kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Ninaingalia Tanzania na na idadi ya Mikoa, Wilaya, Tarafa, Kata, Vijiji na Vitongoji vyake na idadi ya miradi ya maendeleo inayoguza moja kwa moja mikoa, wilaya, tarafa, kata na vijiji kama vile maji ya kunywa, barabara, madaraja, shule, hospitali, umeme, ujenzi wa huduma za benk. viwanja vya ndege, vyombo vya usafiri, na kutembelewa na viongozi wakuu wa kitaifa kutatua kero zao utaona kuwa kuna baadhi ya kanda, mikoa, wilaya, tarafa, kata na vijiji vya upande mmoja wa nchi vilinufaika zaidi kuliko kwingine.
Viongozi wetu tengenezeni dira ya vipaumbele vya taifa kutokana na uhitaji na rasilimali zilizopo. Hii itaepusha kutoa huduma kwa kufuata aneo alikotoka kiongozi kwanza kwa njia ya upendeleo. Mwisho wa siku taifa letu litaathiriwa na siasa za ukabila, ukanda, umikoa, uwilaya, utarafa, ukata na uvijiji huko tuendako. Mambo hayo aliyaepuka sana Mwl Nyerere na Mzee Karume wakati wa Urais wao. TUsikubali kamwe mambo haya yakolee kwenye taifa letu.;