Ayedhaniwa kuwa ni toto wa Rais Magufuli achezea Fedha Snapchat

Ayedhaniwa kuwa ni toto wa Rais Magufuli achezea Fedha Snapchat

Mbona sijaona sura ya huyo anayechezea fedha au ndio maji taka haya
 
Hahah watu mna hasira, kwani hata video ingekuwa kweli hizo hela ni bei gani? Hata 5M hazifiki, kwaiyo mnadhani watoto wa Raisi hawaendi shopping? Hawali bata? siasa za bongo hovyoooo
 
Mtoto wa Magu huyo huko Snapchat...... babake yuko huku anatupigia kelele eti Watu walikuwa na pesa za kuchezea sasa zimeondoka, Mbona mwanae bado ambazo pesa za kuchezea mpaka anazimwaga kwenye sakafu???

Jamani huyu ni mtoto wa kiume wa Magu anaeishi Ikulu kabisa anaitwa Clifford Magufuli. Snapchat anatumia Clifford JPM Ila kablock mtu huwezi hata kumsearch. Yani kawa add only his close friends.

Hata hii video imebidi irekodiwe kwa simu ingine ili asijue nani karekodi au kachukua screenshot....ila bahati nzuri one of us close friends is also my informer ndo kanipa video sasa Hivi. Yani Hapa tunavyooongea hizi video bado zippo snapchat

Leo Clifford atachezea kichapo cha babake, nahisi atakabidhiwa kwa Uncle Bashite Maliyamungu akateswe kidogo kwa kosa la kuwaonyesha Tanzania the real luxury life style ya Magufuli and his family na sio ile ya kutunganyia watanzania na kubana matumizi!

Eti pesa imepotea sababu mlizoea kuchezea. Mbona mwanae bado anachezea pesa kama kawa??



Huyo Mtoto wa Rais Magufuli asipotumia Pesa za Baba yake mnataka atumie za Baba zenu? Katika hili wala tusidanganyane hapa na tusiwe wanafiki hata Sisi wengine Wazazi wetu wangekuwa na ' Fursa ' kama aliyonayo Magufuli na Sisi pia tungekuwa na huyo Clifford ila tatizo ' umasikini ' umetukomaa hadi sasa umetubadili na kutufanya tuwe na chuki na majungu.

Hivi kuna Mtoto wa Rais katika nchi hii ambaye alitumia Pesa vibaya na hovyo hata kwa mambo mengine ambayo ' Kimaadili ' hayaelezeki humu kama Ridhiwani Kikwete Mtoto wa Rais wa awamu ya Nne? Mbona Yeye mlikuwa hamumsemi na wala hamkumbushii ' ufujaji ' wake aliokuwa akiufanya na ambao unajulikana na kila Mtanzania wa Kileo na Mjanja?

Hasira na Chuki Binafsi za Mange Kimambi kwa Rais Magufuli kamwe zisimfanye ' akajisahaulisha ' na matendo ya ' hovyo hovyo ' ya Awamu na Nne na hasa kwa Ridhiwani Kikwete. Tunajua kwamba Mange Kimambi hawezi na kamwe hatoweza kumgusa Ridhiwani Kikwete kwakuwa Marehemu Baba yake alikuwa ni Rafiki wa karibu na ' Undugu ' na Familia ya Rais Mstaafu Kikwete na anatumia ' udhaifu ' wa Awamu ya Tano hii kuficha yale ' mabaya ' yote ya Awamu ya Nne ambayo siyo ' Siri ' Yeye alikuwa na maslahi nayo makubwa sana.

Namuheshimu mno na sana Mange Kimambi ila kuna sehemu zingine huwa ' anapotosha ' kuliko ' uhalisia ' huku pia ' akidanganya ' na bahati mbaya ameweza kuteka Kundi Kubwa la Watu ambao hawawezi ' Kuchuja ' mambo kwa marefu na mapana yake na wanamuamini 100%.

Hakuna Awamu za Uongozi nchini Tanzania ambazo hazijawahi kuwa na ' mapungufu ' yake ama ya Kiutendaji na hata maisha binafsi ya hao ' Viongozi ' kuanzia ya Hayati Baba wa Taifa Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa, na Mzee Kikwete na bahati nzuri kwa Sisi tuliokula ' chumvi ' kidogo tunayajua ila kwa ' maadili ' hatuweki humu lakini cha kushangaza Mange Kimambi Yeye ' attention ' yake 100% ni kwa Rais tu wa Awamu ya Tano Dkt. Magufuli.

Mange Kimambi amekuwa kila uchao ' akijinasibu ' kuwa Yeye ni ' Msomi ' tena wa Masters Degree Elimu ambayo kiukweli hata Sisi wengine mfano Mimi GENTAMYCINE sina na wala sitaifikia na nitabaki tu hii hii yangu ya Darasa la Saba hivyo nimwombe tu ajitahidi kufanya ' logical analysis ' juu ya ' issues ' vinginevyo anavyofanya sasa anaanza kututia shaka kama kweli ana hiyo Elimu kubwa tena ya huko huko Marekani alipo.

Haya niliyoyasema hapa hayabadili ' Heshima ' yangu kubwa niliyonayo Kwake kwani siyo ' Siri ' kuna mahala pengine huyu Dada ( Mange Kimambi ) ameweza kusaidia mno kuleta mabadiliko na nimekuwa nikimsifia sana tu humu na ni Mwanamke ambaye anauwezo wa ' Kuthubutu ' na ' Mpambanaji ' ila ana ' mapungufu ' machache lakini ya Kimsingi ambayo anatakiwa kuyafanyia Kazi.

Yangu ni hayo tu!

GENTAMYCINE ni kama Bahari ambayo huwa haikai na ' uchafu ' daima.
 
Back
Top Bottom