Aucho: Watanzania inabidi wasapoti wazawa na sio ku hype wageni

Hakuna tatizo Kibu kuongezewa mshahara. Anajituma na inawezekana akafanya vizuri sana msimu ujao.
Nimeshika kichwa kwa masikitiko
Mnapenda kuonea wachezaji huruma ndio maana mnayumbaaa
 
Kuna member alianzisha Uzi akaponda sana project ya Kibu kuongezewa mshahara
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Nimeshika kichwa kwa masikitiko
Mnapenda kuonea wachezaji huruma ndio maana mnayumbaaa
Sio huruma Kibu yuko vizuri endapo Simba nayo itatulia
Japo binafsi nataka tuchukue mara 5 ndio wapate utulivu au 6
 
Nimeshika kichwa kwa masikitiko
Mnapenda kuonea wachezaji huruma ndio maana mnayumbaaa
Hakuna huruma yoyote. Kibu anajituma na unaona kabisa anavyosumbua ila akili na bahati ya kufunga kakosa, hilo tu ndo la kurekebisha, hakuna ubaya akipewa nafasi. Akishindwa tena hapo sawa akajaribu kwengine. Simba ilikuwa na msimu mbovu na kikosi hakikuwa kizuri in general ila kibu alikuwa anaonekana kabisa anavyojituma.
 
Hapa kazingua sana hisia za mpira hazina mipaka Leo Ronaldo ni high paid Saudia
Mane kina Neymar Firmino n.k
Hata Azam penyewe Kuna mtu yuko benchi na ndie high paid
Tukianza na mambo ya uzawa mwishoni tutaanza na dini ya mchezaji kwamba mwaka jana kachukua muislamu mwaka huu achukue mkristo, kiufupi aucho kazingua sana kitakachoamua nani abebe kiatu ni wao kufunga magoli tu na sio kingine
 
Mbona Aucho kaongea kitu ambacho wengine huwa tunakiongelea humu siku zote...?? Sema labda wewe umeshindwa kumuelewa sababu ni mmoja wa athirika wa hicho alichokisema Aucho.

Wabongo huwa mnawa idiolize sana wachezaji wa kigeni kuliko wazawa hata kama wageni hao wana viwango vya kawaida sawa na wazawa.... yaani huwa mnawatukuza hadi wenyewe wanawashangaa huku mkiwapa nick names za kishujaa, kumbuka Meddie Kagere,Okwi, Kisinda walivyokuwa wanaimbwa kuliko hata Feisal, Bocco, Sureboy na wakati walikuwa wanamichango sawa tu hao wageni kwenye timu zao.....

Huu upuuzi wakutukuza sana wachezaji wa kigeni huwezi kabisa ukaukuta taifa kama Egypt, Morocco au hata Afrika kusini.. na ndio maana hao hao wachezaji wa kigeni wakisha shine hapa kisha wakaenda kwenye hizo ligi, huwa wanapakumbuka sana Tanzania sababu huko hawapewi media hypes kama hapa kwetu au kushobokewa na mademu mara kwa mara.

Lakini hata hivyo huwa sitaki sana kuwalaumu wabongo, sababu hili ni tatizo la kitamaduni zaidi, watanzana tuna culture flani hivi ya kipuuzi tuko nayo ya kuwathamini sana wageni huku sisi wazawza tukizarauliana na kuchukuliana poa na kupuuzana hata kwenye mambo mengine sio tu kwenye michezo.... hata hapo ofisini kwenu siku ukija jamaa raia wa kigeni kufanya kazi utaona jinsi madada zako wanamvyoshobokea na kuwa desperate hata kama hana maajabu.

We have sick culture that we should get rid of.
 
Boko alikuwa anawania kiatu na Mugalu nasi pia tulifanya mauza uza
Na hata Sasa yanafanyika na uwezekano wa Aziz kuwa mfungaji bora kwa kupambana na Fei ni ngumu juu ya uzawa ila shabiki wa yanga hawezi kuanza kumshabikia fei aliyeko Azam na kumuacha Aziz aliye yanga
Hawa wachezaji wageni tunawashobokea ila wakiondoka wana tutukana kama alivyofanya mayele nadhani aucho aliangalia muktadha huo lucy aymel aliyekuwa kocha wa yanga alituita manyani mayele alisema hatujielewi na kwamba ametupiwa majini hivyo watanzania tujitafakari maana tunawadharau sana wazawa.
 
Lakini umesahau kuna mbongo mwenzetu katuita mambumbumbu
 
Hakuna huruma yoyote. Kibu anajituma na unaona kabisa anavyosumbua ila akili na bahati ya kufunga kakosa, hilo tu ndo la kurekebisha, hakuna ubaya akipewa nafasi. Akishindwa tena hapo sawa akajaribu kwengine. Simba ilikuwa na msimu mbovu na kikosi hakikuwa kizuri in general ila kibu alikuwa anaonekana kabisa anavyojituma.
Kujituma kwake kuna faida gani kama end product ni zero? Freddy hajitumi ana goli 6, Saido hajitumi ana goli 11, Chasambi, Balua wote hawajitumi wanamzidi magoli anajituma kwenda wapi?
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Hawa wachezaji wageni tunawashobokea ila wakiondoka wana tutukana kama alivyofanya mayele nadhani aucho aliangalia muktadha huo lucy aymel aliyekuwa kocha wa yanga alituita manyani mayele alisema hatujielewi na kwamba ametupiwa majini hivyo watanzania tujitafakari maana tunawadharau sana wazawa.
Rage ni mkenya?
 
Kujituma kwake kuna faida gani kama end product ni zero? Freddy hajitumi ana goli 6, Saido hajitumi ana goli 11, Chasambi, Balua wote hawajitumi wanamzidi magoli anajituma kwenda wapi?
Ndo maana nikasema akipewa nafasi kisha akafanyia kazi end product yaani kutupia mipira wavuni halafu akaendelea kujituma atakuwa mchezaji hatari, ila iwapo ataendelea pale alipoishia atakuwa kaua soko lake mwenyewe. Umri bado unamruhusu. Binafsi naona kupewa nafasi tena huu msimu ni sahihi.
 
kama bado hamja jua sababu inayo wafanya mnapambania nafasi ya pili mpka sasa endeleeni kumpa nafasi sisi huku kwetu nafasi hazizidi tano ukizingua una kaa bench hatuwezi kukosa ubingwa kwa kulea uzembe
 
Kuwa nafasi ya tatu ni suala la kikosi chote, huwezi sema Kibu ndo katuweka hiyo nafasi. Ila utakuwa sahihi sana iwapo atapewa nafasi na kurudia aliyoyafanya msimu uliopita. Msimu umekwisha, tusubiri msimu ujao.
 
Basi wapeni nafasi tena kikosi kizima msimu ujao watajirekebisha , tuta kutana hapa mwisho wa msimu kufanya tathimini
 
Hapana, kuna ambao umri umewatupa mkono huwezi endelea nao, kuna ambao uwepo wao unasababisha nafasi ya kuibua vipaji vipya ikosekane, kuna ambao hawana nafasi ya kubadilika sababu wameshaoffer to the maximum na kuna wenye shida za kinidhamu.

Kwani una tatizo gani na kibu kupewa nafasi? Umri unauhusu, tatizo lake linajulikana na anaweza lifanyia kazi na anajituma. Tatizo ni nini?
 
Back
Top Bottom