Ati ni kweli kuwa kuna kada hata wafanye Kazi miaka mia hawezi kuwa na nyumba kama ya Mwijaku?

Ati ni kweli kuwa kuna kada hata wafanye Kazi miaka mia hawezi kuwa na nyumba kama ya Mwijaku?

Ile topic NI rahisi,nzuri, na Applicable.
Ukiijua hiyo na kuitumia hakuna mwanadamu atakayekuchezea wala hutamlaumu yeyote.

Kwani Kunguru utamuweka kwenye Kunguru wenzake
Njiwa kwa njiwa
Kenge kwa kenge
mbzui kwa mbuzi
Popo kwa Popo
N.k

Kosa kubwa ni kumlazimisha Mbwa awe paka. Yaani mtu ushamuona yupo class Hii alafu unataka utumie mawazo na matamanio yako awe vile utakavyo. Hilo ni kosa.

Mbwa m-treat kama mbwa
Paka m-treat kama paka
Kuku m-treat kama kuku.
Wote ni muhimu ila zingatia matumizi yao tuu
Upo sahihi sana,Kuna sehu Huwa tunakwama kulazimisha kunguru kuwa njiwa
 
Kwa hiyo nikimkuta tabia zake mbovumbovu nipambane nazo?

Ni jukumu lake kujibadilisha.
Kama hatajibadilisha basi abadilishwe na matokeo ya kile alichokifanya hayo ndio mabadiliko ya kweli.

Lakini wewe unapambana nazo kivipi wakati wewe mwenyewe unayako ya kukabiliana nayo?

Mimi sio muumini wa kumbadilisha mtu kwani najua ni kazi ngumu inayohitaji uvumilivu na muda
 
Habari wakuu!

Baada ya kuwakandia Machawa na kuwatukana vilivyo mpaka humu ndani uzi wangu kufutwa.

Moja ya viongozi wa bodi ya Machawa Tanzania alinipigia simu jana akiwa na furaha nyingi. Nikiwa najua kuna dili la kibiashara linakuja, nashangaa ananiambia unamuona Mwijaku huko.

Nikamwuliza kafanyaje? Akanijibu, alichofanya kuna bàadhi ya kada hata wangefanya kazi miaka mia na wapewe kiunua mgongo bado hawataweza kujenga nyumba kama ya Mwijaku.

Nikamkatia Simu. Akatuma sms wala sikuifungua. Nilijua ni mpuuzi tu. Sasa nauliza, uchawa unalipa eeeh! Lengo la kuhamasisha uchawa ni nini? Ni kwamba hawajiamini na wanatafuta kutambuliwa ndani ya jamii?

Au je Mwijaku kama moja ya viongozi waandamizi wa uchawa kuonyesha nyumba yake ni kujaribu kuwazima midomo kina siye tunaosakama shughuli yao? Au ni majibu kwa wale wanaomuona ni mwanaume wa hovyo na sasa kawajibu kivitendo kuwa yeye ni mwanaume wa aina gani?

Je, kulikuwa na ulazima upi wa Mwijaku kuonyesha mafanikio ya kazi yake?
Je, kuwawatia moyo Machawa wengine wakaze?
Àu je, kuwafungua macho vijana kuwa kazi yoyote ukiifanya kwa moyo na kwa bidii inaweza kukutoa?
Au je, kuwakatisha tamaa adui na hasimu wake?

Je, huu ndio mwanzo wa Machawa na wale wote wanaofanya kazi zinazodharauliwa ingawaje sio haramu nao kuonyesha kuwa wanapata mafanikio makubwa kwa kazi hizohizo zinazodharaulika. Tuliona kwenye kazi ya muziki ikiwa miongoni mwao kazi zilizodharaulika, kwa sasa wanamuziki kwa kiasi chake wanakaheshima kadogo na bado wanahangaika kujenga heshima?

Kazi ya udalali nayo je viongozi wake waandamizi nao watajibu kwa vitendo kama walivyofanya Machawa?

Wakati sisi Wasomi na wenye elimu za juu na pengine kazi kongwe ambazo zinaheshimiwa kwenye jamii tukiwa hatuna maisha mazuri na hata vijumba vyetu vikiwa dhoofu hali, je tuna haja ya kubadili mtazamo kuhusu maisha na kazi?

Hii inawaambia nini vijana waliomaliza chuo na waliokochuoni kuhusu fursa zilizoko kwenye jamii baada ya kumaliza masomo yao?

Je, tutabdilike ikiwa dunia itatuletea mabadiliko ya kazi mpya na zile za zamani kupitwa na wakati?

Kazi kama utengenezaji wa Memes, Stand up comedy, maigizo mafupi mafupi mtandaoni, online business, n.k je ni wakati wa kuzitambua na kuziheshimu ikiwa watumiaji wake wanapata pesa za kuendesha maisha yao na kuishi maisha mazuri ingawaje wale kina siye hatutaki kuona hilo?

Embu Acha nipumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Cc Lucas mwashambwa
 
Mpwayungu Village unaitwa huku utoe maelezo Kama muwakilishi kada ya ualimu
Magu au JOM alikuwa mealimu. Sasa mlinganishe na mwajaku na co. yake.
Kazi yoyote ile unaweza jenga ghorofa.
Hao hao machawa wapo waliochoka mbaya.
Polisi , Jeshi, walimu, bankers wapo waliojenga ghorofa na wapo waliochoka.
Walimu wanafursa tofauti. Mwalimu aliepo NECTA na wa sekondari wana fursa tofauti. Jeshi aliepo makao makuu na jeshi wa kambini wana fursa tofauti.
 
Yeap baadhi ya kada hawatoboi..Ila wapo waajiri wa serikali wanaweza kabisa.

Kumbuka Mwijaku ana miaka 39-40 hapo kati ,chukulia hawa madogo wa TANPA,TRA, BOT ,TPA walioanza ajira wakiwa na miaka 25 mpaka wakifika miaka 35 yaani miaka kumi mbele wana uwezo wa kujenga ile nyumba, kwa gharama halisi ..
.
 
Yeap baadhi ya kada hawatoboi..Ila wapo waajiri wa serikali wanaweza kabisa.

Kumbuka Mwijaku ana miaka 39-40 hapo kati ,chukulia hawa madogo wa TANPA,TRA, BOT ,TPA walioanza ajira wakiwa na miaka 25 mpaka wakifika miaka 35 yaani miaka kumi mbele wana uwezo wa kujenga ile nyumba, kwa gharama halisi ..
.

Ni kweli kabisa
 
Mkuu kada iyo labda uitaje. Maana ile nyumba ya Mwijaku ikizidi sana labda Mil 200 na kuna mtu anapokea kiinua mgongo mil 300 ashindwe kusimamisha mjengo kama ule?

Sio lazima kuongea waweza kaa kmy tu
Sa nkuulize ww ndg yangu iv unaweza lipwa kiinua mgongo millio300 na zote ukaenda kujengea?
Maisha sio nyumba tuu jarib kuelewa ilo litakisaidia
 
Sio lazima kuongea waweza kaa kmy tu
Sa nkuulize ww ndg yangu iv unaweza lipwa kiinua mgongo millio300 na zote ukaenda kujengea?
Maisha sio nyumba tuu jarib kuelewa ilo litakisaidia
Sio kila mtu ana shida ulizonazo wewe. Kuna watu wameshafanya kila kitu na akajipigia hesabu kiinua mgongo anaenda kunyanyua nyumba yake ya kustaafia. Kama anapokea 300 M basi anatupa ardhini 200M kulingana na mahitaji yake ikiwezekana anatupa yote huko ili mradi moyo wake upate kile anachohitaji.
 
majibu ya mswali yako unayo, sasa unataka tukuthibutishie au tukasahihishe ili tulips maksi ??
 
Back
Top Bottom