Wizara ya Maji
Govt Institution
- Oct 2, 2024
- 34
- 20
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb), amesema hatokuwa kikwazo kwa wananchi kupata huduma ya maji safi na salama nchini.
Akikagua Mradi wa maji wa miji 28 katika eneo la tekeo la maji (Intake) mtaa wa Senga Geita amesema atahakikisha kazi inafanyika kwa saa 24 ili kufikisha huduma ya maji kwa wananchi.
Mradi huo unatekelezwa kwa gharama Dola za Marekani Milioni 53.4 sawa na Shilingi za Tanzania Biilioni 124.
"Ninatambua Miundombinu ya sasa inauwezo wa kuzalisha Maji katika Manispaa ya Geita kwa wastani wa lita Milioni 9 kwa siku wakati mahitaji ni lita Milioni 22. Hivyo kukamilika kwa mradi huu kutaongeza uzalishaji lita Milioni 45 kwa siku sawa na asilimia 100 ya mahitaji" Aweso amesema.
Kazi zilizo kamilika hadi muda huu ni ufungaji wa mitambo ikiwemo ufungaji wa Pampu 11 pamoja na Transforma nne.
Kwa sasa mradi utekelezaji wake umefika asilimia 82 ambapo hadi kufika Desemba 2026 maji yataanza kusukumwa katika matenki yote Matano yaliyojengwa ( Mjini 2 na Vijijini 3) na wananchi kuanza kunufaika na huduma ya maji. Mradi u2tahudumia wananchi zaidi ya 716,948 kwa mji wa Geita.