Azam kuibomoa Yanga tena 99%. Bangala mali ya Azam FC

Azam kuibomoa Yanga tena 99%. Bangala mali ya Azam FC

Hivi hili swali ni gumu kwako hadi ulifikishe kwenye jukwaa hili.
Hebu twambie waliobaki ni wacheza mdako kama wewe siyo?
Ni mfululizo wa matukio ya wachezaji kuikataa Yanga. Niambie na wewe hilo haujiulizi inakuwaje timu inayofanya vizuri na kuchukua mataji wachezaji wake tegemeo wanaikimbia na wengine wanakiri wako tayari waache mpira kuliko kuendelea kuwepo pale. Kunaniii?
 
Viongozi wa Yanga wana akili sana pia wajanja alafu wanajua kusoma tabia za wachezaji… Djuma na Bangala viwango vya viliaza kutilia shaka huku tabia zao ziliaza kushuka pia kujitoa kwa asilimia zote hazikuwepo… Sasa hakuna jinsi ni kuuza na kuleta vijana wenye njaa na mafanikio…
 
Ila mashabiki wa makolo hamnazo kabisa! Badala wajenge timu wamekalia kuisema Yanga!😁😁😂😂😂
 
Ndo ukamuulize sasa kwamba mbona fedha za mauzo zimeenda yanga na kwake azionekani kwenye account
Ungemuuliza wewe ambaye ndiye msemaji wake nachojua kwenye account ya Yanga hazijaingiq hizo 2 bill sababu Mayele alikuwa kwetu kwa mkopo. Ay wewe Hersi ndo anakuambia? 😁
 
K
Wenye hela zao wamejichukulia mchezaji, wengine zilikuwa kelele tu.
Kwani ni Nani anasikitika ndani ya Yanga kwa Bangala kwenda Azam?!?! Hiyo ni blessing kwa Yanga ...Siyo mambo yote yawekwe mitandaoni...
 
Mm ni YANGA ila viongozi wa yanga Ni MATAPELI na hela pale jangwani tumeishiwa
 
Feisal je mbona kwa zaidi ya miezi 6 mlikuwa mnambembeleza arudi, mmekuja kumuachia baada ya kusutwa. Hizi mambo ya kuacha wachezaji ambao bado mnawahitaji bado mnajifunza, mikishakubaliana na hali ambayo hamuwezi kuibadilisha ndiyo mnakuja na maneno haya. Pia unaposema Yanga ilifukuza timu nzima, kumbuka hadi uongozi pia ulikuwa umegawanyika.

Ishu ya Chama hauijui nakushauri achana nayo.
Kuhusu Yanga kumbembeleza Feisal ni nyie Simba ndio mmeshikilia hilo Yanga ilishaachana nae toka alipoaxha kuonekana kambini ila nyie vijipu uchungu ndio mnakomalia Yanga alikua anamng'ang'ania na wakati Yanga ilikua inasimamia utaratibu.

Haya mambo hamuwezi kuyaelewa kwa sababu hamuwezi kusimamia utaratibu zaidi mtahitaji kulamba miguu ili mchezaji abaki
 
Viongozi wa Yanga wana akili sana pia wajanja alafu wanajua kusoma tabia za wachezaji… Djuma na Bangala viwango vya viliaza kutilia shaka huku tabia zao ziliaza kushuka pia kujitoa kwa asilimia zote hazikuwepo… Sasa hakuna jinsi ni kuuza na kuleta vijana wenye njaa na mafanikio…
Mkude na Bangala wanautofauti upi kwenye utovu wa nidhamu?
Vijana wenye njaa na mafanikio ndo kina Mkude?😂😅
 
Mkude na Bangala wanautofauti upi kwenye utovu wa nidhamu?
Vijana wenye njaa na mafanikio ndo kina Mkude?[emoji23][emoji28]

Hakuna kitu kibaya kwenye mpira kama mchezaji kusema nina 20% ya kubaki kwenye timu wakati unajua bado unamkataba wa mwaka na nusu… huwo ni utovu mkubwa wana nidhamu… Ndio maana huko nyuma Ngassa alishawai kutolewa kwa mkopo Kwenda Simba kisa kuvaa Jezi ya Yanga na kushangilia wakati bado anacheze Azam…
 
Kuhusu Yanga kumbembeleza Feisal ni nyie Simba ndio mmeshikilia hilo Yanga ilishaachana nae toka alipoaxha kuonekana kambini ila nyie vijipu uchungu ndio mnakomalia Yanga alikua anamng'ang'ania na wakati Yanga ilikua inasimamia utaratibu.

Haya mambo hamuwezi kuyaelewa kwa sababu hamuwezi kusimamia utaratibu zaidi mtahitaji kulamba miguu ili mchezaji abaki
Risiti tunazo zinaonyesha mkimuomba na kumuhimiza arudi Kimbiji
 
Uhamisho wa Yannick Bangala uko mbioni kukamilika. Yanga imepokea ofa ya milioni 100 kutoka kwa Azam FC.

Yannick alibakisha mkataba wa mwaka mmoja na klabu yake ya Yanga SC.

Biashara

1️⃣ Mayele 2.8B
2️⃣ Feisal Salum 200m
3️⃣ Yannick Bangala 100m
4️⃣ Shaban Djuma 100m ⏳
View attachment 2702069
Mayele ni kitu Kama 3.4 -3.6 bn
 
YANGA MWENZANGU ACHA KUJAZWA UONGO NAWE UKATEMBEA NAO. HUU UJINGA UMEUTOA WAPI? TANGA WAMEINGIZIWA BIL 2? UNAZIFAHAMU WEWE? UNAMFAHAMU MMILIKI WA MAYELE?
Nachelea kusema wew nimbumbumbu kama alivyotwambia sir Aden Rage
 
Back
Top Bottom