Ayatollah wa Iran apinga Hajj, kuwa ni suala la Kisiasa

MlimaSayuni

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2013
Posts
7,285
Reaction score
13,703
Kama Habari inavosema kutoka ukurasa rasmi wa Ayatollah Kiongozi mkuu wa Iran, amehoji sababu za ulazima na msingi Watu waende Hijja.

Naona Watu wanahisi Ayatollah hakusema hayo.
Mjadala uliendelea na akakazia Hijja ni tukio la Siasa, tumieni akili





Mwisho kama Dini zingine Dini zote hukua na kubadilika na kuja mpya Iran inaubadili Uislam
 
Shauri yako wako njiani wanakuja
 
Ayatollah zimeanza kumfyatuka Haji ni katika Arkani Al Islam tano.

Hapo ndipo waislam wanavyo anza kuleta chuki, huyu Ayatollah yeye anaona siasa lakini Qur'an inasema Haji mwenye uwezo lazima aende mara moja ya kwake hakuna Haji mara mbili, hao wanao enda ya pili ni kuwahijia wengine sio wao na Haji huwa ni mara moja kwa mwaka katika mwezi wa Dhuh Al haji

Ayatollah Khomen naona zinataka kumruka 😄 🤣
 
Mleta mada acha kushadania mambo ambayo huyajui! kwanza ujuwe taifa la iran wengi ni mashia, na itikadi zao baadhi zinatofautiani na waislam walio wengi ktk dunia hii ambao ni sunni.
 
Nakubaliana na wewe 100%; Ayatollah kachoka. Hivi huyu naye ni lazima afie ofisini? Hawezi kujiuzulu pale zinapoenda harijojo? Kama yaliyoandikwa kayaandika mwenyewe, alazimiahwe kujiuzulu.
 
Elimu yako ndogo sana , umeshindwa kuelewa intended meaning kwenye huo ujumbe na kurelate na yanayoendelea sasa.

Kweli kunyimwa akili ni umasikini mbaya na zaidi umeioamba habari kiudaku na wengine wasio elewa wanafuata mkumbo . Anyway hata akisema sio ajabu hivyo hao ni Mashia Wana kufuru kubwa sana na ni maadui wa Uislamu.
 
Nimewahi kukutana na jamii ya waislam huko Tanga wanajiita twariqa qadiriya, wao misikiti yao haina upande wa jinsia ya kike ni hall tu

Kwao mwanamke haingii kabisa msikitini wanadai mwanamke hairuhusiwi kuswalia masjid, na hata kufunga na kufungua mwezi ramadhan kuna tofauti na hawa wengine
Na huwa hawafuati maagizo ya mufti wanadai BAKWATA ni taasisi ya serikali, niliiswali nao mda fulani na nikajiridhisha wao ni waIran na misaada yao mingi inatoka Iran

Nadhani kuna namna Iran huionea wivu Saudia kupokea mahujaji kwa kuwa inapata fedha nyingi sana za kigeni "inawezekana ni kweli Saudia walibuni mbinu"
 
Usiwe mjinga kutoa hitimisho pasi na kujua nini unazungumzia.
Iran asilimia kubwa ni Shiite/shia.
Na asilimia 90 ushia ni sawa na ukafiri nyuma ya pazia na hilo liko wazi.
Usihusishe masuala ya kisiasa za kimataifa ya Iran na dini Wacha UPUMBAVU HUO.

Nguzo za uislam ni Tano.
1.Shahada.
2.Swalah
3.Zakah.
4.Swaum
5.Hijjah

Hilo lipo dunia nzima akipinga Iran ama Ayatollah Khomeini haimaanishi mawazo yake yafuatwe.
 

je wewe unaujua uislamu kuliko Ayatollah?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…