Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hamna kitu kinaniuzi kama wazungu kuchukulia rangi nyeusi kama mikosi mashetani mabalaa majanga kisha nyeupe kuwa ndio rangi nzuri ndio maana hata sisi wa africa wanatufananisha na vitu vibaya baya kwa sababu ya rangi yetu (we are poor because we are poor) tuamke
Mkuuu plz naomba uni add katika hizo group nipate elimu hii adhim mkuu 0713522447
Au ni AURORA?
Angalia tena vizuri mkuu..
Rakims
Namba 2 ndo mnavyoeneza u-atheism wenu hivyo?
Mkuu hacha kutumia maandiko ya Mungu Kwa nia ya kupotosha wale wasioelewa chochote. Unatumia lugha nyepesi kuwafundisha watu ushetani! Elimu ya Kikristo ina mipaka yake hakuna mahali watu wanaruhusiwa kujifunza ushetani ispokuwa walio upande wa shetani. Kila Elimu ina makusudi, malengo na chimbuko lake( Mungu au Shetani)Kwanini usianzishe uzi wa mafundisho yako? Si kila kitu utakijua hata nikikuuliza reason ya kukufanya uone haya yanapinga mungu huna,
Kufahamu elimu zote ndio jambo sahihi na itakusaidia kuchambua mbivu na mbichi,
Haya vitabu vya dini vinahimiza kusoma mkuu,
katika kuzingatia hili Allah (s.w) anatukumbusha katika Qur-an:
"... Sema, Je! wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu." (39:9)
Jibu la swali hili ni wazi. Mjuzi na asiyejua hawawezi kuwa sawa kiutendaji na kitabia. Endapo mtu atajiita msomi kwa kusoma vitabu vingi au kupewa shahada nyingi lakini kitabia na kiutendaji akawa hatofautiani na wale wasiosoma atakuwa bado hajaelimika na mfano wake ni ule unaopigwa katika Qur-an: "Mfano wa wale waliopewa Taurati kisha hawakuichukua (kwa kuitia katika matendo) ni kama punda aliyebeba (mzigo) wa vitabu vikubwa (bila ya kufaidika kwavyo) ni mbaya kabisa mfano wa watu waliokadhibisha aya za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalim (62.5)
Nafasi ya Elimu na wenye elimu katika Uislamu
Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo: Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.Tunajifunza katika Qur-an kuwa jambo la kwanza alilotunukiwa Adam (a.s) mara tu baada ya kuumbwa kwake ni kupewa elimu. "Na (Mwenyezi Mungu) akamfundisha Adam majina ya vitu vyote..." (2:31) "Majina ya vitu vyote" katika aya hii inaashiria fani zote za elimu ambazo anahitajia mwanaadamu hapa duniani ili afikie kwa ufanisi lengo la kuumbwa kwake. Pia tunajifunza katika Quran kuwa mwenye elimu na hekima amepewa kheri nyingi. (Mungu ) humpa hikma amtakaye, na aliyepewa hikma bila shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili. (2.269).
Kutafuta elimu (kusoma) ni amri ya kwanza kwa mwanaadamu. Tunajifunza kutokana na historia ya kushushwa Qur-an kuwa Wahay wa kwanza kumshukia Mtume (s.a.w) ambao ndio ulimtawazisha rasmi kuwa mtume ni ule unaopatikana katika aya tano za mwanzo za Suratul-'Alaq:
"Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba.Ambaye amemuumba mwanaadamu kwa 'Alaq (kitu chenye kuning'inia). Soma na Mola wako ni karimu sana. Ambaye amemfundisha mwanaadamu kwa kalamu. Amemfundisha mwanaadamu (chungu ya) mambo aliyokuwa hayajui".(96:1-5)
Kutokana na aya hizi, kwa muhtasari, tunajifunza yafuatayo:
1. Kusoma kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni jambo la kwanza waliloamrishwa wanaadamu na Mola wao.
2. Kusoma kwa jina la Mola wako ni kusoma kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu au ili kuweza kumwabudu Allah(s.w) inavyostahiki na kusimamisha Uislamu katika jamii.
3. Radhi za Mwenyezi Mungu zitapatikana pale mwanaadamu atakapoweza kufikia lengo la maisha yake la kumuabudu Allah (s.w) kwa kuzingatia maamrisho na mipaka ya Mwenyezi Mungu katika kila kipengele cha maisha.
4. Amri hii ya kusoma hailengi fani maalum tu ya elimu; bali kila fani itakayomuwezesha mwanaadamu kufikia lengo la maisha yake kwa ufanisi.
5. Chanzo au chimbuko la fani zote za elimu ni Allah (s.w). Hivyo kwa Muislam mlango wa kwanza wa elimu ni kusoma kwa mazingatio Qur-an na hadithi sahihi za Mtume (s.a.w) na kusoma maarifa ya Uislamu kwa ujumla kutokana na vyanzo hivi viwili.
Christians wanasema:
Elimu ni uzima
Mithali 4:13
"Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako."
Neno la ufahamu
Elimu ni maelekezo ya namna ya kuishi duniani, lakini elimu itokayo kwenye Biblia hutuelekeza hata maisha ya milele kule mbinguni.
Ubarikiwe! Mkuu Mr. Mangi
Rakims
Hacha = AchaMkuu hacha kutumia maandiko ya Mungu Kwa nia ya kupotosha wale wasioelewa chochote. Unatumia lugha nyepesi kuwafundisha watu ushetani! Elimu ya Kikristo ina mipaka yake hakuna mahali watu wanaruhusiwa kujifunza ushetani ispokuwa walio upande wa shetani. Kila Elimu ina makusudi, malengo na chimbuko lake( Mungu au Shetani)
No man can perform Supernaturally by himself unless has got assist from either true God or Satan knowingly or unknowingly.