Aunt Ezekiel: Tununue bongo movie, movie za mbele hazituhusu

Aunt Ezekiel: Tununue bongo movie, movie za mbele hazituhusu

Kamwe siwezi nunua , wakawauzie ccm wenzao waliokuwa wanawashabikia , yaani mtu wa ukawa ukiwaungisha hawa wajinga unakuwa msaliti no 1
 
Picha linaanza....
Sterling-Vicent Kigosi
Story-Vicent Kigosi
Script writer-Vicent Kigosi
Director-Vicent Kigosi
Location manager-Vicent Kigosi

Kila kitu anafanya mtu huyo huyo saa muvi nzuri itapatikana vipi? Acha tu na mtazamaji awe huyo huyo Vicent Kigosi
 
Kinachoiua zaidi bongo movie ni instagram,wasanii hasa wa kike wana mashauzi sana wanapenda kujianika, maisha yao yote skendo zao hata za kipuuzi zote wanaweka mtandaoni(kuringishia watoto wao imekua fasheni),kiasi cha kuboa mashabiki,wakiambiwa ukweli wanajibu shobo na block juu. Nani anunue hizo kazi.

Kipindi insta haijawa maarufu sana bongo movie ziliuza kweli maana mashabiki wengi hawapendi kujua maisha binafsi ya wasanii wawapendao ila wasanii wetu wakaona kiki kujianika ili kuuza movie zao.

ILA KWENYE UKWELI TUWASIFIE BONGO MOVIE ACTRESS LAZIMA WAPATE TUZO YA KUJISILIBA MAKEUPS, KUVAA NGUO FUPI(PAJA NJE NJE). ACTORS WANAONGOZA KUWEKA DAWA NYWELE,PODA WANANISHINDA KUPAKA,WEUPE SASA SIJUI CAROLAIT ILE AU MAJI YA BETRI YALE.
 
Waendelee tu kuuza papachu maana ndo biashara inayowalipa zaid, mtu kujua kuchezea cumputer amekuwa dairecta. pumbafu kabisa, movie za mbele unaangalia mpaka raha.
 
Watu wengi wanazipotezea bongo movie kwasababu sio wabunifu wanatengeneza kazi mbovu yaani jambazi anavua viatu kuingia kufanya tukio!
20aecc8e906dc6be43d324f47c9fb8f2.jpg
Halafu basi ingekua movie ya msanii mchanga lakini hata huyu.
 
Nani aangalie takataka hizo,hyo hela bora nkahonge tu,afu wasivyo na aibu wanaweka part 1&2 kwa kipi hasa?,mtua anaoga anavaa anakunywa chai anatoa gari ana drive mpaka ofisini ndani ya scene moja.
Yaani unatoka kuangalia life of Pi ama Fast n furious 7 alafu unaniambia niangalie huo ujinga.afu kila muvi ina scene ya mganga,mi sound effect meengi kufosi kitu kiwe dramatic.pmbaf zenu
 
tunaanzaje sasa wakati muv ina part 1&2 lakini hata nje ya geti hawatoki muv inaanzia ndani inaishia ndani tena sitting room na bed room hata chooni hawaingii bhana
 
Wale wanamatatizo sana, mapenzi wanayajua sana yaani wanabusu hadi makarioni

Hawa watu ni maarufu kwa maisha yao nje ya sanaa.... Ila ukifwatilia upande wa sanaa utajiuliza why wanamwita super star
 
ila kiukweli bongo movie bado sanaa..zitaishia kutazamwa na house girls tu..
mwisho wa mwaka 2016 nilikuwa nafatilia tuzo za Korea kule nilichokuja kugundua mbali na vipaji walivyo navyo wale waigizaji pia ni wasomi sana wana masters za na degree za masuala ya uigizaji..
sasa imagine mtu anakipaji cha kuigiza jumlisha na elimu ya masuala ya uigizaji hapo kitu kinachotoka ni perfect combo😀😀😀😀😀

sisi tuna force kipaji na exposure ya masuala ya uigizaji Zero

yaani Mtanzania akiwa na makalio makubwa na sura nzuri tu basi nae anajua kuigiza WTF😛😛😛😛😛
 
Tatizo sio kupendelea vya g'ambo,mbona bongo fleva hawalalamiki kwamba tunapenda vya mbele? Mimi kidogo nilikuwa naangalia muvi za marehemu Kanumba (mungu amrehemu) kidogo alikuwa serious na kazi yake ila hawa wa kupaka tomato eti damu na mtu anaigiza ndo kahamka mdada huku kapiga makeup,kwakweli hawanipati mpaka wabadilike aisee.
 
Umeongelea angle nzuri sana.. Yaani umegusia kwa wasanii wenyewe... Hope kama watakuwa wanapitia hizi page na kusoma haya mawazo yetu..
Natamani siku moja nikae kuangalia filamu ya kibongo nikasisimka..
Yaani soko la filamu bongo lina changamoto kila idara.. Waigizaji.. Watunzi. Waongozaji.. Yaani shaghala baghala..
Mfano mzuri ni wahindi.. Yaani kiteknologia na uwekezaji wako nyuma bado tena sana.. Sema kinachowabeba na kuwapatia umaarufu ni simulizi zao.. Yaani unaweza ukaangalia ukajikuta unalia...
Wenzetu wako makini kiasi cha kukubali fanya mazoezi au kujikondesha ili kukidhi mahitaji ya role..
ukitoa Holwood ya Marekani, inayofuata ni Bolwood ya India
 
waache Kutunga story za kitoto yaani movie ukiangalia dakika 5 unaitabiri mpaka mwisho itaishaje.

Kuna watunzi kibao wazuri bongo watu kama Sultan Tamba,Hussein Issa Tuwa,Beka Mfaume wanaweza kuwatumia na wakapata story nzuri tu sio kila siku story zile zile za mapenzi.
 
Back
Top Bottom