FMES...MZEE mwinyi alisema "kila zama na kitabu chake" ,zama za mrema zimepita ..na sioni mantiki ya kumfananisha na viongozi wa sasa ...kwani zaidi labda ya ubunge hakuna nafasi zaidi ya hiyo anaweza kustahili...kifupi hana nafasi ya kugombea urais tena!!!
ni ukweli usio kificho kuwa ukitaja viongozi watatu maarufu [of all the time ] kisiasa miongoni mwa wananchi ...basi mrema,sokoine na nyerere ndio watakaotajwa....tofautisha list hiyo na uamue kuandaa viongozi bora kabisa ...wenye busara kitaifa[wenye busara si lazima wapendwe na wananchi]...ambapo hapo unaweza kumpata tena nyerere,salim,malecela,warioba,mkapa,mwinyi etc........kikwete hapo aingii yeye atakuwa anaingia kwenye kundi la kwanza la popular leaders....na anaweza kuwa chini ya mrema kwenye list ya viongozi waliopata kupendwa na watanzania..[populist]
kwa hiyo napingana na wewe kufananisha mrema na wapiganaji wa sasa kama slaa,zitto ,mbowe na wale wa ccm...kila kitu na wakati wake...wakati wake umekwisha,lakini kubalini kuwa wakati mrema anaapigana na ufisadi enzi zile....watu walikuwa hawamuelewi kama wananchi sasa wanavyoanza kuellewa...enzi zile walikuwa wakimshabikia kama mpira kuliko kumsikiliza ...na hili mwalimu aliliona ,...ndio maana alikuwa akiwaambia serikali wasimchape au kumpiga mabomu...maana ilikuwa kama kuwaamsha wananchi!!!
ni wazi kuwa heshima ya mrema kwenye siasa za nchi hii au legacy yake ipo,na kwa kuwa sasa sio tishio hakuna haja kuogopa kumkiri....hakuna kiongozi aliyepata kuigharimu CCM na idara ya usalama pesa kummaliza kama mrema...kuna watu wamekuwa mabilionia ..just kwa ku hold budget vote ya kummaliza mrema....na wengine iliwagharimu maisha just kwa kushindwa kumdhibiti.....ikabidi wapate "court marshall assasin"!!
kwa kuwa amezeeka na afya yake sio nzuri ..si vema kusubiri vinginevyo kuikiri legacy yake...pande zote !
Kila kitu huenda na wakati, kuna maswali mengi sana humu ndani kwa nini Mrema alifanya hiki au kwa au mbona alishindwa.
Tunachofumbia macho ni kuwa Mrema hakuwa Rais, hakuwa na mamlaka ya mwisho au kauli ya mwisho. Sawa na Sokoine alivyokosa mamlaka ya mwisho kupigana vita na Uhujumu 1983-84.
Mrema akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alikuwa anawajibika kwa Waziri Mkuu na Rais. Kama Mrema alikosea akavunja sheria na kujifanyia alilotaka, aliyepaswa kumkalisha kitako na kumuonya ni Waziri Mkuu na Rais na kama hakusikiliza au kufata amri aliyopewa, angefukuzwa kazi.
Hata alipokuwa Naibu Waziri Mkuu, kama cheo hicho hakikuwapo Kikatiba, ni kosa la aliyempa hicho cheo na wote wale walioridhia kuwa ni sawa na kuvunja na kukiuka Katiba, including Mrema mwenyewe.
Lakini kama leo hii Said Mwema na Masha hawawezi kufanya kazi mpaka Rais aseme, kwani kuna tofauti gani na Mrema alipokuwa akifuka kama povu na kuonekana mwendawazimu kama alichofanya kiliishia kwa yeye kuwekwa kitako Ikulu na kuambiwa nyamaza au sasa basi?
Mrema huyu huyu tunayemtuhumu kuwa alikuwa kichwa mbofu, waliokuwa Watawala walinufaika na alichokuwa anakifanya. Kwa jinsi alivyojizolea mashabiki, ndivyo Serikali aliyokuwa akiifanyia kazi ilipata sifa na kuimbiwa ngonjera nyingi na ndio maana Viongozi wakuu hawakujishughulisha naye mpaka pale Tume ya Nyalali ilipopendekeza kuwepo kwa Vyama vingi na shinikizo la Wahisani kwamba tuachane na mfumo wa Chama kimoja, ndipo kila mtu akabaini kuwa akiondoka Mwinyi, the most popular person ni Mrema.
Si kweli kuwa Mrema na Upinzani ulishindwa uchaguzi wa 1995 kwa ridhaa ya wananchi, CCM ilicheza faulo nyingi sana. Anzia Zanzibar jinsi Sefu alivyonyang'anywa tonge na Komandoo Salmini akabinywa kende na Mzee wa Kizanaki, njoo majimbo mengine ambapo CCM ilijiingiza kwa nguvu ya Dola na pesa na kuhakikisha kuwa inakuwa na nguvu kubwa Bungeni ya zaidi ya theluthi mbili za kura.
Hivyo pamoja na Umaarufu wake, CCM na Serikali ilifany akampeni kubwa sana ya kumwangusha Mrema na walifanikiwa kwa kuuvunjilia nguvu Upinzani na ule umaarufu wa Mrema.
Alichoshindwa kukielewa Mrema ni kuwa walichomsomesha CCM na UWT-TISS, kama mtu wa propaganda, ushushushu, kuvuruga watu na kutifuatifua, ni kuwa waliokuwa Waajiri wake, walitumia mbinu walizomwajiria kummaliza kisiasa na kuhakikisha Upinzani haushindi.
Hivyo kukurukakara za Mrema ni kutokana na mafunzo aliyopewa ya Propaganda za Kikomunisti. Tofauti yake na Kingunge ni kuwa Kingunge alielemea kwenye siasa na maneno, na Mrema ukachero na ushushushu wa kubinya watu makoo ndio aliutumia kwa dhati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, fani iliyokuwa ikifanana na alichosomea na kufundishwa (programmed).
Alipopelekwa Wizara ya kazi, mchezo ukageuka, na kama binadamu yeyote, ni vigumu kuwa makini na fanisi kwenye uwanja ambao huna uwezo.
Leo ukimpeleka Mhasibu akawe Mganga Mkuu unategemea nini?
Alichofanya Mrema kama mtumishi wa Serikali, kilikuwa na baraka za Serikali na Mkuu wa Serikali, na ndio maana hata vile vituo vya polisi pamoja na kuwa zilikuwa ni pesa za Wananchi, Serikali pia iligharamia na kuviendesha hivyo vituo na kupeleka Polisi, Silaha na Mitambo (Radio, Simu) na vifaa vingine vya kazi.
Nyakati zimepita, tupo kwenye vyama vingi, lakini mfumo haujabadilika, bado ni ule ule na ndio maana leo hii, kuna mvutano ndani ya Bunge na Serikali. Wabunge wanaona ni haki yao kuiwajibisha Serikali kuu, lakini Serikali kuu ya CCM inatumia Katiba ya Chama kuzima "Uhaini"!