Nimemsikia nabii mmoja wa Arusha ambaye ana cheo cha daktari wa falsafa (PhD) akifundisha kwenye radio yake kwamba Mungu hujifunua kwa majina tofauti kila anapofanya agano. Sasa ananukuu pale Mungu anapoongea na Musa kumwambia alimtokea Ibrahimu kama Mungu mwenyezi lakini hakujulikana na Ibrahimu kwa jina lake Yehova na anafafanua kwamba hayo yote mawili ni majina ya Mungu. Kwa hiyo hata " mwalimu mkuu" ni jina la mtu (personal name)? Personal name ya Mungu wa biblia ni moja tu ambalo Wayahudi walikuwa hawalitaji hovyo hovyo. Mengine ni vyeo vyake au sifa zake. Ni kama vile mwalimu mkuu anaweza pia kuwa mwalimu wa physics lakini ana jina lake binafsi.