Mkuu
Hiyo shilling 400 bado ni rahis maana tunalipia na madeni ya iptl escrow na richmondi na ufisadi humohumo. Ila kimsingi kama tunalipa 400tsh wa gas tutalipa 2000 per unit.
Kina kupungua kule yawezekana kinapungua sababu kunajaa tope na miti na hatuna tamaduni ya kurekebisha mabwawa kuyachimba na kutoa uchafu toka miaka 100 iliyopita.Basi tuweke imani yetu kwa Mungu ambae hataruhusu maji yakauke kama vile anavyofanya Mtera na Kidatu ambako kina cha maji hakipungui hata siku moja.
Amandla...
Sio philosophically, gas ni yetu. Lakini hii haimaanishi kwa sababu ni yetu basi tuchukue bure kwa mtu aliyewekeza kuitoa. Itakuwa Kama mtu mwenye duka halafu anataka bidhaa zake achukue bure kwa sababu alizinunua. Hilo duka litafilisika mapema sana. Mwekezaji anauza hiyo gesi kwa niaba yetu na kwa namna tulivyokubaliana. Mkataba wetu ukiisha ataiacha gesi iliyosalia na hata ondoka nayo ambapo ingekuwa yake basi angeibeba iliyosalia.Ni kweli, tatizo na gas tulishawapa yote.
Philosophically gas ni yetu iko Tz lakini kiuhalisia tulishaigawa siyo yetu tena. Hivyo mitambo ya gas itakulazimu kununua gas huo ndo uhalisia.
Mkuu400 tsh ni umeme wa sasa wa gas, sasa hiyo 2,000 ni ipi tena, au unachanganya notice nini bro?!
Mkuu nina uhakika na niachoongea.Hapo ndipo unakosea. Unaamini kuwa tutaweza kuzalisha umeme kwa miaka 50 mfululizo bila matatizo. Tujifunze kutoka Kidatu na Mtera. Unaposema gharama za uendeshaji ni ndogo unakuwa hujaweka gharama za kuondoa tope mara kwa mara ambalo kwa mazingira ya mto Rufiji litakuwa linajaa haraka sana. Haujaweka gharama za uharibifu wa Rufiji Delta na hasara watakayopata watu ambao wanaitegemea kwa uhai wao. Samaki, prawns, mikoka n.k. yote itaathirika. EIA ya mradi ilisema hivyo ndio maana marais kuanzia Mwalimu mpaka Kikwete hawakuutaka huu mradi. Hili ni jiwe tunajifunga shingoni wakati tunaenda kuogelea.
Amandla...
Mkuu imebidi nicheke tu, eti umeme wa maji ni rahisi, ila itategemea viongozi wetu wataamuaje. Umeme wa fedha za mkopo utakuwaje bei rahisi? Huo ukweli wa kiinjiania hauna maana yoyote kwetu sisi watumiaji, nasisitiza hakuna umeme utakuwa rahisi kwetu, uwe wa maji, au gas, nyingine hizo ni porojo za furahisha genge.Issue ni kuwa hatuzalishi umeme wa maji kwa wingi, hivyo bado tunanunua umeme kutoka kwenye makampuni yanayozalisha umeme, ndio maana Bei bado ipo juu.
Hata hili bwawa likiisha bado umeme unaweza usishuke Bei, itategemea na viongozi wetu wataamuaje.
Lakini ni kweli kabisa umeme wa maji ni umeme rahisi.
Matope yanaletwa na maji. Na maji ndio mto.Kina kupungua kule yawezekana kinapungua sababu kunajaa tope na miti na hatuna tamaduni ya kurekebisha mabwawa kuyachimba na kutoa uchafu toka miaka 100 iliyopita.
Kupungua kwa kina si sababu ya maji sababu zingine maana mpaka may mwaka huu mvua na mafuriko yalikuwa mengi na imekuwa hivyo for good past 6 years.
[emoji1787]Huu mradi wa strogious gourge ni upi mkuu?
Hebu tushirikishe mkuu.Mkuu imebidi nicheke tu, eti umeme wa maji ni rahisi, ila itategemea viongozi wetu wataamuaje. Umeme wa fedha za mkopo utakuwaje bei rahisi? Huo ukweli wa kiinjiania hauna maana yoyote kwetu sisi watumiaji, nasisitiza hakuna umeme utakuwa rahisi kwetu, uwe wa maji, au gas, nyingine hizo ni porojo za furahisha genge.
Unalinganisha machungwa na apple. Inabidi ulinganishe vyanzo vya maji vya Hoover na vya kwetu. Hata hivyo hata huko, kina cha Lake Mead sasa hivi kiko chini kuliko wakati wowote toka hiyo dam ijengwe kutokana na mto Colorado kuathirika na ukame kwa zaidi ya miaka kumi sasa.Mkuu nina uhakika na niachoongea.
Unless unamaanisha kuwa unajenga dam halafu wewe unaenda zako kusiko julikana na unakula bata raha mustarehe bila kufanya periodical maintainance.
Edgar Hoover Dam, ambalolilijengwa miaka zaidi ya 85 iliyopita , bado linatumika leo.
Na hili dam la Edgar Hoover linalingana kabisa na tnalolijenga leo , bwawa la Julius Nyerere Hydroelectric Power Project(JNHPP), lenyewe lina installed capacity ya 2080 MW, wakati la kwetu litakuwa 2115MW.
Tofauti kubwa hapo niwatu wanaoliendesha na kutunza mabwawa hayo.
Kama tutakuwa na watu kama wa Mtera na Kidatu, basi hata hilo la kwetu la JNHPP halitadumu.
Wenzetu Edgar Hoover limedumu kwa miaka 85 sasa.
Matatizo ya Mtera na Kidatu siyo ya miradi yenyewe bali ya kisiasa.
Watu wanalima hadi kingo za mito na mchnga/tope zinaenda kujaza bwawa.
Utamlaumu nani.
Bila maintainance hata itambo ya gesi ukaiwasha halafu wewe ukaenda kulala, inaknock au kuunga baada ya mwezi tu.
Symbion na IPTL waliletwa baada ya upungufu mkubwa wa uzalishaji uliotokea. Kutokana na hali ya emergency ndio watu wakapiga humo humo. Utasemaje kupungua kwa kina kulikuwa proganda? Una maana maji yalikuwepo lakini wajanja waliyaficha?Kuhusu mabwawa kupungua kina ilikua ni propaganda tu ya kuhalalisha symbion kutuuzia umeme.
Linatengenezwa tatizo ili watu wapate nafasi ya kuleta kampuni ituuzie umeme alafu wachukue 10%
Hilo ndio kinafanywa na serikali ya CCM
Kuhusu kuwa inaweza kutokea Tena kwenye stieglers gorge au laa hiyo hatujui.
Kwa nini hakuna mwekezaji wa maana huko, sababu ni kuwa hili bwana ni letu halimilikiwi na mtu yoyote.
Wawekezaji hawawezi kupenda hii project kwa kuwa ikatokea tukawa na umeme wa uhakika Ina maana hatutaweza Tena kununua umeme kutoka kwao.
Nakubaliana na wewe 100%, kuwa na umeme rahisi ni ngumu kwa nchi yetu na serikali hii yetu.Mkuu imebidi nicheke tu, eti umeme wa maji ni rahisi, ila itategemea viongozi wetu wataamuaje. Umeme wa fedha za mkopo utakuwaje bei rahisi? Huo ukweli wa kiinjiania hauna maana yoyote kwetu sisi watumiaji, nasisitiza hakuna umeme utakuwa rahisi kwetu, uwe wa maji, au gas, nyingine hizo ni porojo za furahisha genge.
Nimemwomba Tindo atushirikishe, tutapata wapi umeme wa bure, mpaka sasa yuko kimya!Nakubaliana na wewe 100%, kuwa na umeme rahisi ni ngumu kwa nchi yetu na serikali hii yetu.
Nilichomaanisha Mimi ni kuwa umeme wa maji ni rahisi kuliko gesi, Ila kwa serikali yetu huo urahisi hautakuwepo.
Huko ndiyo kujihalalishia umasikini.Unalinganisha machungwa na apple. Inabidi ulinganishe vyanzo vya maji vya Hoover na vya kwetu. Hata hivyo hata huko, kina cha Lake Mead sasa hivi kiko chini kuliko wakati wowote toka hiyo dam ijengwe kutokana na mto Colorado kuathirika na ukame kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
Mazingira yetu ni ya udongo wakati wenzetu wana miamba zaidi. Ndio maana Norway wanazalisha umeme wa maji kwa bei nafuu sana kuliko sehemu nyingine yeyote.
Wakulima wataendelea kulima. Na hii inachangia upungufu wa maji kwa sababu wengi sasa wanalima kilimo cha kumwagilia maji. Nenda kaangalie mashamba ya vitunguu Iringa. Huu mradi ni tembo mweupe na tutalia sana na kusaga meno. Na kama kawaida yetu tutawanyooshea vidole mabeberu ingawa ni sisi wenyewe tumekaidi tahadhari zao.
Amandla...
Mkuu kwenye post zangu zote acha hii tu, hakuna popote kuna neno bure bali bei. Au unataka kubadilisha mantiki nini?Hebu tushirikishe mkuu.
Huo umeme wa bure tutaupata wapi?
Nakubaliana na wewe 100%, kuwa na umeme rahisi ni ngumu kwa nchi yetu na serikali hii yetu.
Nilichomaanisha Mimi ni kuwa umeme wa maji ni rahisi kuliko gesi, Ila kwa serikali yetu huo urahisi hautakuwepo.
Hapana. Umasikini ni kushinda ukitaka kuvumbua gurudumu lako lisilokuwa la mviringo kwa sababu tu hautaki kutumia la uviringo kwa sababu ni jirani yako aliyelivumbua.Huko ndiyo kujihalalishia umasikini.
Mbaya zaidi ni kufikiri vya wenzetu ni bora kuliko vya kwetu.
Hakuna maendeleo bila challenges, na ukikutana na challenges unayoosha mikono, huko ndio kujihalalishia umasikini kwenyewe.
Poor in thinking. poor in deed and ultimately accepting your poverty as God sent.
Tusizunguke mbuyu.Hapana. Umasikini ni kushinda ukitaka kuvumbua gurudumu lako lisilokuwa la mviringo kwa sababu tu hautaki kutumia la uviringo kwa sababu ni jirani yako aliyelivumbua.
Nchi zote zilizoendelea hazikusita kutumia vitu vya mwenzao kama ni bora zaidi kuliko ya vya kwao. Ndio maana miradi kama Nyumbu ilishindwa. Na mradi wa jirani zetu wa Volkswagen utafanikiwa.
Mtu makini akikutana na challenges anaangalia mwenzake alifanikiwa vipi kuzikabili. Anachojifunza kutoka kwa mwenzake, anaboresha ili kiendane na mazingira yake. Kwa mtazamo wako unaona ni bora tugundue simu ya mkononi ya kwetu kuliko kumshawishi Samsung aje ajenge kiwanda cha simu hapa kwetu. Wahindi walitengeneza Bajaj baada ya kumkaribisha Vespa ajenge kiwanda nchini mwao. Wametengeneza Maruti baada ya wao kumkaribisha Suzuki ajenge kiwanda chake ingawa tayari walikuwa wanatengeneza magari yao wenyewe.
Isolation breeds poverty. Kama ilivyo kwa North Korea.
Amandla...
Hiyo ni opinion yako. Opinion yangu ni kuwa huu mradi tutaujutia maisha yetu yote. Na watoto na wajukuu zetu watatulaani kwa kuwaharibia future yao na kuwatwika mzigo usio na faida yeyote.Tusizunguke mbuyu.
Mpaka sasa mradi wa JNHPP utakuwa cost effective kwa miaka mingi ijayo, ukilinganisha na mradi mwingine wowote ujao.