Mkuu
Planett , naomba ushee nasi hapa kama una lolote la kutujuza... tupe huo mkasa wako kuhusu hiyo knocking sound... ilianzaje? Ilisababishwa na nini? Ulitibu vipi?
Kuhusu my case, background history iko hivi:
Gari niliagiza Japan. Inaelekea kufikisha miaka miwili sasa.
1. Tangu niipokee huwa inapunguza coolant, kwa kiwango kidogo.... hadi sasa (karibia miaka miwili) nimetumia coolant Lita 1 na robo kwaajili ya kuongezea kila inapopungua.
2. Ndani ya mwaka wa kwanza, eksozi iliziba/ilijaa masega na gari kukosa kabisa nguvu mlimani. Tukaondoa masega na power ikarejea vizuri kama awali.
3. Ndani ya mwaka huu wa pili, ikaanza hiyo knocking sound kwenye engene. Knocking hii hutokea pale tu engene ikiwa na full temperature (warmed up) at idle and low rpm. Yaani engene inapokuwa fully warmed up na ukasimama at idle ndipo hiyo knocking sound inaanza, na ukiendesha knock inakuwepo at low rpm only, mwisho rpm 1,200 knocking inapotea. Kwenye cold start knocking sound haipo kabisa, ni mpaka engene inapokuwa fully hot.
4. Hivi karibuni, services mbili zilizopita, oil imeanza kupungua kwa kiwango kidoooogo sana. Pia jana nimeona mfuniko wa kwenye engene oil unachafuka, yaani pembezoni mwa mfuniko kuna unyevu nyevu wa oil kama kuvujia vile. Hii hali ndo nimeiona jana kwa mara ya kwanza.
Gari naona bado inakimbia vizuri. Service nazingatia kwa wakati, na plag natumia denso iridium genuine.