Azam FC yamtambulisha FEI TOTO, asaini mkataba wa miaka mitatu, afafanua fedha alizochangiwa na wadau

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mara baada ya kutambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa #AzamFC, Feisal Salum (Fei Toto) amesema fedha ambazo alichangiwa wakati wa sakata lake la kimkataba dhidi ya #Yanga, atazipeleka Msikitini, Kanisani na kwa Watoto Yatima.

“Namshukuru Rais Samia kwa kulimaliza hili jambo, nawashukuru viongozi wa Yanga na mashabiki wake, pia kuhusu zile fedha ambazo nilichangiwa siwezi kuzirudisha kwa waliotuma kwa kuwa siwafahamu hivyo nitapeleka kwa watu wenye uhitaji.”

Mara baada ya kutambulishwa Fei Toto na kusaini mkataba wa miaka mitatu, amekabidhiwa jezi namba 6 ambayo atakuwa anaivaa akiwa Azam FC
 
Mbona haraka sana? Mkataba kausoma au anataka aje asumbue watu baadae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…