawana displine. Lets dig down the facts kabla ya kusoma fatwa dhidi ya Maximo.
Tukumbuke pia in the army, wars are won in the generals tents, because they normally lay out the plans and strategies to execute the war. Naamini Maximo anataka kuona tunabadili katika mvumo mzima wa mpira wetu kwa kuachana na uyanga na simba na kuunda timu yenye nia na kucheza mpira kwa nidhamu.
Vinginevo hata tukipata kocha gani, kwa wachezaji ambao hawana nidhamu tutabaki kuwafukuza bila kutatua tatizo
 
Katika historia sijawahi kusikia jeshi lenye askari wasio na nidhamu, likapata mafanikio makubwa vitani.Shuleni walimu walituhimiza kuwa na nidhamu kama kuwahi shule, kuhudhuria vipindi, kuheshimu sheria na taratibu and all those have made the students become good and organized people...team, as an army contigent, must have displined soldiers. kama General, ningejisikia vibaya kama nikisema geuka kushoto halafu kila mtu anafanya anachojisikia kufanya.
Kama issue ni displine basi Maximo yuko sahihi..tusidaganyane hapa Chuji na Boban sio mastaa kiasi hicho labda kibongo bongo. Hawataweza kufika popote kwenye professional football kama hawana displine. Lets dig down the facts kabla ya kusoma fatwa dhidi ya Maximo.
Tukumbuke pia in the army, wars are won in the generals tents, because they normally lay out the plans and strategies to execute the war. Naamini Maximo anataka kuona tunabadili katika mvumo mzima wa mpira wetu kwa kuachana na uyanga na simba na kuunda timu yenye nia na kucheza mpira kwa nidhamu.
Vinginevo hata tukipata kocha gani, kwa wachezaji ambao hawana nidhamu tutabaki kuwafukuza bila kutatua tatizo

Displine ni pamoja kuwachukulia hatua wale walio chini ya mamlaka yako, sasa wachezaji ni Maximo ndio kawaita sasa si awachukulie hatua. Mambo ya kununiana na mtu aliye chini yako si mambo ya kitoto kwani kuna ambaye atahoji kwa nini kawafukuza.

Nidhamu ni pamoja na kuthamini mawazo ya watu wengine hata kama hawakubaliani na wewe, uchezaji mpira wa kibongo bado hata kama tungefika finali ni zali tu! wabongo wanaangalia mpira huku wamebana ***** manake, presha inapanda presha inashuka.
 
Mkuu, Bangi isiwe big issue. Wengi tu wanavuta/walivuta ktk umri huo - Michael Phelps, Obama etc.
Mkubwa huko ulaya watu wengi wamevuta sana bangi lakini hawakufanya mambo mabovu but huku Tanzania mtu unavuta bangi inaleta kiburi,huyo dogo BOBAN hata mazoezi alikuwa anachelewa kuna wakati MAXIMO alimpiga chini wadau wakapiga kelele then akamrudisha sijui issue ya CHUJI but BOBAN alichemsha ile game ya kwanza
 
OK Mnasema MAXIMO uwezo umekwisha sasa tuambiane tumchukue kocha gani naye tumpe muda miaka 3 na hao jamaa waendelee kuvuta bangi tuone kama kutakuwa na mabadiliko
 
Maximo siku siku zako zinahesabika stars.maana sasa imekua too much.baada ya kaseja sasa umeamia kwa boban na chuji. hakuna mtu hasiye jua tabia yako umekua mtu wa kuigawa stars sana ingawa stars inashinda simply coz of juhudi binafsi.

Kwa mshahara gani unaomlipa mpk useme siku zake zinahesabika? Angalia tulipokuwa kabla ya Maximo na sasa. Wakina Mziray, Mkwasa, Kibadeni na wengine wengiiiiiiiii walipita hapo na Blah blah kibaooo. Acha Maximo aendelee kujenga timu. Hakuna mwenye ubora ndani ya timu ya Taifa zaidi ya Kocha. Waache waendee na bora wamefanya hivyo maana Maximo alishawaambia wachezaji wote sasa hivi anataka damu changa kuinua vipaji ndio maana hawa wamekuja na madaaa hiii kabla rungu halijawashukia. Maximo Komaaaa nao hvyo hivyo maana walishazoea kwamba anayetoka Yanga ama Simba basi lazima anakiwango na achezeee HAKUNA HIYOOOO.
 
MAXIMO amewapa nafasi wachezaji kama Bonny,Dihile,Swedi,Nditi,Tegete,Makasi,Jabu ambao wengi ni chipukizi na sijui kama kuna kocha mbongo ambae angewapa nafasi
Makocha wetu kina Mziray angeendelea kuwakumbatia kina Pawasa,Gabriel,Abdalah Juma
 
Maximo siku siku zako zinahesabika stars.maana sasa imekua too much.baada ya kaseja sasa umeamia kwa boban na chuji. hakuna mtu hasiye jua tabia yako umekua mtu wa kuigawa stars sana ingawa stars inashinda simply coz of juhudi binafsi.
Hao kina BOBAN walicheza ile michuano ya kwenda kombe la dunia mbona bado tulichemsha
 
Mpira ya Kitanzania ni maneno na waandishi wa habari, hapa tatizo ni Coach, huyu Maximo tangu mwanzo alionekana na itilafu nyingi tu, akina Mziray walianza kumchambua mkawakalia kooni. Sasa msubiri kufanywa kitu mbaya. Huyu bwana basi, matarajio mmemuwekea mengi na kila siku ahadi zisizo na mafanikio, wengi wenu mnaigiza mchezo wa mfalume aliye uchi. Kwa woga wenu mnakataa kusema ukweli na kupindisha maneno ili bwana JK asikasilike kwani ndie aliyemleta na ofisi yake ndo inalipa mshahara. Kulingana na sheria za TFF ya dunia (FIFA) chama cha nchi husika kina uwezo wa kum discipline Coach, vipi huyu state OG - Tenga anao ubavu. Kama TFF wangekuwa huru sio ndio mzee. Maximo angekuwa tayari amefungasha virago.
 
MAXIMO alishasema mkataba ukiisha anaondoka suala lililopo ni kujadili nani ambye ana uwezo kuliko yeye atakaweza kumrithi lakini sidhani kama kuleta kocha mwingine ndio suluhisha ,soka la Tanzania tuna matatizo mengi sana hilo la kocha ni mojawapo
Kenya wana MARIGA,OLIECH wanacheza ulaya na kina AMBANI,MWALALA,OWINO,SUNGUTI wanacheza bongo,Uganda wana NSEREKO na OBUA wako ulaya .Sijui kama kuna mchezaji wa bongo anayecheza soka Kenya au Uganda
 
Huyu jamaa ndie anaefaa kubadilisha soka la Tanzania hope hata akiondoka viongozi wengi watasoma.ukiuliza makocha wengi wa Tanzania watakwambia tatizo kubwa la ukocha Tanzania ni kuingiliwa kazi na viongozi kwa kweli huu ni ukoma kwa soka ya nchi yetu.Soka inaanza kwenye nidhamu si uwezo kisoka tu kwa tabia zetu watatoka baadhi ya viongozi kuwatetea hawa jamaa.Maximo yuko hadi leo kwa sababu ana support ya Rais na analipwa na rais na ingakuwa viongozi wetu wa soka wana maamuzi juu yake basi asingekuwapo leo hii.Watanzania tubadilike tutizame nchi zilizoendelea kisoka tuache kujifananisha na Kenya na Uganda Please. Think Twice.



SAHIBA.
 
Timu kama haina uelewano kufungwa ni rahisi na ndicho walichovuna huko Ivory Coast. Nadhani Masikio Maskimo amefika ukomo wake.
 
Timu kama haina uelewano kufungwa ni rahisi na ndicho walichovuna huko Ivory Coast. Nadhani Masikio Maskimo amefika ukomo wake.



Ziwepo sababu za msingi za kukosa maelewano sio kwa sababu mchezaji hapangwi eti anaanzisha zengwe mpira ni uwezo sio jina.timu inaleta hope tofauti na miaka mingi iliyopita,Maximo ameleta nidhamu na hicho ndio chalenge yake kubwa hatutaki changes.Kocha yeyote mzalendo atakaekuja atakuja na usimba na uyanga believe me tumebaki kushindana timu ya taifa ina wachezaji wa timu gani wengi yanga au simba bila kujali ushindi.


SAHIBA.
 
Hao wote wawili cha vya bangi.....wange bofoa tu...heri ambavyo hajawapanga.
 
Kama hao kina Boban amewaacha kwa suala la nidhamu, 100% nampongeza maximo. akaze uzi tu tutafika. kutufikisha kwenye hayo mashindano tu ambayo miaka 29 tulikuwa hatuwezi ni jambo kubwa sana.

Makocha wetu( Kibaden, Mziray etc) na kubembelezana na wachezaji wasio na nidhamu ndio hao hawakutufikisha hapo. Watanzania tuwe makini na maamuzi inapokuja suala la kuangalia mambo, Soccer needs a lot of discipline nje na ndani ya uwanja, it is a team which plays, not individuals, so to coordinate them and make them play like a team its not a joke.ukiwa na mandunda wanaotaka kuleta ubrazameni hamuwezi kuwa team,. Kama hawana nidhamu Maximo kick their ass out, we want a team with discipline ndio itafundishika vizuri. Big up maximo.
 
Lakini yeye kama kocha anaweza kubalisha mcheza na pia yeye kama mlezi kafanya juhudi gani za kuwa rekebisha kina kaseja,boban,chuji...hivi kina chuji wamefikia utovu wanizamu kama kina Diof... huyu bwana kazi imemshinda, tumempa mchango wa kutosha kitu ambacho hakija wahi kutokea kwa kocha yoyote wa timu ya taifa lakini mpaka leo hana hata first eleven...tunamshukuru kwa kutuunganisha/kupunguza usimba na uyanga kwenye timu ya taifa lakini mkataba ukiisha aende zake hana jipya tena..
 
Jamani,lazima tuwe na malengo katika soka letu,kipimo cha mafanikio ya kocha ni nini kama sio vikombe?kwa muda wote huu Maximo kashindwa kuchukua kikombe ata kimoja,tumshukuru kwa alichofanya mpaka sasa ila tunahitaji zaidi ya kupanda kwenye rank ya FIFA,tunahitaji vikombe,ni wakati wa kumove on...ni wakati wa kumpatia kijiti kocha mwingine,na nadhani itakuwa vyema tukipata kocha kutoka Ufaransa au Ulaya mashariki,hatuwezi kujiridhisha kwa mafanikio ya mdomoni tu wakati ata challenge hajabeba!!
 
"Pamoja na ubora wake katika ufundishaji, moja ya kasoro kubwa ya kocha huyo imekuwa ni suala la kukasirika mara kwa mara na pia kuweka visasi kitu ambacho wadau wamekuwa wakimuasa kuachana navyo kwa faida ya kikosi chake"

Mimi huwa sipingi professional ya mtu kwasababu hata ya kwangu napenda iheshimiwe sana. Lakini kwa huyu Bwana Marcimo mimi naona ameshindwa yeye mwenyewe kuhiheshimu taaluma yake. Yeye kama kocha anatakiwa ajue kuwa ana-interact na wachezaji wenye tabia na malezi tofauti sasa kwanini hasiwe anaacha hasira za kudumu kwa mchezaji anayekosea. Kwanini hasichukue mifano ya makocha wa Ulaya ambao wana tabia ya kukanya wachezaji wao na kuwasamehe baada muda. Mfano mzuri ni Kocha Fabio Capello wa England, huyu kocha alikuwa hapatani na David Beckham wakati wakiwa Real Madrid, lakini sasa hivi anamtumia kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza. Kwanini Marcimo yeye hasiwe anaiga haya mambo ya msingi. Mimi nafikiri anafanya haya kwasababu ameona na amejua kuwa sisi watanzania tunamnyenyekea sana. Aondoke tu kama alivyofanya Tinocco ambaye kashachuma vya kutosha kaenda zake kupiga business.
 
Hivi Tinocco tumkumbuke kwa lipi wa tanzania...huyu jamaa alikuja kuchuma tu..
 
Last edited:
Back
Top Bottom