Kapwela, kwa maoni yako haya ni wazi huijui Marekani wala siasa zake. Juzi maseneta wa chama cha Upinzani Republican wamemwandikia barua kiongozi Mkuu wa Iran wakimtahadharisha kukaa chonjo na Raisi wao Obama kwa sababu eti haaminiki; je hii ingewezekana Tanzania bila watu kukamatwa na kuwekwa ndani bila kujali nafasi zao ndani ya Upinzani. Mambo yanapofikia hapa ndipo wengine tunapobaki tumeduwaa na kuanza kujiuliza; hivi wengine wetu mnaishi katika sayari gani? Wakati Raisi wao Obama analihutubia taifa, mjumbe moja wa Congress alimwita muongo na hii ilishuhudiwa na wananchi wote waliokuwa wakifuata hotuba hiyo, je itakuwaje siku Kikwete anaitwa muongo live wakati anahutubia taifa kupitia bunge? Hiyo ndiyo Marekani
Kapwela na si hiyo unayofikiria ukiwa kibarazani kwako Kariakoo na kikombe chako cha kahawa.
Haa ha ha sasa isijekuwa wewe ndio umepotoka hulijui hili alafu mie wa Kariakoo na kikombe cha kahawa nalijua hili. Dunia ilivyo sasa unaweza ukawa Kariakoo lakini ukajua siasa za marekani kuliko Mtanzania aliyeko Washington DC, ni information tu.
1. Maseneta wa Republican waliandika barua kwenda Iran waligeuka kituko kwa kufanya jambo ambalo ni la aibu kwao kufanya. Ni jambo la ajabu kufanyika katika utamaduni wa siasa za Marekani, na waliumia kisiasa kwa kitendo hicho, Wamarekani wengi walichukiza na kitendo hicho cha fedhea kwa nchi yao.
Refer:
http://www.huffingtonpost.com/2015/03/12/poll-iran-letter-inappropriate_n_6857644.html
Na wengine baada ya lawama kuwazidia wengine ilibidi wajitokeze kujilaumu kwa kufanya kitendo hicho
..(Bloomberg) -- At least a few of the Republican senators feeling the backlash from signing an open letter to Iran's leaders are expressing some second thoughts. Amid mounting criticism from allies, home-state editorial boards and colleagues who opted not to sign the missive, U.S. Senator Ron Johnson became the latest Republican to suggest he might do things differently if given another chance.
Sasa unataka Dr Slaa aige kitendo kilichowafedhehesha wananchi wa nchi badala ya kujivunia?
2.Hiyo ya Obama kuambiwa muongo kwenye congress kwani ajabu na tatizo lipo wapi hapo?ni siasa ndani ya nchi. Ila wasingemzomea Rais wao wakiwa Mexico; msingi wa hoja ni kuwa husemi ubaya wa nchi yako nje ya nchi
Otherwise sijui kama umemsoma Mitt Romney hapo chini?hii ndio jadi ya siasa za Marekani, unamsikia kila siku Jeb Bush akimsema Obama kuhusu Israel, lakini akienda ziara nje hutamsikia akimsema Obama, ni ndani ya Marekani tu ndio atamsema.Kama ulikuwa haupo aware na hili fuatilia utajua,huu ni utaratibu wa jadi wa siasa za marekani
Refer hapa: Romney foreign policy attack was disgraceful
Romney foreign policy attack was disgraceful - CNN.com
"Partisanship ought to end at the water's edge" is a longstanding adage of American politics.
Na hapa Romney alikuwa mwangalifu kutosema mabaya na nchi yake;
Mitt Romney meets U.K. leaders ahead of London fundraiser - CBS News
"While I'm on foreign soil, I'm very careful not to be critical of my own government's policies," said the presumptive Republican nominee. "I would be even more remiss if I were to be critical of any other government's policies. I will instead look forward to an exchange of ideas."
TOFAUTI ZA KISIASA ZETU ZIISHIE MPAKANI, NJE YA MPAKA KILA MMOJA AENDE AKIIWAKILISHA TANZANIA,NCHI YETU SOTE, HADHI YA TANZANIA NI MUHIMU ZAIDI KULIKO SIASA ZETU. HUKU NDIO KUKUA KISIASA KUFANYA VINGINEVYO HATUAIBISHI NCHI TU BALI TUNAJIAIBISHA WENYEWE
Mcheck na Obama alivyokuwa bado mpinzani alivyoishika hiyo desturi.
http://politicalticker.blogs.cnn.com/2008/07/25/obama-sidesteps-bush-criticism/comment-page-1/
PARIS, France (CNN) - Sen. Barack Obama said Friday he was avoiding criticizing President Bush on his trip through Europe.
Speaking to reporters, the Democratic presidential candidate cited a tradition that "you don't criticize a sitting president while overseas," adding that "it's very important" that U.S. foreign policy is presented "in one voice."
Sasa kwa kumsoma Romney hapo juu na Obama hapa juu utatambua kuwa ni ulivyodhania sivyo na nilivyosema ndivyo ilivyo.