TANZIA Augustino Mrema, Mwenyekiti wa chama cha TLP afariki dunia

Umeumaliza mwendo Mzee wa Kiraracha Augustino Lyatonga Mrema. Nenda Baba. Hakika Kwake Tutarejea. Pole Kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki na wengineo wote walioguswa na kuondoka kwake.
 
 
Mke wake WA Kwanza kumbe akifariki mwaka Jana...mwezi wa Tisa ...so wakati anajianda kuazimisha kifo cha mke wake Naye kafariki..hospital Ike Ile ya muhimbili
 
Jiwe kama kiongozi wa malaika ampokee rafiki yake salama
😂Yule anaweza Anza zile zake "nilikua nachomekea kidogo" katika Hotuba ya kumpokea mrema akajikuta anataja dhambi za mwenzie

Nasikia aliwahi kwenda msibani akajikuta ameropoka marehemu alikuwa na watoto wa nje😂
 
Lyatonga atakumbwa kwa zile purukushani za 1995 na NCCR kama ilikuwa kweli na sio project CCM, alitikisa sana.

Mabucha ya nguruwe yalileta shida sana na kufikia hatua ya kusomewa itikafu misikitini na waislamu.

Naibu waziri mkuu wa kwanza na mwisho katika nchi hii kama sijakosea.
Waziri asiye na wizara maalum wa kwanza na mwisho katika nchi hii kama sijakosea.

Mwisho wa siku akaupiga mwingi dakika za mwisho na kufunga pingu za maisha, Mzee hakupenda uzinifu kama wengine, amekufa akiwa kwenye ndoa.

RIP mwamba Lyatonga, mwendo umeumaliza, Mungu akurehemu.
 
Siasa za Tanzania baada ya Uhuru na kuelekea mfumo qa vyama vingi haiwezi kuelezewa kwa usahihi bila kutaja mchango wa kipekee alioutoa Augustino Lyatonga Mrema. Nimepokea kwa huzuni taarifa za kifo cha Mrema kwa masikitiko makubwa. Nawapa pole wafiwa wote ndugu, jamaa, na marafiki. Apumzike kwa Amani. Amina. JINA la Bwana Libarikiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…