Humu watu wanaleta matatizo yao, watu wanashauriana kwa experience na knowledge walionayo... Ni mhusika mwenyewe anaamua kufuata au kutofauta.
Mimi nilikuwa na ndugu yangu aliumwa akawa anapgwa ganzi ilianza vidole vya miguuni ikapanda hadi kiunoni, anaishi miguu inawaka moto inakaza halali kutembea hawezi, tumezunguka hospital anatumia dawa lakini wapi.
Kuna mtu humu si daktari alishauri atumie dawa inauzwa 12000 wakat hapo tulikuwa tumeshatumia ela nyingi, tumetembelea hospitali kibao.
Ile dawa alipoanza kuitumia alianza kupata nafuu mpaka leo yuko sawa anatembea yuko vzuri na hiyo ilikuwa 2017 hadi 2018.
Na watu wengi huwa wanakuja humu baada ya kuwa wanaona matibabu wanayopewa hayaleti matokeo.