Habari mkuu, mimi aura za baadhi ya rangi nimeshaziona ila sijajua namna ya kuzifaidi.
Mfano rangi ya blue hutoa aura ya chungwa
Nyekundu hutoa aura ya kijani
Njano hutoa pink iliyopauka
Nyeusi hutoa aura nyeupe
Nyeupe hutoa aura nyeusi
Kijani hutoa zambarao nk;
Pia nikiangalia chochote huwa nahama na kimvuli chake au nikisoma hata bango mahali huwa naondoka na copy ya maandishi hayo kwa muda
Pia wakati naanza hii kitu nilikuwa nachukua muda sana kuona aura lakini sasa kuna time najishtukia kuona rangi kali ya ghafla isiyopo kwenye mazingira yangu na mara paahp naduwaa na kuanza kuchunguza na baada ya muda nagundua kuna rangi iliyopo karibu unakuta nimeona aura yake bila kutegemea unakuta nimepitisha tu macho hapo.
Pia kuna vingine huwa havina aura ila nikivitazama na kuondoa macho huwa naondoka na vivuli/ramani zao/vyao.
Pia kisimama kwenye jua nikafumba macho kwa muda kama sekunde 15 na kuendelea, nikifumbua tu macho mazingira yote nakuta yamekuwa ya kijani yote hata kama mazingira hayo hamna rangi ya kijani.
Kwa upande wa aura za watu sijaona isipokuwa naona vizuri kabisa aura za nguo walizovaa ila naona tu ramani za miili yao.
Nisaidie mkuu natanguliza shukrani