Azam FC ni mtoto wa tajiri anayemtesa mzazi wake

Azam FC ni mtoto wa tajiri anayemtesa mzazi wake

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
1,667
Reaction score
2,595
FIKA Chamazi ukajionee uwekezaji wa Azam FC. Eneo la zaidi ya eka 25 lililosheheni miundombinu ya kumfanya Cristiano Ronaldo au Lionel Messi awe mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kushinda Ballon D’Or.

Hivi sasa wanabadilisha taa zao za uwanjani na kuweka za kisasa za LED zitakazofanya mechi za usiku za dimbani hapo zionekane kwa ubora wa kimataifa kama ilivyo Wembley, England au Allianz Arena, Ujerumani.

Wanatumia teknolojia ya GPS kujua maendeleo ya utimamu wa mwili wa wachezaji wao ili kulinda ufanisi uwanjani, kama ambavyo PSG wanatumia kufuatilia utimamu wa mwili wa Kylian Mbappe au Neymar huko Ufaransa.

Katika hali ya kawaida ungetarajia uwekezaji huo ungeambatana na wachezaji wa daraja la juu watakaosaidia kutafsiri miundombinu hiyo kuwa matokeo ya maana uwanjani.

Lakini bahati mbaya sana kwa klabu hiyo, licha ya mambo yote hayo wachezaji wake ni wa daraja la kati ambao hawana uwezo wa kufanya zaidi ya kinachoonekana uwanjani.

Azam FC wachezaji wadogo walionunuliwa kwa bei rahisi na wanalipwa kidogo sana.

ADVERTISEMENT

azam bus pic

Sitaki kusema kwamba kununua mchezaji wa bei ghali na kumlipa mshahara mkubwa ndiyo suluhisho, lakini ili klabu iwe kubwa na kulingana na uwekezaji wa miundombinu inayofanyika Chamazi, ni lazima mabosi wa Azam watoe pesa kununua wachezaji.

Mudathir Yahya, Bryson Rafael, Yakubu Mohamed na Benedict Haule ni wachezaji wa kiwango cha kawaida sana ambao wameichelewesha kwa muda mrefu.

Aggrey Morris na Salum Abubakari ‘Sure Boy’ ni wachezaji ambao wamekaa muda mrefu na hiyo timu na sasa hawana cha zaidi wanachoweza kukitoa kuisaidia.

David Kissu, Ally Niyonzima na Mpiana Monzinzi ni usajili uliolenga kuisaidia timu lakini bila shaka wameshindwa kufikia matarajio.

Hamahama Khlefin Hamdoun, Emmanuel Charles na Awesu Awesu ni wachezaji wenye umri mdogo ambao wanaweza kuwa msaada baadaye, lakini kwa sasa wanatakiwa kuondoka kupisha watu watakaofanya kazi.

Obrey Chirwa, Nicolas Wadada na Danny Amoah ni wageni ambao viwango vyao havipishani sana na wazawa, hivyo hawahitajiki tena.

Hili ni kundi la wachezaji 16 ambao hawastahili kuendelea kubaki na klabu hiyo.

Badala ya kuhangaika kuwekeza kwenye miundombinu, matajiri wa Azam FC wanatakiwa wawekeze hasa kwenye kikosi chao ili washinde mataji.

Matajiri wa Azam FC wanatakiwa waelewe kwamba fahari ya klabu yoyote duniani siyo miundombinu bali ni mataji.

Na huwezi kushinda mataji kwa kuwategemea wachezaji kama ilionao.

Bryson Rafael hata kama atakuwa na vifaa vya mazoezi anavyofanyia Bruno Fernandez hawezi kupiga pasi kama zake.

Chirwa hata ale chakula anachokula Lewandowski, hawezi kufunga mabao kama yeye.

Unapokuwa na timu ambayo haiwezi kushinda mechi mbili mfululizo kwa miezi zaidi ya sita, hapo ujue ni wachezaji ulionao.

Azam FC inatakiwa ijitambue kwamba iko daraja la tofauti na klabu zingine zote, ukiacha Yanga na Simba.

Katika klabu 18 zilizopo kwenye Ligi Kuu, klabu 15 zilizobaki zinaiweka Azam FC kwenye daraja moja na Simba na Yanga - kwa hiyo hata wanapojiandaa dhidi yake wanatumia nguvu za kuifunga Simba au Yanga.

Hii huzifanya mechi zao kuwa ngumu sana kiasi kwamba mtu unaweza kudhani Simba na Yanga wanatia mikono kwenye mechi zako. Ili kuhimili mambo haya, ni lazima wawe na kina Prince Dube zaidi ya watano kwenye timu katika nafasi stahiki. Ukiangakia kikosi cha Simba, ni wachezaji wawili au watatu tu wa Azam FC wanaoweza kucheza akiwemo Dube.

Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC iache kuichukulia poa timu. Iwekeze kwa kununua wachezaji wanaolingana na jina la Azam FC ili timu iishi kitajiri kama klabu inavyoonekana ya kitajiri.



©MwanaSpoti
 
Wangetafuta CEO ambaye sio mtanzania ule uwekezaji wao ungezaa matunda...wabongo wengi wetu ni wababaishaji na tuna uswahili mwingi.mbongo hashindwi kuiendesha azam kama mwadui fc
 
Organization yoyote ile ni watu.
Mie niliwaona azam wapuuzi pale walipowaacha aishi kapombe bocco erasto kuondoka hapo chamazi.

U have the best players alafu unaacha wanaondoka unatarajia nini? Kisa oh mishahara ilingane ya wachezaji....uliona wapi upuuzi kama huo kwenye hii industry? Unazila alafu miaka miwili mitatu mbele unaanza tena kutaka ubingwa wakati ulishauza best players wako.
 
Organization yoyote ile ni watu.
Mie niliwaona azam wapuuzi pale walipowaacha aishi kapombe bocco erasto kuondoka hapo chamazi.

U have the best players alafu unaacha wanaondoka unatarajia nini? Kisa oh mishahara ilingane ya wachezaji....uliona wapi upuuzi kama huo kwenye hii industry? Unazila alafu miaka miwili mitatu mbele unaanza tena kutaka ubingwa wakati ulishauza best players wako.
Hivi hao walivyoondoka azam ilipata sh ngapi kama pesa ya kuwauza? Au ni free mikataba yao ilikuwa imeisha?
 
Tajiri ni mfanyabiashara sio shabiki wa mpira.. anaweka hela sehemu inayoingiza hela ili apate faida..

Aliweka hela nyingi kwenye timu yake .. kaona anapata hasara maana timu ili ikulipe ni lazima iwe na mashabiki wengii... ndio maana mo dewji aliachana na singida utd na kukomaa kuwekeza simba..

Hakuna timu africa ya weusi yenye tajiri anaeweka pesa nyingi bila huyo tajiri kupata faida.. hata mazembe wabahili sana kununua mtu hela nyingii.. ila waambie wao wakuuzie uone wanavyokuuzia fasta fasta ukifika bei..

Bakhressa sio mjinga... kama angekuwa mjinga asingekuwa tajiri...

Simba na yanga ndio timu pekee za kuleta faida hapa Tanzania kila msimu.. sababu zina mtaji wa mashabiki... hutumii nguvu kurudisha hela yako ukiwekeza simba na yanga..
 
Duuuh! Azam wajitafakari aisee
Tena sana tuu....wewe 2017 azam anamfunga kcca mara mbili kwenye kagame cup. Mwenzake two years later anacheza group stage ya caf confederation cup misimu miwili mfululizo wakati azam amebakia kiwa mpenzi mtazamaji.
 
Azam ni Simba
Hapana, sema simba ananufaika na uwepo wa azam huku azam akiugulia maumivu, nikikumbuka azam walivyowakatalia al ahly kukodi miundombinu yake wakati wakijiandaa kucheza na simba pale ndio nikajua kuna uzalendo wa kifala sana
 
Hapana, sema simba ananufaika na uwepo wa azam huku azam akiugulia maumivu, nikikumbuka azam walivyowakatalia al ahly kukodi miundombinu yake wakati wakijiandaa kucheza na simba pale ndio nikajua kuna uzalendo wa kifala sana
Aisee
 
Hapana, sema simba ananufaika na uwepo wa azam huku azam akiugulia maumivu, nikikumbuka azam walivyowakatalia al ahly kukodi miundombinu yake wakati wakijiandaa kucheza na simba pale ndio nikajua kuna uzalendo wa kifala sana
Mwenye Azam alishakuwa MwanaSimba
 
Back
Top Bottom