DOKEZO Aweso nakujulisha kuwa rushwa imetamalaki sana DAWASA pindi wananchi tunapohitaji kuunganishiwa huduma ya maji

DOKEZO Aweso nakujulisha kuwa rushwa imetamalaki sana DAWASA pindi wananchi tunapohitaji kuunganishiwa huduma ya maji

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

gimmy's

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2011
Posts
3,312
Reaction score
3,345
Salaam,

Kwanza nianze kwa kumpongeza Aweso kwa namna anavyopambana kuhakikisha maji yanafika kwa wananchi ili kuyafikia malengo ambayo chama na serikali wamejiwekea.

Licha ya haya mapambano ambayo wazari anapambana kuhakikisha maji yanasambaa kwa wananchi, yanayoendelea huku kwa watendaji wako yanatuvunja moyo,hawa jamaa wanatengeneza mazingira ya Rushwa na kwa kiwango kikubwa wanafanikiwa.

Hivi ndivyo namna watendaji wako wanatuumiza;

Moja ya vigezo vinavyohitajika ili uweze kuunganishiwa maji unatakiwa uwe ndani ya 50m kutoka kwenye bomba la usambazaji la dawasa ambalo kwa kawaida ni bomba lenye kipenyo cha 2inches.

Kwa msingi huo utaona kwamba DAWASA wanalazimika kuhakikisha kwamba wanayasogeza maji kwenye makazi ili wananchi waliowengi wawe ndani ya 50m, DAWASA badala ya kutimiza hili jukumu lao lakuyasogeza maji karibu, kwao wananchi waliopo nje ya 50m wanawageuza fursa.

Wanachokifanya DAWASA mteja aliyekosa vigezo vyakuunganishiwa maji kwa kuwa nje ya umbali wa 50m rushwa itahusika ndipo upate maji.

Mfano mtu yupo umbali wa 90m kutoka kwenye bomba lao la usambazaji Wanachofanya kama mtakubaliana kwenye document wanajaza 50m, mwananchi baada yakukubaliana kiasi fulani cha rushwa ofisi itatambua nakutoa bomba lenye urefu wa 50m, bomba lililopelea la 40m mwanachi atalazimika kwenda dukani+kulipa wachimba mtaro huo wenye urefu wa 40m. Ukikataa kutoa Rushwa utaambiwa mpaka huduma itakaposogea karibu.

Wapo watu pia ambao wapo umbali mrefu zaidi inawalazimu kuhonga mamilioni na kinachofuata maji yanasogea huku material yote ni mali ya DAWASA.Kuna watu wanahonga mpaka 3,000,000/= ili maji yasogee mtaani.Utakuta wanyonge wananufaika kwasababu ya tajiri mmoja, hapa utaona kama si huyu tajiri wananchi wangeendelea kusota.

Ushauri wangu kwako Aweso jaribu kufuatilia kwa makini huku mtaani zipo nyumba nyingi zipo nje ya 50m lakini zinamaji huku makapuku wakiwa watazamaji kwakuwa hawana pesa za hongo.

Nashauri ongezeni urefu unaohitajika kumuunganishia mwananchi walau ufike 200m ili kupunguza hii rushwa kwani kimsingi watu wa hali za chini wanashindwa kuunganishiwa maji kwakukosa fedha za hongo.

Maji ni uhai.

Asante.
 
Back
Top Bottom