Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!


- Mkuu kwanza ninapata kizungu zungu sana ninapoona some of The Great Thinkers wakijaribu kwa nguvu zote ku-promote ujinga, na kwamba eti Tanzania tunahitaji kiongozi asiye na elimu as a solution to our political, ecomomics na legal problems.

- Na besides, hao viongozi uliowasema ni kweli hawakusoma kabisaa angalau Mrema anawazidi mno kwa elimu, lakini tofauti ni kwamba wao wanaheshimu sheria za nchi zao na maamuzi mengi wanayoyafanya hayaendi kinyume na katiba ya nchi zao, as opposed na maamuzi mengi ya Mrema, ingawa Morales naye alitumia ufisadi sana kupitisha ile national memorandum.

Lakini still, solution ya matatizo yetu Tanzania sio kiongozi asiye na elimu kama Mrema, na pia ningeomba kuwatahadharisha kwamba kuna vijana wadogo humu, sasa hizi message za kuwaambia kuwa elimu sio muhimu sana, inatisha sana wakuu!

Respect.

FMEs!
 

- Hapa tupo pamoja sana Mkuu PM.

Respect.

Kamanda FMEs!
 
 
 

Kila kitu huenda na wakati, kuna maswali mengi sana humu ndani kwa nini Mrema alifanya hiki au kwa au mbona alishindwa.

Tunachofumbia macho ni kuwa Mrema hakuwa Rais, hakuwa na mamlaka ya mwisho au kauli ya mwisho. Sawa na Sokoine alivyokosa mamlaka ya mwisho kupigana vita na Uhujumu 1983-84.

Mrema akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alikuwa anawajibika kwa Waziri Mkuu na Rais. Kama Mrema alikosea akavunja sheria na kujifanyia alilotaka, aliyepaswa kumkalisha kitako na kumuonya ni Waziri Mkuu na Rais na kama hakusikiliza au kufata amri aliyopewa, angefukuzwa kazi.

Hata alipokuwa Naibu Waziri Mkuu, kama cheo hicho hakikuwapo Kikatiba, ni kosa la aliyempa hicho cheo na wote wale walioridhia kuwa ni sawa na kuvunja na kukiuka Katiba, including Mrema mwenyewe.

Lakini kama leo hii Said Mwema na Masha hawawezi kufanya kazi mpaka Rais aseme, kwani kuna tofauti gani na Mrema alipokuwa akifuka kama povu na kuonekana mwendawazimu kama alichofanya kiliishia kwa yeye kuwekwa kitako Ikulu na kuambiwa nyamaza au sasa basi?

Mrema huyu huyu tunayemtuhumu kuwa alikuwa kichwa mbofu, waliokuwa Watawala walinufaika na alichokuwa anakifanya. Kwa jinsi alivyojizolea mashabiki, ndivyo Serikali aliyokuwa akiifanyia kazi ilipata sifa na kuimbiwa ngonjera nyingi na ndio maana Viongozi wakuu hawakujishughulisha naye mpaka pale Tume ya Nyalali ilipopendekeza kuwepo kwa Vyama vingi na shinikizo la Wahisani kwamba tuachane na mfumo wa Chama kimoja, ndipo kila mtu akabaini kuwa akiondoka Mwinyi, the most popular person ni Mrema.

Si kweli kuwa Mrema na Upinzani ulishindwa uchaguzi wa 1995 kwa ridhaa ya wananchi, CCM ilicheza faulo nyingi sana. Anzia Zanzibar jinsi Sefu alivyonyang'anywa tonge na Komandoo Salmini akabinywa kende na Mzee wa Kizanaki, njoo majimbo mengine ambapo CCM ilijiingiza kwa nguvu ya Dola na pesa na kuhakikisha kuwa inakuwa na nguvu kubwa Bungeni ya zaidi ya theluthi mbili za kura.

Hivyo pamoja na Umaarufu wake, CCM na Serikali ilifany akampeni kubwa sana ya kumwangusha Mrema na walifanikiwa kwa kuuvunjilia nguvu Upinzani na ule umaarufu wa Mrema.

Alichoshindwa kukielewa Mrema ni kuwa walichomsomesha CCM na UWT-TISS, kama mtu wa propaganda, ushushushu, kuvuruga watu na kutifuatifua, ni kuwa waliokuwa Waajiri wake, walitumia mbinu walizomwajiria kummaliza kisiasa na kuhakikisha Upinzani haushindi.

Hivyo kukurukakara za Mrema ni kutokana na mafunzo aliyopewa ya Propaganda za Kikomunisti. Tofauti yake na Kingunge ni kuwa Kingunge alielemea kwenye siasa na maneno, na Mrema ukachero na ushushushu wa kubinya watu makoo ndio aliutumia kwa dhati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, fani iliyokuwa ikifanana na alichosomea na kufundishwa (programmed).

Alipopelekwa Wizara ya kazi, mchezo ukageuka, na kama binadamu yeyote, ni vigumu kuwa makini na fanisi kwenye uwanja ambao huna uwezo.

Leo ukimpeleka Mhasibu akawe Mganga Mkuu unategemea nini?

Alichofanya Mrema kama mtumishi wa Serikali, kilikuwa na baraka za Serikali na Mkuu wa Serikali, na ndio maana hata vile vituo vya polisi pamoja na kuwa zilikuwa ni pesa za Wananchi, Serikali pia iligharamia na kuviendesha hivyo vituo na kupeleka Polisi, Silaha na Mitambo (Radio, Simu) na vifaa vingine vya kazi.

Nyakati zimepita, tupo kwenye vyama vingi, lakini mfumo haujabadilika, bado ni ule ule na ndio maana leo hii, kuna mvutano ndani ya Bunge na Serikali. Wabunge wanaona ni haki yao kuiwajibisha Serikali kuu, lakini Serikali kuu ya CCM inatumia Katiba ya Chama kuzima "Uhaini"!
 
Wakuu nimepata huu ujumbe sasa hivi kutoka somewhere, vipi umekaaje na hivi vita vya wapiganaji:-



 


FMES,

Tanzania has nothing to loose tukipata Form Four leaver, Form Six leaver au Diploma moja.

If Mkapa with his Masters and Kikwete with his BA or Masters have failed, how can you tell somebody that we only need PHD holders?

Chenge went to Havard, so was Rostam LSE, wengne je? Mramba has masters, Warioba has masters, Salim, Salmin and Shein are PHD holders, Mwandosya is a PHD holder, Mbilinyi is PHD holder, Dr. Bilali is PHD holder, Mattaka has Masters, Late Balali had PHD, Mgonja and Yona are very well educated, and so is Magufuli, Masha, Mwagunga, Hussein Mwinyi, Pinda and so was Malecela, Msuya, Kibona, Malima, Makweta even Mtei!

Great leadership has nothing to do with college degree, to have it is a plus and could provide an advantage, but it is not a solution. We have proof in Tanzania!
 

- Mchungaji vipi tena unaanza kubadilika, kwani wapiganaji 11 unaowa-question effectiveness yao against Mrema, ni marais wa Tanzania?

Respect.

FMEs!
 
Rev. Kishoka,
Mkuu mkitaka kumsifia Mrema fanyeni nyie kwa mapenzi yenu lakini sii sote humu.Ni haki yenu kimsingi, kwani mimi binafsi, mtu kama Mrema kuwa rais wangu au hata kukaribua kuwa rais wangu ilikuwa inatisha sana. Record yake mbaya sana ukianza na vifo vya bi vizee kule Shinyanga..
Niliwahi kuandika mengi kuhusu Mrema akiwa waziri na kama sikosei mkuu JMushi1 alinipinga sana kwa sababu ambazo yeye mwenyewe anaijua. Hivyo poengine ukaribu wenu kwa mtu huyu mnamwelewa tofauti nasi ambao ni raia na hatuna nuru kwake....
Mrema ni kama viongozi wengine waliobobea ktk Ujamaa na mtu KGB system...Sifa za vyombo vya kijasusi au upelelezi ktk enzi za Ukomunist zina sifa yake ya ROHO MBAYA..Ni watu wasiotaka mtu mwingine afanikiwe ila wao au ktk system yao. Na hakuna njia bora ila ile wanayoiona wao..
 

- Tunahitaji wananchi waliosoma na viongozi waliosoma, na Tanzania ni mfano mkubwa sana wa wananchi wengi wasiosoma, kwa sababu inakuwa ni vigumu kwao kuwa-hold viongozi wao to the task, matokeo ndio tuliyonayo ya viongozi wetu kujifanyia wanayotaka.

Respect.

FMEs!
 
- Mchungaji vipi tena unaanza kubadilika, kwani wapiganaji 11 unaowa-question effectiveness yao against Mrema, ni marais wa Tanzania?

Respect.

FMEs!

Alichokifanya Mrema ni kumchallenge Rais kwa kukataa Collective Responsibility na kuondona Serikalini na CCM.

Ninacho wachallenge Wapiganaji 11 ni kumchallenge Rais na Mwenyekiti wao kwa kuwa chini ya Uongozi wake, Tanzania inagota na inayumba kupita kiasi.

Ndio maana nimesema kwenye zile thread nyingine, kelel za Ufisadi hazilipi, bali mengine yote ya kuonyesha wazi kuwa Serikali haina nguvu na aliye madarakani hafai.

This is what I expect from Wapiganaji, kutoa ultimatum ndani ya Chama na ndani ya Serikali si kwa ajili ya Mafisadi wachache bali mfumo mzima wa Kiutawala na Kiutendaji ambao ndio mzizi mkuu wa Tanzania kuwa hapa ilipo.

Kulilia shingo ya Chenge haitoshi na ndio maana kwenye majibu yangu kwa Mzee Mwanakijiji, nilisema wakaze Kende walilie kiti cha Kikwete na wapige mawe Serikali kwa kila kitu kinachoonekana ni udhaifu kama nilivyohoji kwenye thread ya Mafanikio gani ya Ari, Kasi na Nguvu.

Wanapoendelea kung'ata na kupuliza na kuchekeana na Mkuu wao, basi yanayotokea ni sawa na haya ya Makamba kwenda Urambo na kumpigia debe Sitta!

Je umesahau mnajimu wa humu ndani Mzee Mwanakijiji alisema kwenye makala yake kuhusu Wapiganaji kuungana na Mengi kuwa CCM na Mafisadi wanaweza kubadili kibao na kuanza kuwasifia kina Sitta na Mwakyembe na kuwapigia debe la nguvu ambalo halijawahai kuonekana?

Au umesahau kauli ya Kikwete majuzi kudai Chama hakina mfarakano wa kiitikadi bali ni jambo la kawaida watu kutofautiania (I think alitumianeno kuchikiana) na wapiganaji wakashangilia kauli hiyo na kusema ndiyo kukua kwa demokrasia ndani ya CCM?

Kama ndivyo kukua kwa demokrasia, iweje basi Mafisadi walioshikilia hatamu Chama walikuwa na kampeni kali kiasi hicho kumng'oa Sitta uanachama wa CCM na wenzake? au kuanza kupeleka pesa kwenye majimbo ya "Wapiganaji" na kuhonga wagombea wapya?

What kind of epiphany has emerged inside CCM hierachy that now Sitta ni shujaa?
 

Mkandara,

This is where you go wrong kwa ku-internalize na ku-personalize hii issue.

Una haki ya kumpinga Mrema, sawa na wale wanaompinga Nyerere lakini wewe unamtetea Nyerere.

The issue now is about quality character tunazohitaji, sasa kama ni hivyo hata tukisema tuweke jedwali tuandike, Mrema, Mwinyi, Kimario, Nyerere, Mkapa, Kikwete, sijui Kawawa au Msuya, kutakuwa na pros na cons!

Nyerere si aliamrisha watu wakaburuzwa kwenye vijiji vya ujamaa na wakapoteza mali zao na wengine kupoteza maisha?

Mkapa si aliamrisha jeshi litoe mkong'oto Pemba na Mwembechai na watu wakapoteza maisha?

Kikwete si karuhusu wawekezaji wajifanyie wanalotaka na kule Buzwagi, Nulyanhulu na sasa Loliondo, ni dola inatumika kunyanyasa Watanzania kwa kuchoma moto mali, kufunga watu na kila ina ya upuuzi kwa kisingizio ni uamuzi wa Serikali au Serikali kulinda maslahi ya Mwekezaji?

If Mrema was such an evil person, kwa nini Bosi wake Mwinyi ambaye aliwajibika basi tulimpa kura za ndiyo akatuongoza kwa miaka 10? naye Mwinyi huyo huyo, kwa kujiamini akampa Mrema uwaziri wa Mambo ya Ndani?
 

So which one do we need, Taifa la walioelimika au Viongozi wasomi?

Maana wote hao ni Wasomi, sasa kama wao na Usomi na Elimu zao, wanashindwa kuleta maendeleo au kutoa hamasa ya maendeleo, leo wananchi tukielimika na kuanza kudai haki zetu kama tunavyofanya hapa si mbinu za kutumia mabavu zitatumika?

Kama wao wana nia ya kweli kuamsha umma wa Watanzania uwe wachangiaji makini wa maendeleo, basi wangeachana na Umangimeza na Utemi na kufanya kila mtu mpumbavu na kuimarisha Ujinga (ignorance not stupidity) kwa kuwa na mfumo bora na endelevu wa elimu, kuwa na mfumo wa haki na utu na mfumo wa kweli wa Kidemokrasia.
 
Mkuu issue hapa ni Mrema au sio?..na ukiniambia sifa za Mrema kuweza kuukwaa urais nitakusikiliza vizuri kuliko hizi habari za kumsifia mgema.
Bila shaka unaposoma maandishi yangu utakuta namsifia Nyerere kwa yale alokamilisha na wote mnayafahamu..Na pia sijawahi kupinga mapungufu ya mwalimu kama kiongozi au makosa alowahi kuyafanya lakin isii kwa udhaifu wake ila mfumo mzima alojenga kutoweza kufanikiwa...

Kuna tofauti kubwa sana kati ya dereva alopata ajali kina Nyerere ukajaribu kumlinganisha na mtu ambaye hajui kuendesha ukamwachia gari la abiria kwa sababu tu ameonekana kuwa mwendeshaji mzuri wa baiskeli..Tunachotakiwa kuitazama ni dereva mzuri kuliko hata yule alopata ajali yaani kwa mfano huu kwa nini tusifikirie rais ambaye ni zaidi ya Nyerere, Mwionyi, Mkapa na hata JK.. ila mtu anaye chini au anafanana nao!
Hivi kweli wewe katika imani yako unaamini Mrema anaweza kuwa na vision ya tanzania ya kesho?...Mrema anaweza kujenga sera za Kitaifa ambazo mwenyewe anaweza kuamini kitaalam zitafanya kazi ktk mazingira tulokuwa nayo..

Kuna tofauti kubwa ya kiuongozi kati ya Nyerere na Mrema, kifupi Mrema hajawahi kuongoza zaidi ya wizara ambayo binafsi naamini ulikuwa mwanzo wa uharamia nchini.. Mwanzo wa wauza unga, usafirishaji pembe, dhahabu, dollar na hata waarabu kuingia Loliando imetokea wakati wa Mwinyi chini ya jicho la Mrema. Mwinyi, Mkapa na hata JK yawezekana hawakufaa lakini sii chini ya Mrema..kifupi tunaonekana kama vile tumekosa la mama basi hata la Punda linafaa.

Hivi kweli sisi Watanzania tunaweza kukaa hapa na akili zetu tuka suggest Mrema kuwa rais wa nchi! Kati ya majina tunayopendekeza ni kina Lowassa, sijui Rostam huoni kama sisi wenyewe ndio tuna upofu zaidi ya mgombea!
Mku hatupo hapa kulaumu mtu ila uwezo wa mtu huyo kuongoza at least uwe na picha ya maendeleo kwetu..
 

Mkuu naona better way ni tukubaliane kuwa hatuwezi kukubaliana. Ndio demokrasia yenyewe. Kumpigia kura Mkapa sio pride as well as sio shame, na sina uwezo wa kuchagua nani agombee urais. Lakini kwenye machaguo yaliyowekwa mbele yangu whether yaliwekwa na CCM au na NCCR whether yaliwekwa na Nyerere au Mrema, ilikuwa ni mimi kutumia common sense yangu (although now it seems that common sense is not common) kuchagua kati ya waliokuwepo. Kama wewe ulitumia busara zako kumchagua Mrema that was fine as well, ndio demokrasia yenyewe. When i say i knew Mkapa would make a better president than Mrema, that is my personal judgement. And the criterion i use to suggest and which i used to vote for Mkapa is his track record locally, regionaly and internationally. But that does not necessarily mean that no one would have been capable president tha Ben.
Mrema was better Minister of home affairs than many who were schooled than him, this definetly proves that education alone does not make one a better leader, it is much more than that. But that can not be used as justification or an excuse to have a dumb, unschooled and uneducated person in our high offices. Mkuu kila mtu ana kigezo na uhuru wa kuchagua anachopenda, na kila mtu ana uhuru wa kuwa na uhuru wa kuchagua na kupenda anachooona kinafaa. I respect that. Lakini naona hata leo ukija uchaguzi nikiambiwa nichague kati ya Mrema na Mkapa, pamoja na madudu aliyofanya Mkapa kwenye term ya pili, still nitamchagua Mkapa. Najua nataka nini na sitaki nini.
 
mkuu FMES pamoja na kelele wanazopiga wanaojiita wapiganaji 11...bado hawajafikia hadhi ya kufananishwa na mrema sembuse wapiganaji wa upinzani...wapiganaji 11 wanasukumwa na hidden ajenda...wapiganaji wa kweli lazima wasukumwe na utaifa...

nina shaka labda baadhi ya wapiganaji 11 wanasukumwa na kukosa fursa kati ya sababu....wengine walikuwa tayari wamejitangaza kuwa wanateuliwa uwaziri wa maliasili....wengine wana presure ya kuwa upande wa pili mwaka 2005;;;etc ..pamoja na kazi nzuri wanayoifanya ..tuwape sifa wanazostahili...tusiwavimbishe kichwa!!
 

- Mkuu nimefika mahali sasa umenipoteza, katika miaka 45 ya uongozi wa taifa letu viongozi walikua wamefungwa midomo, suddenly ametokea rais wa kuwafungulia midomo and the first thing wanatakiwa kuanza na yeye badala ya kuisafisha system kwanza?

- Eti JF tunaweza kuwapangia strategy wapiganaji? Labda kuwapa ushauri tu so far they are on the right track, na wamefanikiwa kubadilisha mienendo mingi sana ya bunge kwa manufaa ya wananchi, kwa mfano siku hizi shughuli yoyote inayoihusu serikali ikibidi kufanyika nje ya nchi, ni lazima balozi yetu ihusishwe na nchi inayotakiwa kufanyika shughuli hiyo, matokeo yake ni kwamba ile tabia ya baadhi ya viongozi wetu kusaini mikataba mahotelini huko majuu, hakuna tena,

- Kiwira tayari iko njiani kurudi mikononi mwa wananchi, I mean a lot to show for katika kipindi kifupi sana as opposed na Mrema, ambaye hakuna anything cha kuonyesha zaidi tu ya Mrema, Mrema na Mrema, mkuu ukiona kiongozi anatoka sehemu ya uongozi halafu kila kitu kina-fall apart basi huyo sio kiongozi anayefaa ila ni mbinafsi, kama kweli Mrema alifanya mnayosema alifanya basi yangekua yanaendelezwa hadi leo, angalau hata Keeenja ana nafuu sana maana aliyoyafanya City yanafahamika.

- Huenda wapiganaji hawaendi kwa speed unayoitaka, lakini haraka haraka haina baraka mkuu.

Respect.

FMEs!
 

- Tunahitaji wananchi wasomi na viongozi wasomi, period!

Respect.

FMEs!
 
Hivi Mrema alifanya kipi cha maana haswa maanake mimi sielewi?..
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…