Awamu ya Tano iliua UDART, hili tuliseme wazi si kumung'unya maneno

Hayo unayotoa ni mawazo tegemezi ya mtu anayeshindwa kufikiri nje ya box.
Ati mtu hajawahi kuendesha mradi kama huo duniani!
My foot!
Nyie bongolala mmejiaminisha kuwa hamuwezi kitu mpaka mzungu awatie boost.

Mtaamka lini?
Mtimanyongo wenu unaua ari ya uwekezaji wa Watanzania.
Mfanyabiashara akiwekeza kigezo lazima kiwe faida na gharama za uendeshaji.
Walioajiriwa huwa hawajui hii fact.
 
marehemu POMBE alikuwa anapigwa daily na wajanja aisee nashangaa ule ubabe wake wote lkn bado wahuni wa mjini wamepiga hela ndefu Sana hakika wezi WA nchi hii wanatisha
Hapana Mkuu. Jiwe alikuwa akiwabana watu wa kundi fulani ili wa kundi lake waweze kufaidi. Yaani alikuwa akiwapora chakula mezani na kuwapa anaowapenda.
 

Haha, uzi wako ulikuwa sio wa kuongelea matatizo ya mwendo kasi ila ni kunyoosha vidole utawala wa awamu ya tano.

Kama mwekezaji alikuwa anajuwa kigezo chake ni faida, kwanini alitaka kwenda kinyume na mkataba kwa kupandisha nauli wakati hakuna viashiria vyovyote vilivyo support upandishaji wa nauli? Bei ya mafuta ilikuwa ile ile, thamani ya shilingi haikubadilika sana, mfumuko wa bei ulikuwa unazidi kushuka, maishahara haikupanda. Kama sio ulafi na ubinafsi ni nini?
 
Sasa lipo Bora? aliyekua anapandisha nauli kwa shiling Mia ili kampuni iendelee na kuua kamupini isiwepo.
 
Rais ni Taasisi kubwa sana ina kila kitu inauwezo mkubwa sana, lawama lazima ibebe lawama kwa parfomance poor ya mradi wa UDART
 
Serikali haiwezi kufanya biashara
Rais ni Taasisi kubwa sana ila kila kitu inauwezo mkubwa sana, lawama lazima ibebe lawama kwa parfomance poor ya mradi wa UDART
 
Umewahi kujiuliza kwanini Maxmalipo alipigwa Chini?

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Yeye spika aliingia bungeni kwa uadilifu? Pale jizi la kura linapowatuhumu watu kuwa sio waaminifu.

[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2445][emoji2445][emoji2445][emoji377][emoji377][emoji377]
 
Rais ni Taasisi kubwa sana ila kila kitu inauwezo mkubwa sana, lawama lazima ibebe lawama kwa parfomance poor ya mradi wa UDART
Lakini si ni kampuni binafsi ndio ilikuwa na mamlaka ya kuendesha UDART kulingana na makubaliano ya mkataba? Sasa taasisi ya rais itaingiliaje uendeshaji bila ya kuwa na sababu za msingi? Serikali inatakiwa kuingilia pale tu inapoonekana kampuni inaendeshwa shughuli zake kinyume na makubaliano.
 
You must be crazy and misinformed! Usijiandikie tu! Haya ndo yanayochotwa na wabunge na baadhi ya wana JF wasiokuwa na uelewa na kuwapotosha.
Hapakuwa na mwekezaji mwenye mtaji bali mtu tapeli na mwizi. Serikali ilidai hisa zake na zile za jiji. Iliidai UDA yake iliyochotwa kitapeli, sasa ulitaka aachiwe wizi wa wazi? Andikeni kama wenye uelewa na siyo mashabiki wa watu washenzi tu!
 
weka ushahidi hapa
 
Story kama hizi naomba tafadhali msimulie nyanya yako ndiyo atakusikiliza na kukubali lakini sio sisi.
 
Udart sasa nao wapo kwenye kutumikia karma ya maxcom na karma ya kudhulumu wafanyakazi stahiki zao ikiwemo mafao.

Ukweli hawa watendaji wasio na ujuzi na mambo ya magari ni tatizo sana kwa taasisi nyingi + ukabila uliokuwa umetamalaki kwenye huo mradi ni lazima haya yajitokeze, management iliyoshindwa kuendesha daladala zilizopewa njia bila mshindani kule mnazi mmoja kivukoni na baadae kwenye huu mradi kamwe hawakustahili kupewa hiyo nafasi, maana waliwaletea figisu maxcom wanawaibia pesa wakatolewa wakaanza kukusanya wao Pesa majumbani kwa watu na mifukoni, TTCL Sijui kitu gani kiliwashinda kirejesha mfumo kama ule wa awali wa maxcom, haiingii akilini Mashine za Ku swap kadi na ticket zipo na zimeagizwa kwa Pesa nyingi, cha kuzisimamisha kwa miaka mitatu ni hujuma kubwa sana hii.


Ukirudi kwa wafanyakazi waliomaliza mikataba wengi wao mafao yao na hata michango yao ya kila mwezi haikupelekwa hii pia ni uzembe au kuna watu walikuwa wananufaika na ucheleweshwaji wa kupelekwa kwa michango kwenye mifuko husika.

Miaka mitano sasa ni aibu mradi ule wa mabilioni kushindwa kujiendesha kwa faida na inasikitisha wao mishahara haikosekani ila faida na malipo kwa wastaafu hakuna.

Nitarudi baadae mjukuu wangu analilia simu.
 
Mwajiriwa kila Hela inayooingia Ofisini anajua faida

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…