Sun is Sun
JF-Expert Member
- Mar 13, 2024
- 1,254
- 2,014
Nataka kushiriki uzoefu wangu kama somo kwa wengine. Nilicheza mchezo wa Aviator, ambao walisema ni 'provably fair', lakini kwa kweli nilipoteza hela nyingi sana. Mchezo huu uliharibu hali yangu ya kifedha na kuniacha na pressure kubwa ya akili.
Zaidi ya hasara ya pesa, niliona pia jinsi ulivyoniathiri kimasomo. Nilipoteza muda mwingi nikicheza, nikiwa na mawazo ya kujaribu kurudisha hasara. Hii ilisababisha kuwa na umakini mdogo kwenye masomo, kuchelewa kumaliza kazi za chuoni, na kupoteza baadhi ya fursa za kujifunza.
Mbaya zaidi, nilishindwa kununua hata mahitaji ya msingi kama . Hii ilisababisha stress kubwa na kunifanya nihisi kupoteza udhibiti wa maisha yangu.
Nilijifunza kwa njia ngumu kwamba michezo ya kubashiri mtandaoni inaweza kuharibu malengo yetu ya elimu, maisha, na mahitaji ya msingi.
Hii ni onyo kwa vijana wenzangu: michezo inayodaiwa kuwa ‘fair’ si kila wakati inakuweka kwenye nafasi salama. Tukijihusisha na michezo kama hii, tunakosa malengo yetu, tunapoteza muda, na wakati mwingine hela zetu za muhimu huisha haraka. Tafadhali kuwa makini na michezo ya kubashiri mtandaoni jua hatari zake kabla hujashiriki.
Mimi nimejifunza kwa njia ngumu, lakini natumai wenzangu wataepuka hatari hii.
Mwenye sikio na asikie.