Aweso akagua ukarabati wa bomba la Maji Dar

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200

Hivi Aweso ataacha lini hizo drama?!

Jana, Makala kasema issue ni upungufu wa maji ajabu leo Waziri husika anadai uharibifu wa bomba.

Nchi hii!!

----
WIZARA YA MAJI YAUNGANA NA DAWASA CHANGAMOTO YA HUDUMA DAR

Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso (Mb) ametembelea eneo la matengenezo ya bomba kubwa la inch 72 katika kata ya Wazo, Jijini Dar es salaam ambalo ni sehemu ya kimkakati ya kuongeza msukumo wa Maji katika Jijini Dar es salaam ili kukabiliana na hali ya kina cha maji kupungua na kuhakikisha matengenezo hayo yanakamilika.

Akiwa eneo hilo, Aweso ametumia nafasi hiyo kutoa tamko la Serikali juu ya njia mbadala za kupambana katika kipindi hiki cha upungufu wa huduma ya Maji kwa kuruhusu wenye visima binafsi kuwahudumia Wananchi.

Akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe Godwin Gondwe na Afisa Mtendaji Mkuu-DAWASA, Cyprian Luhemeja, Mhe Aweso amesema Serikali ipo bega kwa bega na Wananchi wa Jiji la Dar es salaam na Pwani katika kipindi hiki na kuitaka Mamlaka ya Maji (DAWASA) kuhakikisha migao ya maji iliyowekwa kufuatwa bila ubabaishaji ili kutoa haki kwa kila mwananchi kuhifadhi maji ya kutosha wakati huu.

"Niwaagize DAWASA kuhakikisha ratiba ya mgao inasimamiwa na kufuatwa kikamilifu kama ilivyopangwa.
Pasitokee janja janja yoyote itakayosababisha lawama au upendeleo.

Niseme kuwa Serikali imeruhusu matumizi ya maji ya visima binafsi na vya umma ili vitumiwe na kuendelea kutoa huduma kwa Wananchi bila kikwazo chochote hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo" alisisitiza Mhe Aweso

"Wenye visima binafsi toeni huduma sasa ili wananchi wasiteseke na huduma hii.
Wizara inayo mipango ya muda mfupi ikiwemo kuanza kutumia maji ya mradi wa Maji Kigamboni ambao utawashwa Oktoba 30. Amesema mradi unatarajiea kuzalisha takriban lita milioni 70 za maji ambazo zitasambazwa Kigamboni na maeneo ya katikati ya jiji" ameongezea Mhe Aweso

Waziri Aweso ameongeza kuwa hivi karibuni utiaji saini wa kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa Maji Kidunda utafanyika mwezi Novemba mwaka huu na kushuhudiwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassani.

Mradi wa Kidunda ni suluhisho la kudumu la upatikanaji wa maji ghafi katika Mto Ruvu kwani litatumika kukusanya maji wakati wa mvua na maji hayo yatatumika nyakati za kiangazi.
 
Yale Yale ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma na aliyekuwa waziri wa elimu juu ya makambi ya wanafunzi niliona kituko watu kuona Mtaka alikuwa kituko huku msimamizi mkuu wa Sera ya elimu ni waziri.

Chochote kilichosemwa baina yao hao wawili kuhusu kukatika kwa maji na kukawa na tofauti basi wa kuaminiwa zaidi ni waziri sio kwamba RC haaminiki bali waziri ndio anajua tatizo kwa udani
 
Mjinga mwenzangu ananiuliza mbona wakati Demokrasia na uhuru wa habari ulipokuwa haupo na tatizo la mabwawa kukauka halikuwepo ?

nmemwambia tatizo la ukame likiisha ndio tutaanza kukata maji kuboresha miundombinu ya maji na umeme

sasa hivi mabomba yote yamekauka sasa wakikarabati watajua vipi panapovuja ?
 
WIZARA YA MAJI YAUNGANA NA DAWASA CHANGAMOTO YA HUDUMA DAR

Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso (Mb) ametembelea eneo la matengenezo ya bomba kubwa la inch 72 katika kata ya Wazo, Jijini Dar es salaam ambalo ni sehemu ya kimkakati ya kuongeza msukumo wa Maji katika Jijini Dar es salaam ili kukabiliana na hali ya kina cha maji kupungua na kuhakikisha matengenezo hayo yanakamilika.

Akiwa eneo hilo, Aweso ametumia nafasi hiyo kutoa tamko la Serikali juu ya njia mbadala za kupambana katika kipindi hiki cha upungufu wa huduma ya Maji kwa kuruhusu wenye visima binafsi kuwahudumia Wananchi.

Akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe Godwin Gondwe na Afisa Mtendaji Mkuu-DAWASA, Cyprian Luhemeja, Mhe Aweso amesema Serikali ipo bega kwa bega na Wananchi wa Jiji la Dar es salaam na Pwani katika kipindi hiki na kuitaka Mamlaka ya Maji (DAWASA) kuhakikisha migao ya maji iliyowekwa kufuatwa bila ubabaishaji ili kutoa haki kwa kila mwananchi kuhifadhi maji ya kutosha wakati huu.

"Niwaagize DAWASA kuhakikisha ratiba ya mgao inasimamiwa na kufuatwa kikamilifu kama ilivyopangwa.
Pasitokee janja janja yoyote itakayosababisha lawama au upendeleo.

Niseme kuwa Serikali imeruhusu matumizi ya maji ya visima binafsi na vya umma ili vitumiwe na kuendelea kutoa huduma kwa Wananchi bila kikwazo chochote hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo" alisisitiza Mhe Aweso

"Wenye visima binafsi toeni huduma sasa ili wananchi wasiteseke na huduma hii.
Wizara inayo mipango ya muda mfupi ikiwemo kuanza kutumia maji ya mradi wa Maji Kigamboni ambao utawashwa Oktoba 30. Amesema mradi unatarajiea kuzalisha takriban lita milioni 70 za maji ambazo zitasambazwa Kigamboni na maeneo ya katikati ya jiji" ameongezea Mhe Aweso

Waziri Aweso ameongeza kuwa hivi karibuni utiaji saini wa kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa Maji Kidunda utafanyika mwezi Novemba mwaka huu na kushuhudiwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassani.

Mradi wa Kidunda ni suluhisho la kudumu la upatikanaji wa maji ghafi katika Mto Ruvu kwani litatumika kukusanya maji wakati wa mvua na maji hayo yatatumika nyakati za kiangazi.
IMG-20221027-WA0064(2).jpg
IMG-20221027-WA0055(2).jpg
IMG-20221027-WA0054(3).jpg
IMG-20221027-WA0056(3).jpg
IMG-20221027-WA0053(2).jpg
IMG-20221027-WA0057(3).jpg
 
Naamini ukarabati wa hilo bomba ukiisha na mgao wa majI utakwisha pia.
 
TOKA MAKTABA,
21 FEBRUARY 2014

LOWASSA - DAWASA WAPONGEZWE, MITAMBO YA RUVU NI MIZEE

MH EDWARD LOWASSA AKIWA WAZIRI WA MAJI ASHUHUDIA MKATABA WA CITY WATER NA DAWASCO
Maji toka mto Rufiji kuletwa Dar es Salaam, Pia mitambo ya maji ya, Ruvu kukarabatiwa
 
Back
Top Bottom