Aweso apanda bodaboda kukagua vyanzo vya maji, wenzake wanatumia Chopa

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso kijana wa watu asiye na mbeleko anahangaika kwa usafiri wa bodaboda ili mradi afike ajionee mwenyewe changamoto za maji zinazowakabili wananchi.

Wengine watoto wa wakubwa wanatumia Helkopta kukagua vyanzo vya maji vilivyokauka kwa ukame na kusababisha mgao wa umeme na kukagua anuani za makazi.

Mungu awe nawe Jumaa Aweso katika kutekeleza majukumu yako japo sehemu kubwa mgao wa maji unaolaumiwa wewe ni kutokana na mwenzako kukata umeme na kusababisha mitambo ya maji ishindwe kufanya kazi. Lakini Mungu yuko nawe na watanzania tuko nawe

nappic.jpg

20230104_145347.jpg
 
Aweso ni Waziri anayependa kufanya kazi kwa matokeo na anaridhika na dhamana aliyopewa na Mh Rais, ndio maana hukumuona akihangaika na vyeo ya NEC CCM kwa sababu anajiamini kiutendaji hataki kubebwa na mwavuli wa Chama.
 
Yaani nyie bila kumponda January na Nape hamuwezi? Najua January na Nape sio kwamba hamuwapendi kwa utendaji mbovu, Ila kwa kuwa wameonesha wazi kuwa "shujaa" wenu alikuwa fala tu, boya aliyejiona kafika hajui kiswahili Wala kiingereza.
 
kwani wanapomponda marehemu inafanya wao waonekane mashujaa? Nani aliitwa shujaa kwa kuponda marehemu au kubomoa makaburi?...ni mafala tu ndiyo wanaweza kuendekeza ujinga huo
 
Hakuna anayemponda mtu tumelinganisha utendaji wa Aweso na wenzake
 
PLO said:
Yaani nyie bila kumponda January na Nape hamuwezi? Najua January na Nape sio kwamba hamuwapendi kwa utendaji mbovu, Ila kwa kuwa wameonesha wazi kuwa "shujaa" wenu alikuwa fala tu, boya aliyejiona kafika hajui kiswahili Wala kiingereza.

soma alichoandika PLO. ulinganifu gani mpaka mumtaje marehemu. huo ni udhaifu
 
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso kijana wa watu asiye na mbeleko anahangaika kwa usafiri wa bodaboda ili mradi afike ajionee mwenyewe changamoto za maji zinazowakabili wananchi...
Pamoja na kuwa amefanya jambo jema,ila amevunja sheria za usalama barabarani Kwa kutovaa elementi 😀
 
Mmoja anajifanya mlalahoi wakati kashakuwa njema.
hahaha. eti anajifanya mlalahoi unaijua historia ya Aweso wewe? soma hapa

MTOTO WA MAMA NTILIE JUMAA AWESO ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA NDANI CCM PANGANI

August 3, 2015, 1:45 am
Mtoto wa mama ntilie mwenye uzao halisi kutoka wilayani Pangani mkoani Tanga, Ndugu Jumaa Aweso ameibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa ndani wa chama cha mapinduzi CCM.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo katibu wa CCM wilayani Pangani Bi Zaina Mlawa amesema kuwa, katika uchaguzi huo uliowashirikisha wagombea wapatao kumi na moja, Ndugu Aweso amekuwa wa kwanza miongoni mwa wagombea hao.

Uchaguzi huo uliokuwa na ushindani wa aina yake kutokana na kuwepo kwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Ndugu Salehe Pamba, uliwashirikisha wapiga kura wapatao 10376 wa chama cha mapinduzi.

Awali wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Bi Zania aliwataja wagombea hao kwa idadi ya kura walizopata na kusema kuwa "Ndugu Wahi Ibrahim amepata kura 87, ndugu Rosemary Luanda amepata kura 89, ndugu Elizabeth Alatanga amepataa kura 158, Halima Kimbau amepata kura 222, Ndugu Mohammed Rished amepata kura 442, Ndugu Ayubu Mswahili amepata kura 565"

Bi Zania ameongeza kwa kusema kuwa "Ndugu Omary Mwidadi amepata kura 587, ndugu Omary Chambega amepata kura 720, ndugu Salehe Pamba amepata kura 1567, ndugu Abdurahmani magati amepata 1956, na ndugu Jumaa Aweso 3983"

Ushindi huo kwa ndugu Jumaa Aweso unampa nafasi ya kuwa mgombea wa katika kuipeperusha bendera ya chama cha mapinduzi CCM wilayani Pangani endapo kamati kuu ya maamuzi itaridhia.

Mpaka sasa katika jimbo la Pangani kumepatikana wagombea wawili ambao wanaonekana kupendwa sana na wanancho ambao ni Amina Mwidau wa CUF pamoja na Jumaa Aweso wa CCM ambapo kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya siasa, endapo watakutana katika nafasi ya ubunge upinzani utakuwa wa aina yake.
 
soma alichoandika PLO. ulinganifu gani mpaka mumtaje marehemu. huo ni udhaifu
Naungana nawe wewe kumponda yule anayesema sisi tunawaponda kina nape na januari
 
Nasema kwa sasa anazo, kupanda boda ni kuzuga watu tu.
 
Back
Top Bottom