Bonnie1974
JF-Expert Member
- Mar 19, 2008
- 407
- 17
Bongo tutakuwa na mpira mpaka baada ya miaka 30 na kuendelea ila kwa sasa tuendeele kuwasindikiza wenzetu!!
sawa mkuu, ni kweli ametutoa mbali. Ila issue ni kwamba kuna fighting talk in taifa stars dressing room na inaonekana yeye ndiye tatizo. Ni hulka yetu watz kutopenda mabadiliko. Tusimng'ang'anie tu kama tunavyoing'ang'ania ccm ilivyotutoa mbali https://www.jamiiforums.com/images/smilies/confused.gif
😕.
Maximo anatakiwa kuwatambua wadau wa soka na kuhakikisha maslahi ya wadau yanatimia, sasa wachezaji ni wadau na wana maslahi pia cocher ni zaidi ya mwalimu sasa Maximo ana behave kama mwalimu wakati anapewa vinaja awacoach.
Si sahihi kusema mafanikio ya stars yanaletwa na Maximo, yeye ni mdau mmoja wapo katika kundi la wadau na hakubali na lawama pia. huyo Jk aliyemleta analaumiwa kila kukicha ndio itakuwa Maximo bwana, amebwagwa Big Phil wakati timu ni ya Tatu katika msimamo. Lakini wabongo tunaambiwa tulidhike na kufungwa, kudroo na kushinda game moja hata kama tuna mtazamo tofauti hii haipo mpira unanoga kama kuna wanao pinga, sio siasa kusema ndio mzee kila siku.
Kwa mazingira ya sasa Tanzania inastahili kuwa mbali zaidi ya ilipo, hata ushindi wenyewe sio predictable kama zilivyo timu za wenzetu. Ukilinganisha na majirani zetu sisi ndio tumewekeza zaidi katika timu ya taifa na hata ligi kuu, tunawazidi hata kenya katika matumizi wakati uchumi wetu ni mdogo lakini kiwango chetu ndio cha chini. tukisema mnalinganisha na miaka 18 iliyopita tena mnafunika hata historia kwamba mashindano yale ya mwaka 1982 ilikuwa CHAN ya ukweli sio hii ya wachezaji wa ndani.
Lakini mnakuwa wakali mkiambiwa bongo bado, si tunaona wakicheza sifa hazikutosha kutupeleka nusu fainali na Afrika mashariki ndio tumechezea kichapo hata cha wasomali. Pesa inayoenda stars ni nyingi kuliko kinachopatikana huko, uliza hata zambia wametumia ngapi ndio mjue Tanzania wanapiga hela na kugombana. Kama bangi wachezaji wengi wa kibongo wanakula jani na sio kigezo cha mwalimu kuchuniana na wachezaji kama vipi si awafukuze yeye si ndio kawaita anaogopa nini sasa.
tatizo bangi wakuu, hawa vijana, na wengine wapo ila maximo hajawagundua, wanapuliza balaa!!
MAXIMO alishasema mkataba ukiisha anaondoka suala lililopo ni kujadili nani ambye ana uwezo kuliko yeye atakaweza kumrithi lakini sidhani kama kuleta kocha mwingine ndio suluhisha ,soka la Tanzania tuna matatizo mengi sana hilo la kocha ni mojawapo
Kenya wana MARIGA,OLIECH wanacheza ulaya na kina AMBANI,MWALALA,OWINO,SUNGUTI wanacheza bongo,Uganda wana NSEREKO na OBUA wako ulaya .Sijui kama kuna mchezaji wa bongo anayecheza soka Kenya au Uganda
Unamaaanisha hujang'amua lolote hapo?
Mpaka sasa ni Maximo tu anayeongea na hatujamsikia Chuji na Boban upande wao. Actually mimi ningependelea hawa wawili wakae kimya kwani tunajua what happened in Ivory Coast.
Maximo kaitenga timu na hakumchezesha Chuji eti mpaka semi finals kwakuwa alikuwa majeruhi wiki 8. Wakati huohuo cheti cha daktari wa timu kimempa clean bill of health - Chuji anacho hicho cheti. Vilevile Chuji alikuwa na watu wamekuja kumuona live michezo yake na walivyotaka kumuhoji kuhusiana na maswala ya kucheza nje ndipo Maximo akapiga marufuku kuwa hakuna ruksa kuongea na wachezaji bila idhini yake kwanza. Chuji alienda kuomba idhini na Maximo akamtolea nje. Usiku huo hakulala vizuri kiasi kwamba asubuhi alichelewa kuamka na kukosa mazoezi na hapo Maximo akasema Chuji ana utovu wa nidhamu amesusia mazoezi. Wakati huohuo kwenye mazoezi watu wanakwambia Chuji alikuwa mnyama, yaani a beast in practice, akipiga zoezi mpaka watu wanashangaa kwa nini hapangwi?
Baada ya matukio hayo Chuji akawa anajifua sana mwenyewe beach na alisikika akisema yeye sasa anajifua kwa ajili ya timu yake ya Yanga ktk kombe la klabu bingwa Afrika na ndiko ataonekana na kutoka huko. Habari hizi zilipomfikia Maximo ndia ikawa mwisho wa wao kuzungumza, manake hata kusalimiana Maximo hasalimii wala kumjibu!
Maximo has a lot to answer to and the sad fact is that he is being given the benefit of the doubt in this issue. Chuji anaonekana mvuta bangi tu lakini wote tunaopenda mpira tunajua uwezo wake kimpira, Bangi ni nini bwana? It is not even a Performance Enhancing Drug but a "social" drug that is known for ruining ones potential in the long run - for short time relaxation it is da bomb! Peter Tosh said it best - some lawyers, doctors, politicians etc smoke it. Sasa iwe Chuji?!
My suggestion to Chuji and Boban: let sleeping dogs lie!. Muacheni Maximo asemeeee weeee lakini si July anakitoa zake? Kocha anayekuja si atachagua timu yake bwana na si atawaona mchezo wenu?
Stay cool, my brothers, stay cool!!!!
Lakini kuna kitu alitaka kukieleza nafikiri ameshindwa kupangilia
Hebu usituchekeshe hapa, wewe ni lazima utakuwa ni komandoo wa Yanga.
Ati unasema hao wavuta bangi wakae kimya wasiseme, then wewe ndiyo unawaongelea badala yao. Tafuta kazi ya kufanya na wala siyo kuongelea mambo yasiyokuwa na mbele wala wa nyuma.
He / She failed. Dunia haiwezi kusimama kumsikiliza a failure.
Watu wengine bwana........Kaaazi kwelikweli!!!!
Your rambling ndi umeona ya maana kumbe hakuna kitu! Niliyoandika hayasemi ni kwa niaba ya nani bali ni maoni yangu tu na nimeshauri wakae kimya na wasizue mtafaruki mkubwa. Au mwenzangu inglishi not richabo because I sincerely began the sentence with "I suggest......" Ooooops, sorry, nimeanza na sentensi inayosema "Napendekeza....."
Kwa jinsi hiyo basi naona wameamua kukaa kimya (kama nilivyopendekeza??) - sasa nani mwenye mayai usoni mwake??? Wewe!!!