Mimi sijasema camera za offside ndiyo zitumike kama main camera. Camera za pembeni zilikuwepo kwa ajili ya kuchukua matukio ya pembeni ikiwemo offside ila kuna tukio moja ambalo Mohammed Hussein aliitiwa offside, camera haikuwa positioned kulichukua kwa usahihi hadi mtangazaji naye akashangaa maana katika marudio, mwanzo camera ilikata eneo ambalo isingeweza kuonyesha hiyo offside ilipo, ila ilipokuja kusogea ikaonyesha MH alipokuwa bado kuna wachezaji wengine wa Kagera upande wa goli lao na kuifanya ile kutokuwa offside. Mtangazaji akabaki kuguna tu. Ndiyo maana wengine tunapata tafsiri kuwa kuna ulipuaji wa kazi maana kama ni mfuatiliaji utajua production uwanja wa uhuru inakuwaga chini kwa maeneo mengi.
Vilevile narudia kusema, vipi wakiamua kuweka main camera upande huu wa pili wenye jukwaa chakavu, au na huku wamekatazwa maana huku ukikaa kwenye ngazi za juu kabisa nadhani kwanza unakuwa juu zaidi halafu unakuwa hauna makorokoro mengine kama nguzo za bendera zinazoziba camera.
View attachment 2843650
Ila vilevile kuna sababu nyingi za kutotumia huo uwanja, hilo la camera ni mojawapo tu. Ona mabenchi ya ufundi, yaani unamlipa kocha milioni 80 kuja kumkalisha sehemu kama hii?
View attachment 2843649