Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Mkuu Tume ya Katiba huyu pengo kweli ni mnafiki sana, kashapata mgawo wa Escrow, hakuna jina jingine la kuitwa zaidi ya mpuuzi, kwanza Pengo hamuwezi Gwajima kwa lolote lile hata kifedha.

CCM yenyewe inakodi vyombo vya kupigia kampeni kwa Gwajma alafu ndo watamuweza?

Alichosema Gwajma ndiyo ukristo huo unavyofundisha, hata yesu aliwaita wafalme wa roma na mafarsayo kuwa ni mbweha na wapumbavu.

Kula like laki 8! Unafikiunafiki wa waafrika kutokuambiana ukweli ndiyo umetufikisha hapa!
 
kuna crip ndefu ya Gwajima ambayo ndio inakuja kuunga hapo alipo muanzia pengo lkn ilianzia ktk kuichambua mahakama ya kadhi ndio akamtolea tamko pengo..

<<<<<AUDIO>>>>
 

Attachments

Mkuu Tume ya Katiba huyu pengo kweli ni mnafiki sana, kashapata mgawo wa Escrow, hakuna jina jingine la kuitwa zaidi ya mpuuzi, kwanza Pengo hamuwezi Gwajima kwa lolote lile hata kifedha.
CCM yenyewe inakodi vyombo vya kupigia kampeni kwa Gwajma alafu ndo watamuweza?
Alichosema Gwajma ndiyo ukristo huo unavyofundisha, hata yesu aliwaita wafalme wa roma na mafarsayo kuwa ni mbweha na wapumbavu.

Pengo ni nani kwani, si mwanadamu tuu kama wanadamu wengine walivyo, isipokuwa yeye anakula na CCM.
 
Last edited by a moderator:
Pengo baada ya kuanza kutetea katiba ya ccm hata nilimdharau sana ila Gwajima amempa makavu live safi sana

Babu zima limeambiwa linavaa pampers! loh limelewa wines linasahau watanzania wanavomaskinishwa na watawala waovu!
 
Wakuu rudini juu muone nimetuma crip 2 ndefu moja ni hyo ambayo inaunga katika ujumbe wa pengo lkn ilianza mbali sana alikuwa anaielezea mahakama ya kadhi jaa ndio akaja na pengo
 
Tatizo watu wametekwa na siasa, hawataki kuambiwa ukweli hata kidogo.

Mahaba ya siasa ndio yanayowafanya wamtukane Pengo na kuona kakosea alichokisema. Pengo kama mkuu wa kanisa katoliki Tanzania hawezi kuona mambo yanaenda kinyume halafu akakaa kimya, haiwezekani.

Kanisa halijafikia hatua ya kufanya maamuzi kwa niaba ya waumini wake, kanisa halijafikia hatua ya kulamisha watu katika suala linalohitaji haki na uhuru wa mtu. Kumwambia mtu lazima akapige kura ya hapana hiyo si sawa hata kidogo, na hata kumwambia mtu lazima akapige kura ya ndiyo nayo si sawa hata kidogo.

Mtu anapaswa kupiga kura kwa mujibu wa maamuzi na matakwa yake binafsi na si kulazimishwa. Ni sahaihi kuwaelimisha watu manzuri na mabaya ya katiba pendekezwa lakini si sahihi kuwapangia watu kura ya kupiga.

Mkuu uhuru una mipaka yake. Kanisa lina jukumu kuwaelimisha waumini ni kitu gani ni kibaya na kipi ni kizuri. Pengo anajua kabisa hiyo katiba pendekezwa haikupatikana kihalali.

Anajua kabisa hila zilitendeka na hivyo hiyo katiba ni haramu. Inakuwaje awape uhuru kondoo wake wakubali kitu haramu? Anatakiwa kuwa mkweli na kuwaambia kuwa hiyo katiba haikupatikana kihalali na hivyo ni dhambi kuikubali.

Ila siungi mkono matusi ya Gwajima.
 
Alaaniwe kabisa, kwanza tumeshamjua na yeye ni FISADI mwizi wa pesa za waumini wake.

Abarikiwe Gwajima kwa sababu sisi waumini tunamnyonya yeye hatufikishi hata nusu ya fedha ya kuendesha kanisa!
Hajawahi kutukaba wala kutulazimisha kutoa fedha! So maneno yako ya uzushi peleka kwa mumeo!
 
Ha ha ha wahuni wanatukanana hadharani tena kwenye jukwaa la dini eti..

Si amini kama huo ni ustaarabu mzuri tena kwa mtu anaditwa mchungaji ana mtukana mtu anaeitwa kadinari muashamu anatukanwa mbele za watu na mbele ya vyombo vya habari.

Mtukanaji bila kujali wadhifa wa anae mtukana mbaya zaidi hakujali hata umri wa mkombe pengo

Ivi gwajima huo ndio uchungaji na ndio utamaduni wa mtanzania na muafrika?
Ivi baba yako akikosea ingawa sijui mkombe penge alicho kosea sikijui lakini ungewza kumtukana baba yako hivyo??
 
Safi Sana, huwezi mtumishi wa Mungu kujiunga Kwenye siasa Za kifisadi Za CCM, hasa kushawishi waumini kupiga Kura ya ndio hawa ndo wale wale majizi ya escrow na account Zao Za mkombozi bank
 
Ngwajima ni rafiki wa Slaa na Josephine...msimamo wa Ngwajima unafanana na wa UKAWA..

Matusi ya Ngwajima yana fanana na ya baadhi ya vijana wa Bavicha hasa Crashwise CHADEMA KWANZA na parameter...
 
Last edited by a moderator:
Safi sana Askofu mzima tena katibu wa maaskofo unasema kinyume na wezako wakati umesaini lol.Huyu si ndio yule muuza madawa ya kulevya???Kibaraka wa CCM
 
Siungi mkono matusi ya gwajima,lakini pengo nae alichemka mbaya. Anawasema maaskofu kwa kuwambia wananchi wapige kura ya hapana,lakini hakuna hata sehemu moja ya hotuba yake anapoisema serikali kwa kuwafundisha wananchi kupiga kura ya ndio! Hapo ndipo aliponunua matusi.Bora angewasema wote.
 
Wanatamani makafiri (muwe makafiri) kama wao walivyokufuru ,ili wote muwe sawaa (ngoma iwe draw )

Kafir kafir tu hana pointi
 
Mkuu Remote, watu wanachanganya madawa tu. Nitaendelea kuwapiga wasaliti wote hadi dakika ya mwisho. Jitu kama Zitto linastahili kuwa CCM. Chadema tulimvumilia sana

atakua kamsalit mamako mpaka username otherwise utakua unatumwa hata chacha alikufa kabla ya kuthibitishiwa tuhuma....
 
Last edited by a moderator:
Duh hiyo mipasho kama mfokaji wa nyimbo za vigodoro...
 
haya nayo ni mahubiri au mipasho? Tunahitaji busara sana. Siungi mkono alichofanya Pengo. Lakini busara haijifichi,Pengo amepotoka lakini unaweza kuona soni,hekima na busara katika matamshi yake.
Leo hii kila mhubiri akisimama na kuanza kutukana watu anaotofautiana nao mísimamo si itakuwa hatari?

Tuseme ilikua ni lazima kwake 'kuhubiri' alichosema. je hakuna namna angeweza kusema mtazamo wake bila kumtukana Pengo?
 
Back
Top Bottom