Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!

Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!

So unataka kuniambia kuna sera yoyote ya kulinda ufisadi inayotekelezwa sasa na serikali, kwenye ilani ya CCM? Hii ni sera inayitekelezwa lakini haipo kwenye manifesto. Sera za chama zinatengenezwa na nani, na wanachama au zinajitengeneza zenyewe?
Kwa hiyo kiongozi anaweza kuja na policy suggestion ambayo inaweza kuja kuwa sera, au akatawala kwa decree, kama mrema alivyokuwa antoa siku saba kwa watendaji wa serikali. Angekuwa rais angekuwa mtawala wa kiimla na sio wa sheria au anayeongozwa na sera.

Kama kazi yake ilikuwa kukamata wezi angeenda wizara ya nishati angeshindwa, kwa sababu nishati hawakamati wezi, isipokuwa wanashughulikia mambo ya nishati, ku explore vyanzo vipya vya nishati, kunahitaji innovation capabities and alike.
Nilikuwa na uhakika kuwa Ben Mkapa akiingia madarakani ataweza kustabilize uchumi na kupunguza inflation, which he did. Nilidhani kuwa atapigana na rushwa i was wrong.
Kwa hiyo inawezekana kabisa kuwa you are wrong on what you think about Lyatonga.
Mfano mzuri uko kwa magufuli, amejaribu kung'ara kwenye wizara ya ujenzi, kungia ardhi imekuwa kinyume ameuzia nyumba ndugu zake, kuna uwezekana hata Lyatonga angefanya hivyo.

Tayari una muhukumu Mrema kwa mambo amabayo unadhani yangetokea...Pathetic!Yani unasema kuwa mtu huyu hafai kwasababu nadhani angefanya hivi...What a great thinker!
 
- Mushi kwani ni nini hasa maana ya siasa? Na nini hasa kazi ya vyama vya siasa?



- Again bado hata hii quote, ina fall kwenye maswali yale yale kwamba what is politics na hasa kazi ya vyama vya siasa? Majibu ya haya maswali yanaweza kukupa mwanga on what is political propaganda hasa wakati wa kampeni za uchaguzi wa kisiasa, and how the political campaigns are won and lost.

- Sasa think kwamba wewe mwenye elimu kubwa bado una tatizo ku-grasp hizi meaning, sasa kwa mtu kama Mrema inakuwaje? Kwani Mrema angeshindwa nini kusoma Degree akiwa waziri, au hata baada akiwa ndani ya CCM ili kukata mzizi wa fitina? ndio tunakwambia mkuu elimu ndogo haiwezi kuwa covered na anything zaidi tu ya maamuzi finyu na empty.

Respect.

FMEs!

Tukienda step by step tutaelewana,na pia tukiacha ushabiki na maneno ya kejeli.
Mambo mengi ya kisiasa tunayoyafanya sasa hivi ni nje ya hatua ya kijamii tuliyoifikia...Huwezi kutaka profesa aende kufundisha vidudu!Na pia mechanism tunazotumia hazitunufaishi bali zinazidi kutudidimiza. Ni kama vile tunavyoingia kwenye ubepari kabla ya kuvuka stage nyingine zote ambapo stage ya kwanza ni ujima! Huwezi kuoongeza unga kabla uji haujatokota,hii ni kama unajua kupika ugali.

Nimesema hapo nyuma kuwa siasa za vyama zimeturudisha nyuma na bado zinatufanya tuwe stagnant...Hatuendi mahali,sio Taifa kwanza ni chama kwanza,na ndio maana nikasema hapo nyuma kuwa viongozi wote wanachaguliwa kwa vigezo vya ukada,ama kuwa kada maarufu zaidi ya uzalendo kwa taifa,hatuna sera za kitaifa zenye mwongozo wa kututoa kwenye umasikini na sheria tulizo nazo ni mbovu hata mwenye kuzivunja anaweza kuwa na justifiable reasons to do so.
Katiba ile ya mkoloni iliyokuwa ya kumkandamiza Mtanganyika ndiyo iliyokuwa adapted na viongozi wetu ended up Black colonialists.

Jamaa yako Zakumi anaponda kuhusu elimu ya Mrema na kufagilia ya Zuma huku akijichanganya kwa kusema kuwa Mrema hafai kwasababu ambazo ukilinganisha na Zuma ni kama usiku na mchana.

Sikatai kuhusu umuhimu wa political propaganda kwenye kugombea madaraka,ila nachohoji ni kuhusu hizo propaganda zenyewe,wakati wenzetu wanatumia political system kuendelea,sisi tunazitumia kurudi nyuma,hapo ndipo kwenye swali uliposhindwa kuelewa,kwamba baada ya siasa zetu kutumika kumng'oa mkoloni,je ni right kwa siasa hizo hizo kutumika kutuondolea wazalendo?Mfano wa Sokoine na Mrema ni wa karibu zaidi...Kwanini kuna watu wanataka tuendelee kucheza kwenye tope tuu?
 
Vigogo na majambazi wa wakati ule ni tofauti na hawa wa sasa? Si ni wale wale? Toauti ni msamiati tu kwani wakati ule waliitwa simply vigogo na sasa ni mafisadi,majambazi ni wale wale ushahidi upo....Inawezekana sisi watanzania tunachukua muda mrefu kutambua....Kumbuka kuwa failure to understand back then is what costs us this time. Matatizo yote aliyokuwa akiyafanyia kazi na kukatishwa tamaa na watu kama nyie ndiyo yamesamiri na kukubuhu hivi sasa na hata kuwaumiza vichwa wapiganaji wengi.
Sasa wezi na vigogo wa wakati ule si ndio hawa wanaotucost wakati huu? Ebu nieleze,hao kina Mramba si ndio aliokuwa akipambana nao?Kina Mkapa? Halafu na hao majambazi unaodai wa wakati ule si ndio hao hao waliomfanya JK aigawe Dar kikanda kwenye idara ya polisi?
Mkuu tumia muda kidogo kufikiri kabla hujaposti,itasaidia sana kwani mnategemewa na wananchi. Say what you think is right bila kujali nani atafikiri nini hapa jamvini.

Mkuu JMushi

Uko juu sana pengine hii inaweza kuwa ni faida ya kuwa na hili jukwaa.
Wananchi wamelishwa propaganda mpaka wamekubali upuuzi wa wanasiasa ambao wakati wanamsakama Bwana Mrema kwa kila aina ya misamiati hatimaye muda umekuja kuwaumbua jinsi walivyolifilisi taifa.

Tanzania ya leo inamuhitaji sana Bwana Mrema kuikwamua katika tope la ufisadi.Tunahitaji migodi yetu ina inayotoa dhahabu nzuri ianze kunufaisha taifa.Tunahitaji mafisadi wote wafikishwe mahakamani bila kujali kama ni wajumbe wa NEC au CC.Tunahitaji kuona viongozi wa ngazi mbali mbali wanafuata sheria na taratibu.Tunahitaji kuwa na Rais atakayetumia muda wake mwingi kushughulikia matatizo ya wananchi wake badala ya kuzurura ughaibuni.Tunahitaji kuwa na sheria kali dhidi ya wahujumu uchumi ikiwezekana adhabu ya kifo kama walivyo ndugu zetu wachina.

Viongozi wa zamani ambao bado wako kwenye system kama J malechela,Kingunge,Makweta na wengineo wengi wanatakiwa kupumzika kupisha damu changa kwakuwa mchango wao katika ujenzi wa taifa ni mdogo sana au haujapata kuonekana kabisa.Hawa kwa kiasi kikubwa wanachangia kuendeleza system mbovu.Haiwezekani kiongozi umekaa kwenye system kwa zaidi ya miongo mitatu huna kitu/mark unachoweza kuwaeleza watanzania.
 
Mfano mzuri uko kwa magufuli, amejaribu kung'ara kwenye wizara ya ujenzi, kungia ardhi imekuwa kinyume ameuzia nyumba ndugu zake, kuna uwezekana hata Lyatonga angefanya hivyo.

Hivi Maghufuli ameuza nyumba hata alipokuwa wizara ya ardhi?
Amandla.....
 
Sikatai kuhusu umuhimu wa political propaganda kwenye kugombea madaraka,ila nachohoji ni kuhusu hizo propaganda zenyewe,wakati wenzetu wanatumia political system kuendelea,sisi tunazitumia kurudi nyuma,hapo ndipo kwenye swali uliposhindwa kuelewa,kwamba baada ya siasa zetu kutumika kumng'oa mkoloni,je ni right kwa siasa hizo hizo kutumika kutuondolea wazalendo?Mfano wa Sokoine na Mrema ni wa karibu zaidi...Kwanini kuna watu wanataka tuendelee kucheza kwenye tope tuu?

- Mkuu hizo system unazoziongelea zimedumu kwa miaka karibu 300 sasa, wakati yetu ni only 45 years old, kumbuka kwamba hata hizo system unazozisema kua saafi zilianzia tulipo sasa, infact zao zilikua even worse, kwa mfano kule US wanawake na masikini hawakuruhusiwa kupiga kura wala kujihusisha na siasa, na imewachukua muda mrefu sana kurekebisha hayo,

- Huwezi ku-question propaganda kama kweli unaelewa maana ya hili neno politically, Mrema alikuwa na a big chance ya kuwachafua CCM kuliko walivyomchafua yeye, lakini kwa vile na yeye alikuwa fisadi ndio maana alishindwa kusema anything worthy against the establishment, mimi naamini kwamba kulikuwa na an agreement ya siri between CCM na Mrema ya kutogusana kwenye maovu yao.

- Tizama majuzi Chadema na Zitto, ngoma ilivyoishia kua draw wamejaribu kumchafua Zitto na yeye akawachafua, ikaja Compromise unafikiri bila ya Zitto kuwa na elimu ya juu na clean leader angeweza kuyafanya haya, ya kuwachafua Chadema na kubaki Naibu Katibu wao? au unafikiri yametokea kwa bahati mbaya tu bila elimu kutumika?

- Maovu yote ya CCM yaliyokuja kutolewa baadaye na Mrema, yalikua ni yale ya kupewa na Mzindakaya tu na sio aliyoya-experience yeye mwenyewe kama waziri, unafikiri ni kwa nini mkuu? Kwa nini hakuongelea tena dhahabu ya Airport?

Respect.

FMEs!
 
Zakumi stay kwenye hoja na uache kwenda personal kwasababu hakuna mashindano hapa,dont punch below the belt na pia acha ukigeu geu,hapo juu ume mu acuse Mrema kwa mambo hayo kuwa hafai kuwa rais lakini hapa chini ukimfagilia Zuma,Unaajua ya Zuma?acha hizo mkuu,lets stay on the point ili mjadala usiharibike....Kama ulishasema kuwa tatizo ni katiba na check and balance basi ungeendela kuinyambulisha hoja ako na si kujichanganya mwenyewe....

Mkuu hakuna mashindano hapa. Matatizo ni kuwa mnaomshabikia Mrema mnashindwa kujenga hoja. Mnatumai emotions kumpamba mtu wenu.

Mnaleta mifano ya Zuma na John hili kuonyesha kuwa asiye na elimu pia anaweza. Lakini mnashindwa kuonyesha kuwa mazingira aliyonayo Zuma ni different proposition.

Hayo mambo niyo-accuse Mrema yanaeleweka. Na yalikuwepo kwenye kikao cha NCCR kilichofanyika Tanga.
 
Mkuu JMushi

Uko juu sana pengine hii inaweza kuwa ni faida ya kuwa na hili jukwaa.
Wananchi wamelishwa propaganda mpaka wamekubali upuuzi wa wanasiasa ambao wakati wanamsakama Bwana Mrema kwa kila aina ya misamiati hatimaye muda umekuja kuwaumbua jinsi walivyolifilisi taifa.
Tanzania ya leo inamuhitaji sana Bwana Mrema kuikwamua katika tope la ufisadi.

- Mkuu naona na wewe uko juu sana, naomba kukuuliza Mrema alifanya nini hasa katika kupigana na mafisadi, yaani viongozi wa juu wezi? Au kwa kuanzisha vuto vingi vya polisi mitaani kama alivyosema mwingine huko nyuma? Can we talk with facts please?

Tunahitaji migodi yetu ina inayotoa dhahabu nzuri ianze kunufaisha taifa.Tunahitaji mafisadi wote wafikishwe mahakamani bila kujali kama ni wajumbe wa NEC au CC.Tunahitaji kuona viongozi wa ngazi mbali mbali wanafuata sheria na taratibu.Tunahitaji kuwa na Rais atakayetumia muda wake mwingi kushughulikia matatizo ya wananchi wake badala ya kuzurura ughaibuni.Tunahitaji kuwa na sheria kali dhidi ya wahujumu uchumi ikiwezekana adhabu ya kifo kama walivyo ndugu zetu wachina.

- Again nini record ya Mrema on all this uliyoyataja yaani migodi, mafisadi na sheria ya jamhuri, na sheria za wahujumu uchumi?

Viongozi wa zamani ambao bado wako kwenye system kama J malechela,Kingunge,Makweta na wengineo wengi wanatakiwa kupumzika kupisha damu changa kwakuwa mchango wao katika ujenzi wa taifa ni mdogo sana au haujapata kuonekana kabisa.Hawa kwa kiasi kikubwa wanachangia kuendeleza system mbovu.Haiwezekani kiongozi umekaa kwenye system kwa zaidi ya miongo mitatu huna kitu/mark unachoweza kuwaeleza watanzania.

- Yale yale, mkuu unasema Kikwete ni kiongozi wa zamani? au Membe ni kiongozi wa zamani? Au Zitto ni kiongozi wa zamani? Sasa how does Mrema fit na hii idea mkuu au yeye bado ni kiongozi wa sasa?

- Eti unasema age ya viongozi wetu ndio sababu ya ubovu wa uongozi wetu wa taifa, are you serious mkuu au ni just a big joke? I mean nini age ya Mrema as of this point?

Respect.

FMEs!
 
Tukienda step by step tutaelewana,na pia tukiacha ushabiki na maneno ya kejeli.
Mambo mengi ya kisiasa tunayoyafanya sasa hivi ni nje ya hatua ya kijamii tuliyoifikia...Huwezi kutaka profesa aende kufundisha vidudu!Na pia mechanism tunazotumia hazitunufaishi bali zinazidi kutudidimiza. Ni kama vile tunavyoingia kwenye ubepari kabla ya kuvuka stage nyingine zote ambapo stage ya kwanza ni ujima! Huwezi kuoongeza unga kabla uji haujatokota,hii ni kama unajua kupika ugali.

Nimesema hapo nyuma kuwa siasa za vyama zimeturudisha nyuma na bado zinatufanya tuwe stagnant...Hatuendi mahali,sio Taifa kwanza ni chama kwanza,na ndio maana nikasema hapo nyuma kuwa viongozi wote wanachaguliwa kwa vigezo vya ukada,ama kuwa kada maarufu zaidi ya uzalendo kwa taifa,hatuna sera za kitaifa zenye mwongozo wa kututoa kwenye umasikini na sheria tulizo nazo ni mbovu hata mwenye kuzivunja anaweza kuwa na justifiable reasons to do so.
Katiba ile ya mkoloni iliyokuwa ya kumkandamiza Mtanganyika ndiyo iliyokuwa adapted na viongozi wetu ended up Black colonialists.

Jamaa yako Zakumi anaponda kuhusu elimu ya Mrema na kufagilia ya Zuma huku akijichanganya kwa kusema kuwa Mrema hafai kwasababu ambazo ukilinganisha na Zuma ni kama usiku na mchana.

Sikatai kuhusu umuhimu wa political propaganda kwenye kugombea madaraka,ila nachohoji ni kuhusu hizo propaganda zenyewe,wakati wenzetu wanatumia political system kuendelea,sisi tunazitumia kurudi nyuma,hapo ndipo kwenye swali uliposhindwa kuelewa,kwamba baada ya siasa zetu kutumika kumng'oa mkoloni,je ni right kwa siasa hizo hizo kutumika kutuondolea wazalendo?Mfano wa Sokoine na Mrema ni wa karibu zaidi...Kwanini kuna watu wanataka tuendelee kucheza kwenye tope tuu?


Nimeponda elimu ya Mrema kwa sababu mbili. Kwanza alikuwa anatoa amri bila kufuata sheria. Kwa mfano alikwenda Arusha na mwanamke akamletea malalamiko kuwa Mume aliyeachana naye amechukua mali zote. Mrema akatoa amri kuwa mwanamke apewe nyumba. Mahakama ni chombo pekee yake chenye kuweza kutoa amri kama hii.

Pili nimeponda elimu ya Mrema kutokana na system na demokraci yetu. Insitutions zilizopo Afrika kusini zinaweza ku-afford kuwa na mtu kama Zuma at the helm. Kwa Tanzania, kuna uwezekano wa kumkaribisha Idd Amin au Bokasa.
 
Phillemon Mikael said:
ni kweli mwambie MKULU FMES..
Phillemon Mikael said:
UKWELI ni kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya elimu na busara ya uongozi....

kwanza lazima mjuwe hofu ya mrema kuwa rais ndio iliwafanya ccm waweke kipengele cha degree kwenye kazi ya urais...kalini hicho kipengele hakina maana yeyote!!!

mrema alikuwa very charismatic na tishio...alikuwa ana damu ya kupendwa ....nakumbuka enzi zile tulienda uwanja wa ndege wakati mzee mwinyi rais na mrema ni naibu waziri mkuu..unaweza hata kucheka,ukipangwa msafara kuelekea ikulu kwenye gari la wazi na rais mgeni...ukipita maeneo ya mkusanyiko ...vingunguti,buguruni ....uhuru...ilikuwa inawashangaza hata viongozi wageni kwani wananchi walikuwa hawawashangilii...lakini wakishapita ...wanasikia kelele nzito nyuma[nadhani walikuwa wakifikiri watanzania wanachukua dakika moja kufanya utambuzi kichwani na kuanza kushangilia]....kifupi baadaye ilibidi mrema awe gari lake linapangwa nyuma kidogo ya gari la rais ....ili kuondoa hisia za yeye kushangiliwa na rais kuachwa...mzeee mwinyi hakuwa na tabu hata kidogo na umaarufu wa mrema ..na alimkubali ...isitoshe aliposimamishwa kazi miaka ile walikuwa na mrema....ambaye umaarufu wa mrema ulikuwa ukimkera ni waziri mkuu cleopa msuya....kwani wananchi hawakujuwa hata kama yeye yupo...na hata aliye engneer kwa kiasi kikubwa mrema kuondolewa unaibu ni cleopa baada ya kumlalamikia mwinyi kuwa hawezi kufanya kazi naye[nadhani zilikuwa siasa za urais wa 1995].

Wakuu tukirudi kwenye elimu..dunia imeshuudia viongozi wazuri tu wenye elimu za kawaida..tukianza na hapa nyumbani ..mzee mwinyi hakuwa graduate[ana diploma ya uwalimu wa kingereza], mrema ana diploma ya uwalimu [ ana diploma ya masuala ya ujasusi na propaganda ya east europe,huwa haitajwi sana].., ,ukienda hapo kenya MOI ana diploma ya ualimu tu ..na walimuita profesa wa siasa[alimudu kuishika nchi pamoja kuliko mchumi kibaki]

nenda uingereza ...john major ...hakuwa msomi[kwenye nchi ya wasomi],marekani regan [one of favourites presidents-hakuwa msomi]..and the list is long....,tuache hapo south africa ambapo Zuma ..zaidi ya elimu ya uzoefu kazini ya kijasusi [russia] -only field training ..hana elimu ya kawaida ya darasani....

tofauti waliyonayo viongozi wenye elimu ndogo ambayo inawasaidia ni usikivu....wanawasikiliza wananchi na washauri kuliko hisia zao...na mara nyingi huwasaidia kuliko wasomi ambao hujiona wanajuwa !!




Philemon Mikael,

..nadhani kuna mambo umeyaacha hapo ktk kuelezea matukio yaliyopelekea Mrema kufukuzwa kazi na Raisi Mwinyi.

..Mrema alikiuka utaratibu wa Collective Responsibility ktk baraza la Mawaziri baada ya kupingana na msimamo wa serikali ndani ya kikao cha Bunge.

..serikali ilikuwa inajaribu kulizima suala la kashfa ya ununuzi wa mashamba ya mkonge uliofanywa na mfanyabiashara anayeitwa Chavda.

..kwa mtu anayeelewa jinsi serikali inavyofanya kazi lazima angejua kwamba kilichokuwa kinafuatia baada ya hotuba ya Mrema bungeni ni kufukuzwa kazi tu. hata Mrema mwenyewe alijua kwamba atafukuzwa kazi na alieleza ndani ya bunge kwamba yuko tayari kwa lolote.

..Isaac Mruma ambaye alikuwa mwandishi wa habari wa Malecela,Msuya,na baadaye Sumaye, aliandika makala nzuri sana kuhusu matukio yaliyopelekea Mrema kufukuzwa kazi. tena aliandika kama mwandishi wa habari wa Waziri Mkuu, jirani ya Mrema wakati wakiwa Dodoma, na zaidi mtani wake wa kikabila.

..siku aliyotofautiana na serikali bungeni, Mrema alilalamikia mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na kuandikiwa barua na mwanasheria mkuu wa serikali akielezwa kwamba cheo cha Naibu Waziri Mkuu kilikuwa hakipo kwenye Katiba na hakitambuliwi Kisheria.


..kwa mtizamo wangu nadhani Mrema alikuwa frustrated na kuondolewa kwake Wizara ya Mambo ya ndani na kuhamishiwa Wizara ya Kazi.

..kitendo cha Raisi Mwinyi kumruka "Naibu Waziri Mkuu" Mrema ktk kuziba nafasi iliyoachwa na Cygwiyemwisi John Malecela nacho kilikuwa kielelezo machoni mwa Mrema kwamba Mzee Mwinyi alikuwa hana imani naye.

..CCM waliweka masharti kwamba mgombea wao wa Uraisi lazima awe na shahada ya Chuo kikuu.

..kwa mtizamo wangu, Mrema alikuwa anataka kuwa Raisi, na wakubwa wenzake CCM walikuwa hawana nia ya kumpa nafasi agombee.
 
Zakumi said:
Nimeponda elimu ya Mrema kwa sababu mbili. Kwanza alikuwa anatoa amri bila kufuata sheria. Kwa mfano alikwenda Arusha na mwanamke akamletea malalamiko kuwa Mume aliyeachana naye amechukua mali zote. Mrema akatoa amri kuwa mwanamke apewe nyumba. Mahakama ni chombo pekee yake chenye kuweza kutoa amri kama hii.

Zakumi,

..wananchi wanafikiri kwa system yetu ya Tanzania Raisi wa ajabu-ajabu anaweza kudhibitiwa na wasaidizi au washauri wake.

..Mrema aliendelea na tabia yake ya kudharau sheria na taratibu, hata baada ya kupewa naibu waziri mwenye utalaamu wa sheria Jaji Edward Mwesiumo.

..NCCR nao walidhani wanaweza kumrekebisha Mrema kwa kumteua Prof.Mwesiga Baregu kuwa msaidizi wake. mwisho wa ndoa ya NCCR na Mrema ilikuwa ni chama kusambaratika.
 
Mrema ana matatizo yake lakini sioni kama yanaingiliana na kabila lake.

Yanahusiana kabisa maana wachaga wengi wako hivyo, hawataki kushindwa wala kuwa chini ya wengine ndo maana asilimia kubwa ya watuhumiwa wa ufisadi ni wachaga. Meza kama ilivyo ukitaka data sema tukuangushia. Mrema kama walivyo wachaga wengine walipata wasaa wa kushika madaraka wamekuwa hivyo....Mengi, Mbowe, Mrema, Mgonja, Mramba, Yona n.k. wote hovyo kabisa
 
Yanahusiana kabisa maana wachaga wengi wako hivyo, hawataki kushindwa wala kuwa chini ya wengine ndo maana asilimia kubwa ya watuhumiwa wa ufisadi ni wachaga. Meza kama ilivyo ukitaka data sema tukuangushia. Mrema kama walivyo wachaga wengine walipata wasaa wa kushika madaraka wamekuwa hivyo....Mengi, Mbowe, Mrema, Mgonja, Mramba, n.k. wote hovyo kabisa

Hivi Mgonja mchaga? Yale yale! Hatuwezi kumjadili mtu bila kuingiza kabila au rangi yake.

Amandla......
 
Yanahusiana kabisa maana wachaga wengi wako hivyo, hawataki kushindwa wala kuwa chini ya wengine ndo maana asilimia kubwa ya watuhumiwa wa ufisadi ni wachaga. Meza kama ilivyo ukitaka data sema tukuangushia. Mrema kama walivyo wachaga wengine walipata wasaa wa kushika madaraka wamekuwa hivyo....Mengi, Mbowe, Mrema, Mgonja, Mramba, Yona n.k. wote hovyo kabisa


ukichukia watu kupita kiasi ..ndio unawapa catalyst ya kusonga mbele .....[catalyst change the speed of the chemical reaction but it self remain unchanged at the end of the reaction]....all haters ...you are just the catalyst....na mtabaki hivyo hivyo....asilani!!!!

Tupendane watanzania!!!
 
FMES...MZEE mwinyi alisema "kila zama na kitabu chake" ,zama za mrema zimepita ..na sioni mantiki ya kumfananisha na viongozi wa sasa ...kwani zaidi labda ya ubunge hakuna nafasi zaidi ya hiyo anaweza kustahili...kifupi hana nafasi ya kugombea urais tena!!!

ni ukweli usio kificho kuwa ukitaja viongozi watatu maarufu [of all the time ] kisiasa miongoni mwa wananchi ...basi mrema,sokoine na nyerere ndio watakaotajwa....tofautisha list hiyo na uamue kuandaa viongozi bora kabisa ...wenye busara kitaifa[wenye busara si lazima wapendwe na wananchi]...ambapo hapo unaweza kumpata tena nyerere,salim,malecela,warioba,mkapa,mwinyi etc........kikwete hapo aingii yeye atakuwa anaingia kwenye kundi la kwanza la popular leaders....na anaweza kuwa chini ya mrema kwenye list ya viongozi waliopata kupendwa na watanzania..[populist]

kwa hiyo napingana na wewe kufananisha mrema na wapiganaji wa sasa kama slaa,zitto ,mbowe na wale wa ccm...kila kitu na wakati wake...wakati wake umekwisha,lakini kubalini kuwa wakati mrema anaapigana na ufisadi enzi zile....watu walikuwa hawamuelewi kama wananchi sasa wanavyoanza kuellewa...enzi zile walikuwa wakimshabikia kama mpira kuliko kumsikiliza ...na hili mwalimu aliliona ,...ndio maana alikuwa akiwaambia serikali wasimchape au kumpiga mabomu...maana ilikuwa kama kuwaamsha wananchi!!!

ni wazi kuwa heshima ya mrema kwenye siasa za nchi hii au legacy yake ipo,na kwa kuwa sasa sio tishio hakuna haja kuogopa kumkiri....hakuna kiongozi aliyepata kuigharimu CCM na idara ya usalama pesa kummaliza kama mrema...kuna watu wamekuwa mabilionia ..just kwa ku hold budget vote ya kummaliza mrema....na wengine iliwagharimu maisha just kwa kushindwa kumdhibiti.....ikabidi wapate "court marshall assasin"!!

kwa kuwa amezeeka na afya yake sio nzuri ..si vema kusubiri vinginevyo kuikiri legacy yake...pande zote !
 
Tunatakiwa kuwa na kiongozi mwenye vision, mwenye akili, mwenye uwezo wa kuongoza , kupenda maendeleo, kutoa leadership na mwenye uwezo wa kumanage. Si lazima kila hii quality ipatikane kutokana na elimu. Unaweza kusoma kama baadhi ya viongozi wetu wa sasa lakini usiwe na hivyo, unaweza usisome lakini ukawa na uwezo mkubwa wa ku-manage.

Kiti cha urais, uwaziri, ubunge na uongozi mwingine hauhitaji kufanya kazi kwa kubahatisha au kutegemea tu ushauri wa watu. So Mrema kwa maoni yangu alikuwa very patriotic kwa kuwa aliipigania sana Tanzania, lakini hakuwa na uwezo wa kuwa rais kwa kuwa sera yake kubwa ilikuwa ni kuwiangiza magereza wezi na vigogo wa wakati ule. Hakuwa na mapendekezo yoyote ya sera ambayo ingemsaidia mtanzania.
Angefanya alilotaka kwa mwezi au miezi miwili kuwa rais kunakuhitaji ufanye kazi kwa at least miaka 5, yeye angefanya nini?

Wajibu wa kuwa na Washauri na Wasaidizi ni nini?

Mshazoea ya yule mmoja kati ya Mamilioni Nyerere, aliyewaza, tafakari kuota na kisha kuhakikisha linafanyika ndiyo maana tunatafuta mtu aliye na sifa zote.

Mwinyi, Mkapa na Kikwete, pamoja na usomi wao, walikuwa na wana washauri.

Tatizo la Tanzania ni mfumo mbovu na Katiba chovu ambayo inafanya Serikali Kuu ijiamini kupita kiasi na kufanya kazi kama Mungu na kudharau Bunge na Mahakama.

Leo ukimweka Rais wa Tanzania katika mfumo huru ambao Bunge na Mahakama vinaweza kumpinga bila kutishiana na kuwekeana vikao vya Chama, tunaweza kufika mbali sana.

Ni mara moja tuu, katika historia yetu ambapo Kiongozi wa Serikali Bungeni alithubutu kulipa nguvu Bunge kwa kutumia Demokrasia na uamuzi wake huu uliishia yeye kuwekwa kati kwenye vikao vya chama, akavuliwa madaraka, akaandikiwa kitabu na akawekewa doa la milele kwenye paji la kuwa kamwe hataachiwa awe Rais wa Tanzania.
 
- Sio CCM, Mwalimu wala Mrema waliofanya anything kuwasiaidia wananchi na hayo matatizo, hilo ninakubaliana na wewe kwa 100%.



- Mkuu kwani kamati ya madini ya Zitto, ilifanya nini?

Respect.

FMEs!

Dear Jemedari FMES,

Kwi kwi kwi kwi au nikitumia kicheko chako Bwa ha ha ha Umenifanya nicheke na kutabasamu muno kwa muno kwa kauli yako hapo juu. Sasa kama CCM imeshindwa kuwasaidia Wananchi, kwa nini unang'ang'ania kuwa CCM ndiyo pekee suluhisho la matatizo ya Mtanzania?

Kamati ya Madini haikuwa ya Zitto, ilikuwa ni kamati iliyoundwa na Rais Kikwete na Mzee Jaji Mark Bomani alipewa madaraka ya kuwa Mwenyekiti.

Kumbuka hii Tume/Kamati haikuwa ya Bunge, na hivyo Bunge halina mamlaka ya kufanyia kazi mapendekezo ya hiyo kamati bila ya ridhaa ya Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM.

Katika mgawanyo wa Tonge la kupigana vita kati ya Richmond na Buzwagi, Bunge lilipoteza mwelekeo lilipokimbilia mradi wa Richmond ambao ukipima kati ya Richmond na Madini na Nishati ni kipi chenye nguvu na chenye gharama kubwa, utagundua ni Madini na Nishati.

Compromise iliyofanywa ili watu wamkabe koo Lowassa na Richmond yake, imetoa upenyo kwa Bunge kushindwa kuwasilisha muswaada wa kubadilisha Sheria za Madini na Nishati na hata kufuta na kusitisha mikataba ya Madini iliyofanywa na Serikali.

Bunge lilipoteza haki na nguvu ambayo in the end, kama wangekimbilia tonge la Madini na Nishati, bado wangekuja weza mkaba koo Lowassa.

Cha kamati ya Bomani/Zitto, si umuulize Mshikaji akija GA wiki hizi zinazokuja? au ni usawa wa kilauri Musee na biashara zingine ni kapuni?
 
Lula wa Brazil si msomi, na nchi yake iko katika nchi kumi zenye uchumi bora duniani.

Eva Morales wa Bolivia si msomi lakini anaendesha nchi na kinaeleweka.

Ni Waafrika pekee tunaopenda Prestige za Usomi kama vile ni tija na njia ya kuleta maendeleo!
 
Dear Jemedari FMES,

Kwi kwi kwi kwi au nikitumia kicheko chako Bwa ha ha ha Umenifanya nicheke na kutabasamu muno kwa muno kwa kauli yako hapo juu. Sasa kama CCM imeshindwa kuwasaidia Wananchi, kwa nini unang'ang'ania kuwa CCM ndiyo pekee suluhisho la matatizo ya Mtanzania?

- Mchungaji sijawahi kusema CCM ndio suluhisho pekee, ninachosema kwenye hii thread ni kwamba wapiganaji wame-accomplish more kuliko Mrema na yanaonekana, na besides haya Upinzani bado kutuhakikishia wananchi kwamba wanao uwezo wa kuongoza tofauti na CCM.

- Kwamba ati nimesema CCM ndio the only solution, labda unionyeshe maneno yangu hayo niliandika wapi mkuu?

Kamati ya Madini haikuwa ya Zitto, ilikuwa ni kamati iliyoundwa na Rais Kikwete na Mzee Jaji Mark Bomani alipewa madaraka ya kuwa Mwenyekiti.
Kumbuka hii Tume/Kamati haikuwa ya Bunge, na hivyo Bunge halina mamlaka ya kufanyia kazi mapendekezo ya hiyo kamati bila ya ridhaa ya Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM. Katika mgawanyo wa Tonge la kupigana vita kati ya Richmond na Buzwagi, Bunge lilipoteza mwelekeo lilipokimbilia mradi wa Richmond ambao ukipima kati ya Richmond na Madini na Nishati ni kipi chenye nguvu na chenye gharama kubwa, utagundua ni Madini na Nishati. Compromise iliyofanywa ili watu wamkabe koo Lowassa na Richmond yake, imetoa upenyo kwa Bunge kushindwa kuwasilisha muswaada wa kubadilisha Sheria za Madini na Nishati na hata kufuta na kusitisha mikataba ya Madini iliyofanywa na Serikali. Bunge lilipoteza haki na nguvu ambayo in the end, kama wangekimbilia tonge la Madini na Nishati, bado wangekuja weza mkaba koo Lowassa. Cha kamati ya Bomani/Zitto, si umuulize Mshikaji akija GA wiki hizi zinazokuja? au ni usawa wa kilauri Musee na biashara zingine ni kapuni?


- Strong education, ila nothing to do na Mrema.

Respect.

FMEs!
 
hakuna kitu kinaniuma kama makampuni ya dhahabu yanavyotufanyia umafia ile nchi uliobarikiwa na mafia wa CCM,yaani siamini kama Serikali yetu ni incompetent/mafisadi kiasi kile...tunahitaji mapinduzi ili vizazi vijavyo viweze kuishi vizuri!
 
Back
Top Bottom