Aweso apanda bodaboda kukagua vyanzo vya maji, wenzake wanatumia Chopa

Nasema kwa sasa anazo, kupanda boda ni kuzuga watu tu.
Kuwa nazo lazima awe nazo si anafanya kazi halali ya Ubunge, Uwaziri na analipwa mshahara na stahili zake halali kwa mujibu wa sheria
 
Ila kuwa chawa si kazi ndogo
 
Daah. kumbe mtoto wa mama ntilie ndio maana ana adabu anajua alikotoka anaheshimu watu wote
 
naona anawajaza, wabongo bwana.

Kwangu mimi huyu si mtendaji mzuri....maana ya serikali kuwepo kila mahala hapa haipo, katibu, naibu katibu, watu wa mkoani, watu wa wilayani wanafanya nini?....Kazi ya Waziri ni kuwaza mambo makubwamakubwa na kuleta solution kwenye kila sintofahamu..
 
Aweso yuko vizuri mtoto wa mama ntilie hawezi kuleta ujuaji
 
Kupanda bodaboda sio kigezo cha kuwa mtatua matatizo tuliyo nayo.
Lazima tuachane na hizi kasumba za kuonekana tuna jali kumbe tunataka kuuza sura.
Matatizo mengi yanashindwa kutatulika kwa sababu watu Fulani wanatumia ujinga wetu kutuhadaa .
Mtatua matatizo hatumii makamera hili tuone matukio yake
 
Huyo mwenye Shati LA kijani mbona anawasiwasi kama mjusi ...
 
Huyu akija na sababu za ukosefu wa maji zinakuwa na reliable .Hata akisema mgao wa umeme sababu ni ukame watu hawatabisha.
 
wale pinga pinga fc naona wameanza kumwagia sifa,
 
Makamba na Nepi hamnaga kitu wanabebwa bebwa tu na majina ya baba zao
 
Yaani nyie bila kumponda January na Nape hamuwezi? Najua January na Nape sio kwamba hamuwapendi kwa utendaji mbovu, Ila kwa kuwa wameonesha wazi kuwa "shujaa" wenu alikuwa fala tu, boya aliyejiona kafika hajui kiswahili Wala kiingereza.
Msipopenda kuusikia ukweli mtapotea kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…