Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!

Hivi Mrema alifanya kipi cha maana haswa maanake mimi sielewi?..
Your Answers:
1. He was the first Minister to catch a bust of Gold belonging to the President spuase and telling the President I can't bow! "You're corrupt". And he quit his position as a Deputy Prime Minister!
2. What did Mkapa or Kikwete achieve before being a President? At least we saw what Mkapa did, the macros, the country was in shit before him. What does this present guy doing what Mrema couldn't accomplish?
3. WE are judging the guy; but we fail to know in a country like Tanzania, if at that time Mwl Nyerere had backed Mr. Mrema then he could be our President.
There are more factors than these factors; we in Tanzania are in a different world, and don't forget we are in Africa.
 


Rev. Kishoka:

Si kweli kabisa kuwa waafrika wanapenda prestige za USOMI. Kumbuka kuwa Mrema alikuwa mbunge wa kuchaguliwa. Na kama sikosehi alikuwa mbunge wa Kutoka mkoa wa Kilimanjaro.

Kilimanjaro ni mkoa unaongoza kwa kutoa wasomi. Lakini pamoja na hayo alichaguliwa kuwa mbunge.

Mzee Mwinyi naye hakuogopa kumpa uwaziri wa mambo ya ndani. Hivyo, ndugu Mrema alikuwa one step away kuwa President.

Kwa mujibu wa katiba yetu. Waziri mkuu, spika na mawaziri ni wabunge. Na mbunge yoyote yupo karibu sana na kushika madaraka ya uwaziri mkuu, uspika, uwaziri mpaka urais. Kichotakiwa ni bahati, jinsi ya kuchanga karata na personality.

Mrema ana strength zake kama charisma na guts. Lakini ana kasoro zake kama kutokuwa msikivu, kutofuata ushauri, kutokuwa na elimu.

Na kwa kipindi alichokuwa maarufu alishindwa tools za ku-minimize weakness zake.
 


So after all he needed Nyerere's backing to become president.
 

FMES,

Wewe unakaa Marekani, kwa nini presure groups kama Moveon. Org, na watu kama Rush Limbaugh, Glenn Beck, Bill Maher, Chris Matthews, Bill O'Reily wana msukumo wa nguvu kiasi cha kuangusha Wabunge wa Marekani hata Rais wa Marekani halafu udai kuwa JF haina nguvu hizo au kuainisha kuwa Tanzania ni Mbuge pekee mwenye uwezo?

Hivi leo hii tukiachana na mapenzi yetu kwa watu fulani fulani na uanza kuwadai uwajibikaji mmoja mmoja na kwenda majimboni mwao, unafikiri ni nini kitatokea?

Wabunge wa Tanzania hawana watu ambao ni diversed pool of brains kama JF ilivyo. Hapa you name it, kila watu wapo na wanaweza kumpangia mtu strategy nzuri sana.

Kama huamini, chunguza vizuri sana SSM na Serikali yake pamoja na kujifanya wanachukia JF. Wengi wao wanajifunza hapa kutoka kwa Wana JF mbalimbali hata kama mara ingine tunamwaga upupu. Guess what, CCM wamepevuka kwa kusoma nyakati na kutumia kinachosemwa humu kujijenga.

Upinzani ambao ulitarajiwa uwe upande mmoja na JF kwa kuwa lengo ni kukosoa Serikali, wao badala ya kufanya transformation na kutumia strategies na ideas zinazomwagwa humu ndani, wamebakia na Ubuntu wa kujiona wao ni mali na ndio maana wanapigwa mweleka kila mara especially CHADEMA!

So do not under estimate our power and our strength, maana kama si sisi, hao Wapiganaji wasingekuwa na ammo za kupigana!

Hivyo basi, kama Rush Limbaugh na Bill Maher, sisi huku ndani ambao tunaona mambo yankwenda kinyume na inavyopaswa kufanyika na kule kujivutavuta kisa eti bado nchi changa, iko siku tutachoshwa kutumiwa na na kunyonywa juhudi zetu za kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu uajibikaji na rurawageukia hao wawakilishi majimboni mwao na kuwahoji wamefanya nini la maana tangu wapewe kura za wananchi kuleta maendeleo majimboni mwao.

Nimesema katika vita hii, kama Wapiganaji wanataka kufanikiwa, kwanza ni kumjengea Mtanzania mazingira ya kuwa huru kwa kusukuma maendeleo yatakayoinua hali ya maisha ya Mtanzania ambaye akishaweza kujitegemea na kuridhika, atapanuka mawazo na kuweza kuachana na woga na unyonge wa kuwa mtegemezi wa misaada na hongo na ataamua kwa haki na utu ni nani anafaa kupata kura yake na si nani aliyeleta Pilau na Gagulo!
 

Katiba ya Tanzania inasema mtu anaweza kuwa Rais kama anajua kusoma na kuandika, na hi ni kutokana na kuwa na sifa za kuwa mbunge haisemi lolote kiwango cha elimu!


So elimu ya juu is a plus but not a requirement per Katiba. CCM that was their preference kubadili katiba na kudai lazima mtu awe na Shahada ya chuo, na guess what, kila mtu kajiendea hata katika vyuo tunavyodai kuwa havina credibility na wamejipatia Shahada mpaka Udaktari!

Hata wewe na mimi na Bwana Mkandara tunaweza kuwa Rais wa Tanzania. Tunachohitaji kuwa nacho ni uwezo wa kuwa watu wa haki na kufuata kanuni (this does not need PHD), zaidi tuwe na busara, hekima, unyenyekevu na wachapakazi (this also does not need a degree).

Maamuzi hufanywa kwa kuaminiana. Ndio maana Rais ana washauri na wasaidizi katika kila nyanja, Sheria, Uchumi, Afya, Siasa, Utamaduni, Biashara, Utawala, Demokrasia, Ulinzi na Usalama na mengineyo.

Kila Rais wa Tanzania ana watu hao ambao ni wataalamu kisomi wa fani hizo, ambao wako kwenye ofisi yake, halafu kuna watendaji wa kazi ambao ni Mawaziri ambao ni Wanasiasa kama Rais, nao wana Makatibu wakuu, wakurugenzi na wafanyakazi wengine ambao ni wasomi na wana utaalamu katika fani zao kutimiliza majukumu na kazi zao.

Narudia kuuliza, kama Elimu ya Chuo Kikuu ni tija, kwa nini mfupa umemshinda Mkapa na Kikwete?

Kama katika mwaka wa Kwanza wa Mchumi Kikwete aliamua kuongeza ukubwa wa Serikali kama njia ya kutoa shukrani kwa kisingizio cha kuleta usawa wa kikabila, kimkoa na kidini ndani ya Baraza la Mawaziri na hivyo kuongeza gharama na matumizi, je Uchumi na usomi wake ulikuwa na maana gani?

Na si hilo tuu la gharama na matumizi, bali kukosekana kwa juhudi za kuhakikisha kuna uchapakazi na uwajibikaji.

Ikiwa mchumi kama yeye anadai kuwa hajui kwa nini Tanzania ni masikini, je Usomi wake una maana gani ikiwa Mdengereko na Mfipa wakiangalia mbingu wakaona anga halina mawingu wanajua kuwa hakuta kuwa na mvua na hivyo mavuno yatakuwa haba?
 
3. WE are judging the guy; but we fail to know in a country like Tanzania, if at that time Mwl Nyerere had backed Mr. Mrema then he could be our President.

God forbid! Na kwa hili daima nitamshukuru Nyerere.

Amandla........
 
Mkuu FMES respect...unajuwa walioibua suala la miakataba kusainiwa hotelini ni mashujaa wa upinzani wakiongozwa na dr slaaa, pamoja na mashujaa wa hapa JF....Waliotoa intelligence support and doziers...

Alichofanya kikwete ni kutumia akili ya kisiasa ...waswahili tunasema ,mchawi mpe mwana alee....,".... alimteua mmoja ya wapinzani aliyeshiriki kuwasulubu bungeni zittt kabwe....nadhani pale kikwete alitaka kuizima hii hoja kisiasa ..na ndio maana hoja ya buzwagi ni kama imekufa ....na utekelezaji wa ripoti ya jaji bomani hatuuelewi...., na wapinzani kuliongelea hawawezi tena ....kwani waziri atawapa jibu rahisi..."vuteni subira ...mlikuwa na wawakilishi wawili kwenye tume ya jaji ,...,waulizeni.

Hawa wapiganaji wa ccm ...ukweli ni kuwa wanapigwa vita sana ndani ya chama hata jk amekiri ...lakini wana ccm lazima kuelewa kuwa kama si wapiganaji hawa kupaza sauti wakiwa ndani basi CCM ilikuwa inakenda na maji .....kwani angalau sasa wananchi waeona kuwa kumbe hata ccm kuna wabunge wanawatetea...ndio maana upepo uendavyo kisiasa inaonekana kundi la mafisadi tayari limemtuma makamba kufanya ziara ya kuomba suluhu kwenye majimbo ya wapiganaji yaliyochafuliwa kama kwa sitta......ba kinafiki amewaomba wana tabora wahakikishe spika sitta anarudi bungeni na kumsifu kwingi.....tukielekea mwaka 2010 ...nadhani hata ..dizaini ya yule mbunge wa kigoma mjini wa ccm na wenzake wa aina hiyo chamani ambao wazi wanajulikana ni pro ufisadi ...watakiunga na vita ya kupinga ufisadi ili wawe na ajenda ya kushinda......mwakani ....
 

Lula aliikuta nchi ikiwa tayari iko juu!

Eva Morales- the jury is still out.

Usomi ukitumika vizuri una faida yake. Lee Kuan Yew wa Singapore ni mfano. Shule inasaidia lakini si panacea.

Tunahitaji mtu mwenye vision, mwenye committment, mwenye integrity, mwenye empathy. Mtu ambae anaweza kutuambia na tukamuelewa ukweli kuhusu hapo tulipo na mtu atakaetuonyesha kwa vitendo kuwa sote tunaweza kutoka hapo tulipo. Hajapatikana bado huyo mtu.

Amandla........
 
Naomba kutoa hoja.

Hapa tuna demokrasia moja nzuri kabla ya vijembe kuanza na laiti vyama vyeetu vya siasa vikianza kutuiga kwa kuruhusu majadiliano ndani yao katiya wanachama wao yawe kama sisi.

Naomba kufafanua: Nimemleta Mrema na nimemjengea hoja na natetea hoja yangu. Kuna wanaounga mkono na kuna wanaopinga. Hii ni demokrasia.

Wanaounga mkono wanatoa sababu zao, wanaopinga wanatoa sababu zao, huu ni utaratibu mzuri na uungwana.

Sasa basi, ombi langu kwa wale wanaopinga na kusema Mrema hafai, naomba watupe majina ya watu wanaofikiri kwa mtazamo wao kuwa wanafaa kutuongoza au ni "Wazalendo" na Wapiganaji wa kweli, ili tuweze kuwachambua na kuwapima uwezo wao kuongoza.
 
FMES,

Naomba kurudi nyuma kwenye swali moja nililokuuliza na ukanijibu.

Niliuliza
Ukajibu
 
 
 
 
 

Rev Kishoka:

Huu sio ushabiki wa mpira kwamba kama nafasi nzuri aliyoshindwa Zamoyoni Mogella kufunga goli, basi Kibadeni angeweza.

Hivyo mjadala ni kuhusu Mrema. Na tunamjadili kuhusiana na nafasi zake alizowahi kushika, jinsi alivyo-capitalize hizo nafasi, mchango wake kwa taifa na pale alipo sasa.

Wengi wetu tunaopinga AUGUSTINO LYATONGA MREMA, hatufanyi hivyo kwa sababu kuna kiongozi anayefanya kazi nzuri kuliko MREMA. Na vilevile hatufanyi hivyo kutafuta KIONGOZI MWINGINE mwenye sifa za MREMA.

Wengi wetu tumefikia kwenye conclusion kuwa juhudi za kufatuta kiongozi ambaye atakuwa na charisma na guts za MREMA, au kiongozi hatakayekuwa sio fisadi kwa hiari kama NYERERE, hazisaidia taifa in long terms.

In long term, taifa ni lazima liwe na system nzuri ya utawala wa kikatiba ambao utamwezesha hata asiye na Elimu kutawala kama Professor. Na Fisadi kuongoza kama malaika.
 
Rev Kishoka:

In long term, taifa ni lazima liwe na system nzuri ya utawala wa kikatiba ambao utamwezesha hata asiye na Elimu kutawala kama Professor. Na Fisadi kuongoza kama malaika.
That is the best quote of the day. Kama alivyosema Obama Ghana, Africa does not need strong men. It needs strong institutions.
 
Interesting Observer,
Your Answers:
1. He was the first Minister to catch a bust of Gold belonging to the President spuase and telling the President I can't bow! "You're corrupt". And he quit his position as a Deputy Prime Minister!

Mkuu Unajua hakuna kitu kibaya duniani kama kutunga vitu...Umezungumzia Mrema kwa sifa ambazo hazikuwepo hata kidogo...huu ni uzushi mkubwa kwa sababu Mrema hakujiuzuru toka Deputy Prime Minister...Mrema baada ya hapo alipelekwa wizara ya kazi (1994-95)ambako alifanya kazi kwa mwaka..sielewi hii habari ya kujiuzuru kwake umeitoa wapi! Mrema kaondoka CCM ama uongozi mwaka 1995 kujiunga na NCCR, mwaka ambao Mwinyi alikuwa anamalizia ngwe zake iweje leo wewe uje hapa na story za kutunga ati alimwambia Mwinyi hawezi ku bow!..
Je, sii huyu Mrema aliyekwenda Butiama kumwona Nyerere kabla hajajitoa CCM na kujiunga na NCCR Mageuzi? au Mrema mwingine! Why ikiwa kweli alikuwa na msimamo wake binafsi why kwenda kumwona Nyerere Butiama kupata baraka zake!
Mkuu sisi watoto wa mjini tunayajua mengi yalliyofanyika mjini pale wakati wa Mrema ambayo wewe huyajui na wala hutayajua.. Akiwa Waziri wizara ya mambo ya ndani, Airport yetu ilikuwa pathway ya magendo yote unayoweza kufiiiria wewe tena inasemekamna hata mkewe Mwinyi aliingia biashara haramu.. Nani sitamtaja hapa kwani sina ushahidi mkononi..
 
- Bob ndio maana nilisema hivi in the absence of mashujaa, labda Mrema ndio anaweza kuwa shujaa. I mean alijiuzulu cheo ambacho hakitambuliwi na katiba ya Jamhuri?

- Sasa unaona madhara ya kukosa elimu, angekua nayo walipompa angekataa kwamba siwezi kushika cheo kisichokuwepo kwenye katiba, lakini yeye akakkubali tu tena bila hata kuapishwa na rais, kwamba yeye ni naibu waziri mkuu, no wonder Msuya waziri mkuu mpya alikifuta bila kumfahamisha.


Respect.

FMEs!
 

mkuu hata salim ambaye mimi binafsi namuheshimu na namuona kama ndiye aliyestahili kuitwa rais leo...alipata kupewa na mwinyi cheo cha NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA ULINZI [CHINI YA WARIOBA]...KABLA HAJAENDA OAU...na hakukataa ..

kukikubali hicho cheo ni heshima tu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…