Ayub Rioba: JamiiForums ni chombo cha habari na si jukwaa la mtandao

Huyu jamaa ndio anahitaji Elimu na sio kwamba yeye ndio atoe Elimu.... Huenda Jamii Forums kama Taasisi kwa ujumla wake ikawa chombo cha habari ila hili lidude ninalotype hapa sasa hivi na kutoa maandishi yangu ni Mtandao wa Kijamii...

Au kwa maana yake yeye ni kwamba duniani hakuna kitu kama Jukwaa / Mtandao / Social Media
 
Nakubaliana na wewe JF wanamapungufu.

Hatahivyo, JF ni user-generated content site fahamu hilo.

Huko kwa Millard Ayo ninaweza kusajili akaunti yangu na kuanzisha mada na kujadili na wanachama wengine?
Kuna utofaut gani na Millard ikiwa mada zinazopendwa ndio zinabakishwa? Utofaut wa hapa na Millard ayo ni kuwa waaandish wa Millard ayo wanalipwa wew hulipwi, ila wote mna kazi ya kuhakikisha idea za mwenye website zinafika,

Huwez post mada ambayo millard hapend same huku, huwez post mada jf haipend
 
Hii ndio platform wenye akili tunatumia.
 
Anataka tuanze kulipia kodi?
 
Nimekuuliza ninaweza sajili akaunti kwa Milard Ayo na kuanzisha mada kwa lengo la kujadili na member wengine kama inavyofanyika hapa JF?

Kama huwezi kuona kitu kilicho dhahiri nikusaidiaje?

JF ni jamvi.

Hapa watu wanajisajili, wanaweka mabandiko yao, wanajadiliana na wanachama wengine.

Kwasababu unaweza "ku-comment" kwenye social media pages za Milard Ayo hiyo haifanyi iwe sawa na JF.

Kuhusu kulipwa au kutolipwa hiyo ni jinsi unavyo tumia JF

JF ni jamvi hapa ukitaka unaweza tengeneza pesa vizuri kabisa.

Amka toka usingizini chalii.
 
Natamani Malaika waje wafunge Mitandao!

In Jiwe voices!
😁😁😁😁
 
Kihiyo,
Hajui tofauti ya chombo cha habari na jukwaa
 
"Waandishi wa Milard Ayo" huwezi kuwalinganisha hata na Moderators wa JF, wewe umeenda mbali zaidi kuwalinganisha na members!

Umesahau pia kuwa hapa kuna fursa ya kuwa anonymous "kutojulikana" tofauti na kwa Ayo.
 
"Waandishi wa Milard Ayo" huwezi kuwalinganisha hata na Moderators wa JF, wewe umeenda mbali zaidi kuwalinganisha na members!

Umesahau pia kuwa hapa kuna fursa ya kuwa anonymous "kutojulikana" tofauti na kwa Ayo.
Jamiiforums ina creativity ndogo sanaaaaa, utofaut wake na Millard Ayo ni mdogo sana
 
Inaonekana watu wengi wanashabikia huu mjadala bila kuelewa maana halisi na tofauti, hususan kisheria.
Kwa akili za kiccm hapo wanawaza kuwabambikia Kodi tu.

Huyu Dr sijui sasa hivi ni Profesa huyu Ayoub Ryoba zamani alikuwa na akili Sana, lakini tangu amejiunga na kundi la wajinga na yeye amekuwa mjinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…