Azam, Azam Udini utawaharibia

Azam, Azam Udini utawaharibia

Akisoma habari kwa ufupi saa nane mchana leo, mtangazaji alijifanya kushindwa kutamka maneno "Parokia ya mwenye heri Maria Theresa..." Akaishia kusema parokia ya mwenye heri! Kama mnaona ukakasi kutamka hayo maneno si bora hiyo habari mungeipotezea kuliko kupotosha.
Al jazeera ya tanzania 🤣🤣🤣
 
Huwa nafuatilia kipindi Cha sport Cha siku ya jumapili au jumamosi asubuhi kama Kuna timu ya Tanzania inacheza mechi ya kirafiki ,Kuna mtangazaji mmoja huwaalika wachezaji wa zamani baada ya uchambuzi wanamchagua mmoja wao aombe Dua ya kiislamu. Hata huwa hawajishtukii huyu jamaa anaona ni halali na haki yake kufanya maombi ya dini Moja kwa Watanzania wenye Imani tofauti
 
Hicho chombo mjue kinatumia masafa ya umma, umma huu watu wake wana dini zao japo nchi hii haingozwi kwa misingi ya kidini. Bila shaka azam media sio chombo cha habari cha kidini na hakipaswi kuonekana kina element za dini fulani kwa kuwa mmiliki wake ni muumini wa dini fulani. Wanapaswa kwenda kufanya coverage ya matukio ya kitaifa ya dini ambayo mmiliki wake haabudu huko. Kama kuna habari inataja eneo fulani, kanisa fulani itaje tu kama ilivyo bila kuona ukakasi ki imani/dini. Kama kanisa linaitwa moyo mtakatifu wa Yesu kuna ibada ya kitaifa imefanyika huko au kiongozi wa kitaifa kasali pale na kufanya iwe habari basi isomeke hivyohivyo. Labda hicho chombo kingekuwa cha kidini hapo tungeona ni sawa kuona ukakasi kutaja maneno ambayo hawapaswi kuyatamka kwa mujibu wa imani/dini yao. Siku hizi kuna redio za kidini ambazo hazina kizuizi cha kuandika na kusoma habari za dini nyingine maadamu zinahusu wananchi wote kwa ujumla
 
Mtoa mada nadhani kidogo dishi limeyumba, yaani uumie kisa mwandishi amekosea kutaja jina la kanisa? Like seriously??? Kwenye maisha haya yenye shida na Karaha lukuki bado mtu ujiongezee stress za kutajwa jina la kanisa? Alafu then inakusaidia nini kwenye maisha yako? Ifike kipindi tuwe serious kwenye mambo ya msingi yanayotuletea tija.
 
Hizo dini kwani zina faida gani?

Mimi mwenyewe nikisalimiwa "Assalam alekum" huitika salama kwa sababu sina mazoea nayo.

Sasa ukiona mtu kashindwa kutaja jina la dini isiyo yake basi usishangae.
 
Labda dish la mmeo ndilo limeyumba, mambo ya msingi kwako sio ya msingi kwangu
 
Hizo dini kwani zina faida gani?

Mimi mwenyewe nikisalimiwa "Assalam alekum" huitika salama kwa sababu sina mazoea nayo.

Sasa ukiona mtu kashindwa kutaja jina la dini isiyo yake basi usishangae.
Swala sio kutaja dini bali kushindwa kusoma kiswahili makusudi
 
Kwa hawa waswahili wa Tandale hilo walijui
Mkuu waislamu wote wanamuheshimu Maria
Na kama nilivyokuambia ana surah kwenye quran...
kama unavyosema Mathayo...kwenye biblia..

kama Mmoja ya wanawake Waliobarikiwa kuliko wanawake wote...
Ambao miongoni mwao ni ASIA (aliyemujifadhi Musa kipindi cha farao),MARIA (mama yake yesu),Khadija (Mke wa mtume) etc
 
Unaijua tasnia ya habari hata kwa bahati mbaya,

Yani news anchor ashindwe kutamka maneno rahisi namna hiyo ?...

Hata hivyo binafsi yangu siwezi kuchukulia vitu kama hivyo serious ila kama mtangazaji alishindwa kutamka maneno rahisi hivyo bhasi Azam kuna walakini kwenye hiring process yao
Rahisi kwa nani babu!!?..kadinali pengo anaweza kusema inna Lillah wa inna ilaihiyir raajiun!?
 
Un
Hizo dini kwani zina faida gani?

Mimi mwenyewe nikisalimiwa "Assalam alekum" huitika salama kwa sababu sina mazoea nayo.

Sasa ukiona mtu kashindwa kutaja jina la dini isiyo yake basi usishangae.
Unawezaje kuandika usichoweza kukisoma?
 
Akisoma habari kwa ufupi saa nane mchana leo, mtangazaji alijifanya kushindwa kutamka maneno "Parokia ya mwenye heri Maria Theresa..." Akaishia kusema parokia ya mwenye heri! Kama mnaona ukakasi kutamka hayo maneno si bora hiyo habari mungeipotezea kuliko kupotosha.
Si unagalie Agape Mkuu wa ile TV ya mzee wa upako.
 
Back
Top Bottom