Awamu ya 5 imeongeza mishahara ya Watumishi kwa njia ya kupunguza kodi ya PAYE

Awamu ya 5 imeongeza mishahara ya Watumishi kwa njia ya kupunguza kodi ya PAYE

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wapinzani wamekuwa wakieneza propaganda kwamba serikali haiwajali Watumishi na kwamba haijawaongezea mishahara kwa miaka 5 sasa.

Hii si kweli, kuna njia mbili za kuongeza mshahara wa mtumishi ikiwa ni kuongeza mshahara ghafi au kuongeza net salary (take home).

Serikali ya awamu ya 5 imetumia njia ya pili ya kuhakikisha mshahara wa kwenda nao nyumbani unaongezeka ndio maana kila mwaka kodi ya Wafanyakazi PAYE imekuwa ikishuka na sasa imefikia 9%

Kwahiyo ni ukweli usiopingika kuwa mshahara umeongezeka kila mwaka baada ya PAYE kupungua to single digit.

Ijumaa kareem.

Maendeleo hayana vyama!
 
johnthebaptist,

Ignore inakuhusu kwakweli sina namna. Ebu waeleze wanajamvi hii aslimia imeshuka kuanzia mwaka gani?

Hivi unadhani mtumishi anaumia kwa PAYE peke yake, bora hiyo aslimia ingebaki ila ya HESLB wakawapunguzia kurudi awali na waliomaliza waongezewe tu mishahara maana ni haki yao.

Baada ya apo nakupiga ignored. Ahsante sana JF kuweka hii option.
 
Ignore inakuhusu kwakweli sina namna, Hebu waeleze wanajamvi hii aslimia imeshuka kuanzia mwaka gani? Hivi unadhani mtumishi anaumia kwa PAYE peke yake, bora hiyo aslimia ingebaki ila ya HESLB wakawapunguzia kurudi awali na waliomaliza waongezewe tu mishahara maana ni haki yao.

Baada ya apo nakupiga ignored. Ahsante sana JF kuweka hii option.
Bwashee hilo la mkopo ni swala binafsi siyo la watumishi wote!
 
1. Nina hakika wewe sio Mtumishi wa Umma hivyo hauna unacho kifahamu

2. Hakuna mtimishi wa umma aliepongeza kwa " dhati " hicho ulicho kiongea kwasababu watumishi wa wanahitaji nyongeza ya mshahara na si pungozo la kodi

3. Je, unajua nikiasi gani kimeongezeka katika mishahara ya wafanyakazi?

wakati mwengine ni bora kukaa kimya kuliko kuongea vitu usivyovielewa
 
Mchezo unakuwa kama ifuatayo.

1. Unaongeza makato ya bodi ya mikopo (Hesbl) karibia na nusu iliyokuwepo 2016.

2.Haupandishi madaraja wala nyongeza ya mshahara 2015-2020

3.Unakuja punguza asilimia za kodi mwishonii 2020 ili tupate kura.

Yaan kama mtu unakumbukumbu nzuri angalia mshahara ulokuwa wapokea 2014 na mshahara unaopokea baada ya hiyo kodi kushushwa 2020 utapata jibu.
 
True
Hajangeza Nominal wage yeye anaongeza Real wage
 
Miye naichukia awamu hii sehemu moja tu kuongeza makato ya walionufaika na mkopo wa elimu ya juu na kuongeza riba ya deni kila mwaka hapo ndio hufanya nione hii awamu ya tano haipo fair kabisa
 
Back
Top Bottom