Tatizo ni stori za movie na creativity hakuna siku Uzi. Kingine mliharibu pale mhindi alivyowalazimisha mshushe bei ya CD zenu pale ndipo mlipopoteza uthamani wenu ... Ilitakiwa mpande na sio mshuke. Sasa mnakazi kurudi kama zamani inatakiwa muinvest kwenye movie, igizeni na wasanii wa nnje na stori zenu zisijirudie rudie njoo na story mpya zile za mapenzi acheni na punguzeni tumeshazizoea. Fuateni mfano wa marehemu Steven kanumba basi. Alikuwa harudii stori mfano mdogo fake smile,stollen will,village pastoer, red Valentine,uncle JJ, n.k yaani alikuwa mbunifu kwa kweli toka amefariki nilifuatilia job kidogo tulitegemea ndio angekuwa mrithi wake lakini nae hana creativity ukichukua movie zake tatu alizotoa mfulululizo zinakaribia kufanana. Star wewe,main actor wewe,editor wewe,director wewe, producer wewe, script wrigter wewe. Unafikiri utakuwa na mawazo gani mmbadala hapo. Jifunzeni distribution of power na wekeni wataalaamu ktk kila sector kulingana na profession yake.