Awamu ya tano ndiyo ya hovyo kuliko awamu zote

Mbona huyo mbunge aliyeugua Corona Makonda hamsemi?? Au kwa kuwa ni ccm. Bashite ni bogus kabisa.
 
Jitihada zinazofanywa na kamati zilizoundwa pamoja na wakuu wa mkoa ili kuthibiti kusambaa kwa maambukizi ya corona wewe huoni

Endelea kulaumu wanaume wako kazini
Kwa vile umemaliza kuandika kalale.

Ingeundwa kamati ya wataalam ili kukabiliana kikamilifu na kusambaa kwa corona virus. Wakuu wa mikoa kimsingi ni wawakilishi wa m/kiti wa chama tawala wa mkoa husika. Wana utalamu gani hawa?
Huzioni jitihada za Mseveni, Kenyata, na Kagame? Mapambano dhidi ya corona virus ni vita ingawa adui haonekani.
Rais ndiye Jemadari mkuu; anabakije nyuma? Amewatanguliza ummy mwalimu, makonda, na PM.
Tuendelee kuomba kila mtu kwa imani yake wakati kasi ya ongezeko la maambukizi ina sura ya "arithmatic progression". Pamoja na dua na sala kwa siku 3, wiki ijayo siku kama ya leo idadi ya wagonjwa wa covid 19 itakuwa imepindukia 500. Watu wajinga watadai nashabikia!
 
Tuombe isifike huko aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ya hovyo sana
 
Eti bora kuwa mbwa ulaya kuliko kuwa mtu afrika...hahaha
 
Rais yuko chato kuonesha mfano wa lockdown, sio lazima tuambiwe wandugu tutazame picha na matendo inatosha.

Kesho nafunga ofisi huyo kujilockia ndani, why? Because my Boss is also on the same boat of stay home, stay safe!

Wandugu zangu, tuweke siasa pembeni, tuweke lawama pembeni (ktk hili watanzania tumebarikiwa, Mungu atuponye sote)....HUU NI WAKATI wa WEWE MWENYEWE kujali afya yako.

Hatupaswi kuendelea kulaumu tu bila kuchukua hatua...TUAMKE watanzania, akifa mwenzi wako, mtoto, kaka au dada au mzazi unaumia wewe sio viongozi na sio serikali. Ni kweli kuna uzembe na mzaha, lakini je, tuongeze tatizo juu ya tatizo? La Hasha! Ni wakati kujitetea na kumtetea wa karibu yako, TUPAMBANE na adui, tukinyamaza na kutaka wengine wamchakaze huenda wakafeli tukaangamia sote au wakamteketeza na kubakiwa na majeraha makubwa.

Nukupenda Tanzania, Nawapenda Watanzania
 
Mloganzila imefurika wagonjwa wengi
 
Namtafakari Magufuli sipati majibu..
Yani simuelewi kabisaa
Huyu ni janga lingine la taifa. Tutakapozinduka usingizini tayari tutakuwa tumeshaangamia.
 
Kuna kitu hakipo sawa kuhusu awamu hii namna inavyoshughulikia majanga makubwa yanayoikumba nchi na wananchi, kimsimgi kuhusu majanga wananchi hawajawahi kupata msaada wowote wa maana wa kuwasaidia kutoka serikalini refer ishu ya njaa watu waliambiwa serikali haitaoa chakula cha bure refer tetemeko kule kagera wananchi walivyojibiwa na meko tuje kwenye hili la sasa hatuoni za dhati kabisa yani hatua wanazochukua wao sio level za hatua za serikali inayotakiwa izichukue... Nisahihishwe kama nimekosea
 
Hakika nakuunga mkono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…