Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!


Tayari una muhukumu Mrema kwa mambo amabayo unadhani yangetokea...Pathetic!Yani unasema kuwa mtu huyu hafai kwasababu nadhani angefanya hivi...What a great thinker!
 
 

Mkuu JMushi

Uko juu sana pengine hii inaweza kuwa ni faida ya kuwa na hili jukwaa.
Wananchi wamelishwa propaganda mpaka wamekubali upuuzi wa wanasiasa ambao wakati wanamsakama Bwana Mrema kwa kila aina ya misamiati hatimaye muda umekuja kuwaumbua jinsi walivyolifilisi taifa.

Tanzania ya leo inamuhitaji sana Bwana Mrema kuikwamua katika tope la ufisadi.Tunahitaji migodi yetu ina inayotoa dhahabu nzuri ianze kunufaisha taifa.Tunahitaji mafisadi wote wafikishwe mahakamani bila kujali kama ni wajumbe wa NEC au CC.Tunahitaji kuona viongozi wa ngazi mbali mbali wanafuata sheria na taratibu.Tunahitaji kuwa na Rais atakayetumia muda wake mwingi kushughulikia matatizo ya wananchi wake badala ya kuzurura ughaibuni.Tunahitaji kuwa na sheria kali dhidi ya wahujumu uchumi ikiwezekana adhabu ya kifo kama walivyo ndugu zetu wachina.

Viongozi wa zamani ambao bado wako kwenye system kama J malechela,Kingunge,Makweta na wengineo wengi wanatakiwa kupumzika kupisha damu changa kwakuwa mchango wao katika ujenzi wa taifa ni mdogo sana au haujapata kuonekana kabisa.Hawa kwa kiasi kikubwa wanachangia kuendeleza system mbovu.Haiwezekani kiongozi umekaa kwenye system kwa zaidi ya miongo mitatu huna kitu/mark unachoweza kuwaeleza watanzania.
 
Mfano mzuri uko kwa magufuli, amejaribu kung'ara kwenye wizara ya ujenzi, kungia ardhi imekuwa kinyume ameuzia nyumba ndugu zake, kuna uwezekana hata Lyatonga angefanya hivyo.

Hivi Maghufuli ameuza nyumba hata alipokuwa wizara ya ardhi?
Amandla.....
 
 
 
 
 
Phillemon Mikael said:
ni kweli mwambie MKULU FMES..



Philemon Mikael,

..nadhani kuna mambo umeyaacha hapo ktk kuelezea matukio yaliyopelekea Mrema kufukuzwa kazi na Raisi Mwinyi.

..Mrema alikiuka utaratibu wa Collective Responsibility ktk baraza la Mawaziri baada ya kupingana na msimamo wa serikali ndani ya kikao cha Bunge.

..serikali ilikuwa inajaribu kulizima suala la kashfa ya ununuzi wa mashamba ya mkonge uliofanywa na mfanyabiashara anayeitwa Chavda.

..kwa mtu anayeelewa jinsi serikali inavyofanya kazi lazima angejua kwamba kilichokuwa kinafuatia baada ya hotuba ya Mrema bungeni ni kufukuzwa kazi tu. hata Mrema mwenyewe alijua kwamba atafukuzwa kazi na alieleza ndani ya bunge kwamba yuko tayari kwa lolote.

..Isaac Mruma ambaye alikuwa mwandishi wa habari wa Malecela,Msuya,na baadaye Sumaye, aliandika makala nzuri sana kuhusu matukio yaliyopelekea Mrema kufukuzwa kazi. tena aliandika kama mwandishi wa habari wa Waziri Mkuu, jirani ya Mrema wakati wakiwa Dodoma, na zaidi mtani wake wa kikabila.

..siku aliyotofautiana na serikali bungeni, Mrema alilalamikia mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na kuandikiwa barua na mwanasheria mkuu wa serikali akielezwa kwamba cheo cha Naibu Waziri Mkuu kilikuwa hakipo kwenye Katiba na hakitambuliwi Kisheria.


..kwa mtizamo wangu nadhani Mrema alikuwa frustrated na kuondolewa kwake Wizara ya Mambo ya ndani na kuhamishiwa Wizara ya Kazi.

..kitendo cha Raisi Mwinyi kumruka "Naibu Waziri Mkuu" Mrema ktk kuziba nafasi iliyoachwa na Cygwiyemwisi John Malecela nacho kilikuwa kielelezo machoni mwa Mrema kwamba Mzee Mwinyi alikuwa hana imani naye.

..CCM waliweka masharti kwamba mgombea wao wa Uraisi lazima awe na shahada ya Chuo kikuu.

..kwa mtizamo wangu, Mrema alikuwa anataka kuwa Raisi, na wakubwa wenzake CCM walikuwa hawana nia ya kumpa nafasi agombee.
 

Zakumi,

..wananchi wanafikiri kwa system yetu ya Tanzania Raisi wa ajabu-ajabu anaweza kudhibitiwa na wasaidizi au washauri wake.

..Mrema aliendelea na tabia yake ya kudharau sheria na taratibu, hata baada ya kupewa naibu waziri mwenye utalaamu wa sheria Jaji Edward Mwesiumo.

..NCCR nao walidhani wanaweza kumrekebisha Mrema kwa kumteua Prof.Mwesiga Baregu kuwa msaidizi wake. mwisho wa ndoa ya NCCR na Mrema ilikuwa ni chama kusambaratika.
 
Mrema ana matatizo yake lakini sioni kama yanaingiliana na kabila lake.

Yanahusiana kabisa maana wachaga wengi wako hivyo, hawataki kushindwa wala kuwa chini ya wengine ndo maana asilimia kubwa ya watuhumiwa wa ufisadi ni wachaga. Meza kama ilivyo ukitaka data sema tukuangushia. Mrema kama walivyo wachaga wengine walipata wasaa wa kushika madaraka wamekuwa hivyo....Mengi, Mbowe, Mrema, Mgonja, Mramba, Yona n.k. wote hovyo kabisa
 

Hivi Mgonja mchaga? Yale yale! Hatuwezi kumjadili mtu bila kuingiza kabila au rangi yake.

Amandla......
 


ukichukia watu kupita kiasi ..ndio unawapa catalyst ya kusonga mbele .....[catalyst change the speed of the chemical reaction but it self remain unchanged at the end of the reaction]....all haters ...you are just the catalyst....na mtabaki hivyo hivyo....asilani!!!!

Tupendane watanzania!!!
 
FMES...MZEE mwinyi alisema "kila zama na kitabu chake" ,zama za mrema zimepita ..na sioni mantiki ya kumfananisha na viongozi wa sasa ...kwani zaidi labda ya ubunge hakuna nafasi zaidi ya hiyo anaweza kustahili...kifupi hana nafasi ya kugombea urais tena!!!

ni ukweli usio kificho kuwa ukitaja viongozi watatu maarufu [of all the time ] kisiasa miongoni mwa wananchi ...basi mrema,sokoine na nyerere ndio watakaotajwa....tofautisha list hiyo na uamue kuandaa viongozi bora kabisa ...wenye busara kitaifa[wenye busara si lazima wapendwe na wananchi]...ambapo hapo unaweza kumpata tena nyerere,salim,malecela,warioba,mkapa,mwinyi etc........kikwete hapo aingii yeye atakuwa anaingia kwenye kundi la kwanza la popular leaders....na anaweza kuwa chini ya mrema kwenye list ya viongozi waliopata kupendwa na watanzania..[populist]

kwa hiyo napingana na wewe kufananisha mrema na wapiganaji wa sasa kama slaa,zitto ,mbowe na wale wa ccm...kila kitu na wakati wake...wakati wake umekwisha,lakini kubalini kuwa wakati mrema anaapigana na ufisadi enzi zile....watu walikuwa hawamuelewi kama wananchi sasa wanavyoanza kuellewa...enzi zile walikuwa wakimshabikia kama mpira kuliko kumsikiliza ...na hili mwalimu aliliona ,...ndio maana alikuwa akiwaambia serikali wasimchape au kumpiga mabomu...maana ilikuwa kama kuwaamsha wananchi!!!

ni wazi kuwa heshima ya mrema kwenye siasa za nchi hii au legacy yake ipo,na kwa kuwa sasa sio tishio hakuna haja kuogopa kumkiri....hakuna kiongozi aliyepata kuigharimu CCM na idara ya usalama pesa kummaliza kama mrema...kuna watu wamekuwa mabilionia ..just kwa ku hold budget vote ya kummaliza mrema....na wengine iliwagharimu maisha just kwa kushindwa kumdhibiti.....ikabidi wapate "court marshall assasin"!!

kwa kuwa amezeeka na afya yake sio nzuri ..si vema kusubiri vinginevyo kuikiri legacy yake...pande zote !
 

Wajibu wa kuwa na Washauri na Wasaidizi ni nini?

Mshazoea ya yule mmoja kati ya Mamilioni Nyerere, aliyewaza, tafakari kuota na kisha kuhakikisha linafanyika ndiyo maana tunatafuta mtu aliye na sifa zote.

Mwinyi, Mkapa na Kikwete, pamoja na usomi wao, walikuwa na wana washauri.

Tatizo la Tanzania ni mfumo mbovu na Katiba chovu ambayo inafanya Serikali Kuu ijiamini kupita kiasi na kufanya kazi kama Mungu na kudharau Bunge na Mahakama.

Leo ukimweka Rais wa Tanzania katika mfumo huru ambao Bunge na Mahakama vinaweza kumpinga bila kutishiana na kuwekeana vikao vya Chama, tunaweza kufika mbali sana.

Ni mara moja tuu, katika historia yetu ambapo Kiongozi wa Serikali Bungeni alithubutu kulipa nguvu Bunge kwa kutumia Demokrasia na uamuzi wake huu uliishia yeye kuwekwa kati kwenye vikao vya chama, akavuliwa madaraka, akaandikiwa kitabu na akawekewa doa la milele kwenye paji la kuwa kamwe hataachiwa awe Rais wa Tanzania.
 
 
Lula wa Brazil si msomi, na nchi yake iko katika nchi kumi zenye uchumi bora duniani.

Eva Morales wa Bolivia si msomi lakini anaendesha nchi na kinaeleweka.

Ni Waafrika pekee tunaopenda Prestige za Usomi kama vile ni tija na njia ya kuleta maendeleo!
 
 
hakuna kitu kinaniuma kama makampuni ya dhahabu yanavyotufanyia umafia ile nchi uliobarikiwa na mafia wa CCM,yaani siamini kama Serikali yetu ni incompetent/mafisadi kiasi kile...tunahitaji mapinduzi ili vizazi vijavyo viweze kuishi vizuri!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…