Audi A4 Gari Moja Ya Kichawi Sana, Twende Pamoja utanielewa

hahahahahah mafundi hawazipendi D-4 sababu hazitaki ubabaishaji kuanzia sheli mpaka kwenye oil zake. Pia zina mfumo wa umeme ambao haukawilii kuloga🤣
... hapo nimekuelewa chief. Ni kweli nina ka D-4 kangu kuna sheli fulani fulani huwa nikiweka wese naona tofauti kabisa na nikiweka kwenye sheli kama TotalEnergies, Oryx, Puma, n.k. gari inakuwa imetulia vizuri sana.
 
... Mkuu hebu fafanua japo kiduchu kuhusu D4 engines za Toyota; kuna ubishi mwingi miongoni mwa mafundi wa chini ya miembe kwamba ni injini za ovyo sana na hata gari ikiwa na aina hiyo ya injini kuuzika ni msala. Msaada tafadhali.
Kama huwezi kutunza engine ya D4, yes usinunue. Hazitaki ubabaishaji kwenye spea na service.

Japo D4 inayolalamikiwa sana naona ni 1AZ-FSE ambayo ipo kwenye Rav 4, Noah Voxy, Wish, Nadia, Caldina, Ipsum, Premio n.k.

D4 ya Toyota Crown hailalamikiwi naona.

Maana Toyota Crown zote kuanzia 4GR mpaka 2GR ni D4.

D4 kama ya 1AZ siyo gari ya kununua kwa mtu hasa kwa sisi ngozi nyeusi,hata mimi siwezi kumshauri mtu.

Agiza nje au kachukue yard.
 
....

D4 kama ya 1AZ siyo gari ya kununua kwa mtu hasa kwa sisi ngozi nyeusi,hata mimi siwezi kumshauri mtu.

Agiza nje au kachukue yard.
... Mkuu umegusa penyewe! Ya kwangu ni the same model (D4-1AZ) niliagiza mwenyewe. Hebu fafanua kidogo Kiongozi; zina shida gani hasa hizo engine! By the way nilivyoagiza niliipenda kwa sababu ya low mileage ila gari ilivyofika ilikuwa nzito sana haina mwendo kabisa. Baada ya uchunguzi ilionekana kabureta imepasuka engine haipati fuel ya kutosha.

Baada ya kubadili kabureta na gearbox oil (hydraulic original from Toyota); aisee gari kama mpya! Since then huu ni mwaka wa pili iko safi sana. Ukigusa accelerator inapotea vibaya sana. Ila kitu kimoja nazingatia - service kwa wakati na engine oil za kueleweka.
 
... Mkuu umegusa penyewe! Ya kwangu ni the same model (D4-1AZ) niliagiza mwenyewe. Hebu fafanua kidogo Kiongozi; zina shida gani hasa hizo engine!

Shida hapa watu wengi hawazingatii service hivyo engine kama hiyo kuchukua kwa mtu itakunyayasa, zinaweza zikakutoka sana hela.


Baada ya uchunguzi ilionekana kabureta imepasuka engine haipati fuel ya kutosha.
Kabureta?
 
Shida hapa watu wengi hawazingatii service hivyo engine kama hiyo kuchukua kwa mtu itakunyayasa, zinaweza zikakutoka sana hela.



Kabureta?
Mkuu haya ma-technical jargon yenu sometimes mnatuchanganya; ni pipe fulani hivi inapeleka petrol kwenye engine; ina-interface na engine directly.

Naomba kuuliza, ni advantages zipi D4-1AZ inazo over the other models; na ni hasara zipi inazo. Thanks.
 

D4 ni nzuri inakupa more power huku ikitumia mafuta kidogo zaidi.

Mfano D4 kama hiyo yako inakupa power inayokaribiana na 2AZ ambayo ina Cc2360 huku ikitumia mafuta kama 1ZZ ambayo ina 1790Cc au hata chini ya hapo.

D4 yanaingia mafuta kidogo direct af yanagandamizwa sana halafu yakilipuka inatoka nguvu kubwa.



Ila kiboko ya Zote ni Technology ya Skyactiv ya Mazda.

Ukikuta mazda ina hiyo Tech inatumia mafuta kidogo sana. Yaani wameitengeneza engine ya petrol ifanye kazi kama engine ya diesel na wamefanikiwa.
 
... shukrani Mkuu kwa ushauri wa bure ambao tulipaswa kuulipia. "Fundi Maiko" alinishauri niwe naweka treatment kila mara; is that OK? Nisije nikawa naharibu engine kwa ushauri wa vijiweni. Asante sana.
 
Mkuu upo na uku? Safi sana uwa napitia sana tweets zako
 
Audi A4 ni gari nzuri sna sema sipendekezi mtu aje kununua zilizotembea over 50k miles maana naona gari nyingi used zinazokuja bongo hazijagi na service records, zaidi ya tag unazokuta kwny engine component zilizobadilishwa, na zinaandikwa kwa kijapan unless umeibeba kutoka stock za UK. Na pia zikishavuka kwenye hio milestone ndo zinaanza uchawi wakuwa na defective sensors na oil consumption issues. To be on the safe side bora kupurchase Audi A4 zenye facelift, maana zilifanyiwa marekebisho kwny common problems kma kunywa oil na pump issues zilizokua common kwny matoleo ya zamani. All in all ni gari tamu kama mfuko unaruhusu🤙🏾
 
Utazijuaje Sasa kuwa hii ndio nzuri kununua Elivate

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…