Azam FC 1-2 Yanga SC|| Uwanja wa Chamazi|| NBC Premier League

Mwananchi hashikiki huu Msimu[emoji91]
.
Mayele anawika Chamazi Complex tena Mbele ya Prince Dube akiwa haonekani kabisa. Huyu Mkongo misimu Miwili ligi ya Kongo aliibuka na kiatu na mwingine akiwa nafasi ila sioni kama katika hii ligi kwa huu Moto kuna Mtu anaweza mzuia kubeba Ng'ombe zaidi ya wawili alionao kabla ya kupewa kiatu cha ufungaji bora. MAN ON FIRE [emoji91] [emoji1430][emoji460]
.
Hii sio Bahati mbaya heshima kubwa kwa Usajili wa Yanga hongera kwa ufanisi wa Benchi la ufundi la Yanga . Sio rahisi kumfunga Azam Fc aliye katika ubora huu ndani ya kiwanja tena akiwa full huku wewe ukiwa huna key players wa 3 .
.
Sureboy mtoto wa mzee Aboubakar Sureboy Senior katika dimba alilozoea dhidi ya mpinzani aliyemlea miaka 13 na akawaonyesha ukubwa wake dimbani kwa ladha eneo la kiungo.
.
Kadi yake ya 3 ya Mchezo na kweli atakksa mchezo mmoja wa Azam Sports cup Federation hivyo mechi ya April 30 dhidi ya Mtani atakuwepo huku ikiwa Yanga Sc inatimiza Mwaka na Siku 5 bila kupoteza mchezo wowote wa ligi Kuu.
.
WAITE TU PRESS [emoji16]
.
Mwisho wa Siku Yanga Sc walikubali kukimbia zaidi kuliko mpinzani kiwanjani wakaamua kuonyesha Spirit na Character ya timu kubwa na inayotaka Ubingwa.
.
Deserving Win na alama 51 kibindoni akiwa kileleni kwa Alama 14 zaidi ya mtani wake.
.
KWELI MPIRA UNADUNDA ILA HUU MLIMA NI MREFU MNO WAJOMBA TUWE WAKWELI.
 
Nafasi ya kwanza ana point 51 halafu nafasi ya tatu ana point 28!!!? Hii league haina usawa kabisa bora ifutwe tuu[emoji23]
 
Prince Dube majeraha yamemuondoa kabisa katika ramani ya mpira wa miguu. Bila shaka anahitaji muda zaidi kurudi kwenye kiwango chake cha awali.

Kiufupi hana tofauti na Balama Mapinduzi. Vipaji wanavyo, ila ndiyo hivyo tena. Majeraha yamewarudisha nyuma.
 
Hivi tunamtazama mayele kwenye kisimbuzi kimoja na kibuda denis kweli?

tff waliangalie hili sio siri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…