Aweso apanda bodaboda kukagua vyanzo vya maji, wenzake wanatumia Chopa

Aweso apanda bodaboda kukagua vyanzo vya maji, wenzake wanatumia Chopa

Ni rahisi kucheza na akili ya watanzania. Wanapima utendakazi wa mtu kwa kula kwa mama lishe, kupanda daladala, kula mahindi ya kuchoma barabarani, kunywa kahawa na raia. Yaani, watanzania tuna shida kweli
Mitz ndivyo tulivyo.
 
Aweso ni Waziri anayependa kufanya kazi kwa matokeo na anaridhika na dhamana aliyopewa na Mh Rais, ndio maana hukumuona akihangaika na vyeo ya NEC CCM kwa sababu anajiamini kiutendaji hataki kubebwa na mwavuli wa Chama.
Angekuwa serious tusingekuwa tunakosa maji ya mgawo Jijini kisa presha down na wanaofungua wanafanya watakavyo.

Taarifa zimejaa jukwaa la Dawasa
 
Huyu jamaa nilikuwa namuona mwanzoni kama mpenda sifa flani hivi,lakini sasa hivi namkubali sana,he is a very hard working person.Chapa kazi mkuu,nakutabiria kufika mbali sana...
 
Anafanya maigizo baada ya kuona Mama anapanga upya serikali yake ili akumbukwe. Saivi wengi wanafanyq vituko na kushinda kwa waganga ili wakumbukwe wasiachwe kwenye uwaziri

Ni ujinga tu
 
Yaani nyie bila kumponda January na Nape hamuwezi? Najua January na Nape sio kwamba hamuwapendi kwa utendaji mbovu, Ila kwa kuwa wameonesha wazi kuwa "shujaa" wenu alikuwa fala tu, boya aliyejiona kafika hajui kiswahili Wala kiingereza.
Alafu hawajui kuwa ni raisi wao ajae.
 
Duh!

Utendaji thabiti unapimwa kwa kupanda boda boda?
 
Aweso ni Waziri anayependa kufanya kazi kwa matokeo na anaridhika na dhamana aliyopewa na Mh Rais, ndio maana hukumuona akihangaika na vyeo ya NEC CCM kwa sababu anajiamini kiutendaji hataki kubebwa na mwavuli wa Chama.
Ni kijana mchapakazi ila chama alichomo ndiyo tatizo.
 
Back
Top Bottom