JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mara baada ya kutambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa #AzamFC, Feisal Salum (Fei Toto) amesema fedha ambazo alichangiwa wakati wa sakata lake la kimkataba dhidi ya #Yanga, atazipeleka Msikitini, Kanisani na kwa Watoto Yatima.
“Namshukuru Rais Samia kwa kulimaliza hili jambo, nawashukuru viongozi wa Yanga na mashabiki wake, pia kuhusu zile fedha ambazo nilichangiwa siwezi kuzirudisha kwa waliotuma kwa kuwa siwafahamu hivyo nitapeleka kwa watu wenye uhitaji.”
Mara baada ya kutambulishwa Fei Toto na kusaini mkataba wa miaka mitatu, amekabidhiwa jezi namba 6 ambayo atakuwa anaivaa akiwa Azam FC