Azam anapita njia ngumu CAFCL, atatoka hatua ya awali

Azam anapita njia ngumu CAFCL, atatoka hatua ya awali

Wanapata sare Chamazi, wanaenda kutolewa Rwanda
Unaambiwa APR wametua Arusha hawajatumia Airport ya Dar, sijui intelejensia Yao imegundua Nini,
APR wapo serious nadhani mtaani hili neno baada ya game
Hahahahaha, dar wamekuja na usafiri gani sasa au Arusha kisha wakapanda ndege nyingine?
 
Nilitamani Utopolo ipitie njia hii
Ili uondokane na hiyo njia lazima umpasue aliye bora zaidi yako na kusonga mbele. Yanga hiyo njia wameshaivuka wapo kwenye kuteremka tu sasa. Azam wanatakiwa hivyo vigingi avivuke kisha aingie makundi misimu miwili mfululizo atakuwa na yeye anateremka tu wenzie Simba na Yanga.
 
Napenda azamu afungwe.maana wanatupandishia Kila siku vifurushi vyao.
Hapo wanakosea sana unalipia vifurushi bei utafikiri siku wanaonyesha mpira wanagawa na chakula. Ni vema wa husika waka ingilia kati hili kuwe na ushindani wa kuonyesha ligi yetu isiwe wao pekee. Vinginevyo manunguniko ya wateja siyo mazuri hadi mnapangiwa timu vigogo hatua ya awali si bure.
 
Azam wana team nzuri, wamemsajili vizuri sana, nilidhani watafuzu hizi hatua ila kila nikiangalia naona anaangukia pua

Azam hatua ya awali wamepangwa na mbambe APR ya Rwanda, hii ni team ngumu haswa, wana uchumi mzuri, wana wachezaji wakubwa hasa.

Kuna yule Mghana na dogo Fulani beki ni wachezaji wazuri mno,

Azam wanaanzia nyumba ambapo hawana nguvu ya mashabiki hapo ARR watakuwa comfortable kupiga kandanda, na baadae wanatenda kumalizana Rwanda hapa Azam wanatoboa vipI?

Wakitoka hapo wanatenda kukutana na Pyramid matajiri wa Misri team ya Mayele, hapo ndo ya makundi wataisikia kwenye redio

Azam nawapa pole mapema
Nilikuwa naliongelea Leo Hilo
 
Back
Top Bottom