Vipo vingi, mkuu ila si wote wanaoweza kulipia supersport via Dstv nk...Kwamba king’amuzi hapa nchini ni Azam tu, si mdio eeh
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vipo vingi, mkuu ila si wote wanaoweza kulipia supersport via Dstv nk...Kwamba king’amuzi hapa nchini ni Azam tu, si mdio eeh
Hapana. Hakuna gharama yeyote utakayokatwa kwa ku'access' menu ya AzamPesa katika mtandao wowote. Ni bure.Hii huduma ina makato yeyote kwenda kwa Mtandao host?
Mfano Tigo, nikiingia kwenye menu ya AzamPesa watanikata salio?
Gharama za kutuma na kutoa pesa ni chini kulinganisha huduma nyinginezo za kifedhaNa je gharama za kutuma na kutoa Pesa zikoje?
Gharama za kutuma na kupokea zipo chini na nafuu kuliko huduma zingineNa kitu gani hasa nitanufaika nacho kwenye AzamPesa ambacho kwenye Mpesa sikipati? Hasa kama situmii King'amuzi cha Azam?
Sarafu ni huduma ya kutuma na kupokea malipo ya huduma na bidhaa.Tofauti ya hii huduma na SARAFU ni nini?
AzanPesa ni nafuu kulinganisha na huduma nyinginezo za kifedha.Kama Nina Tigo pesa, je kwanini niongeze na Azam pesa? Nini Cha zaidi na Cha ziada Azam pesa watanipatia?
Weka makato yake tuone apa mfano kutuma laki moja na kutoa wanakata shs ngap?????.......na je tozo za serikali ipo umo kwenye azampesa.Hapana. Hakuna gharama yeyote utakayokatwa kwa ku'access' menu ya AzamPesa katika mtandao wowote. Ni bure.
Gharama za kutuma na kutoa pesa ni chini kulinganisha huduma nyinginezo za kifedha
Gharama za kutuma na kupokea zipo chini na nafuu kuliko huduma zingine
Good question.Kwa mawakala nini wafanye ili waweze kusajiliwa kuwa mawakala wa AZAM PESA?.
Ili kuwa wakala wa AzamPesa, fika katika kibanda cha kusajili wateja wa kawaida wa AzamPesa.Kwa mawakala nini wafanye ili waweze kusajiliwa kuwa mawakala wa AZAM PESA?.
Nikuhakikishie;Kingine sio huduma inaanza baada ya muda inapotea tena.
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Nitaweka 'sheet' yenye gharama za kutuma na kutoa pesa kwa wateja wa AzamPesa.Weka makato yake tuone apa mfano kutuma laki moja na kutoa wanakata shs ngap?????.......na je tozo za serikali ipo umo kwenye azampesa.
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Hayo yanabaki kuwa makubaliano baina ya pande zote mbili.Kwa hiyo hii mitandao imekubali kiroho safi kutumika na nyie?
Sababu umesema gharama zenu ni nafuu zaidi kuliko watangulizi wenu mnaowatumia kufikia wateja wenu
1.kuna mawakala wengine wapo mikoani tena vijijini mfano wakala yupo matombo morogoro vijijini.Ili kuwa wakala wa AzamPesa, fika katika kibanda cha kusajili wateja wa kawaida wa AzamPesa.
Muombe akuelekeze kwa Wakala Mkuu wa AzamPesa. Ukifika, atakusajili kwanza kama mteja wa kawaida. Kisha atakupa form ya kujaza ukiambatanisha na vifuatavyo:
1. TIN NUMBER
2. LESENI YA BIASHARA
3.KITAMBULISHO CHA NIDA.
Ukishajaza na kusaini kukubaliana na vigezo na masharti, utamuachia Wakala Mkuu.
Naye atazikusanya na kuscan, zitatumwa kwetu. Tutakuandalia TILL number pamoja na vifaa vinginevyo.
Kisha, kumfikishia wakala Mkuu ambaye naye atakupigia simu ukafate documents zako tayari kama Wakala wa kawaida wa AzamPesa.
Karibu.
Ndio nashindwa kuelewa. Wana nini cha ziada?Kama Nina Tigo pesa, je kwanini niongeze na Azam pesa? Nini Cha zaidi na Cha ziada Azam pesa watanipatia?
Pia unaweza kutuma pesa kwenda mtandao washindani????......mfano kutuma pesa kutoka azampesa kwenda Tigo pesa au airtel moneyNitaweka 'sheet' yenye gharama za kutuma na kutoa pesa kwa wateja wa AzamPesa.
Ndiyo, tozo za serikali ni takwa la kisheria. Hivyo AzamPesa haina 'exception' ya kutojumuisha tozo za Kiserikali.
Kwa style hii mtawapata wachache sana.maswali ni mengi kuliko majibu.kuna faida/uzuri gani wa kujiunga na hiyo azampesa badala ya kutumia tigo pesa ya kawaida? Au hii ni sawa na Nala ile yule mtoto wa Fenandes?Kampuni kubwa na iliyoenea katika nchi ya Tanzania pamoja na nchi jirani 'Bakhresa Group' imeleta sokoni huduma mpya ya kifedha ijulikanayo kama 'Azam Pesa'.
Huduma hii ni kama zilivyo huduma nyinginezo za M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa and the like.
Ili kuielewa zaidi huduma hii, nitaenda katika mtindo wa Maswali na kisha majibu.
Je, Azam wameanzisha mtandao wao wa simu?
Hapana. Azam bado hawajaanzisha mtandao wao kama zilivyo kampuni kadhaa za mawasiliano hapa nchini.
Bali AzamPesa wameingia makubaliano na baadhi ya mitandao kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa huduma kupitia line za mitandao hiyo.
Mpaka sasa AzamPesa wameshakubaliana na Tigo, Airtel na Zantel. Hivyo huduma hii inapatikana katika line za mitandao tajwa.
Vodacom, Halotel na mitandao mingine bado wapo kwenye mazungumzo. Watakapokubaliana basi huduma hii itawezeshwa katika line hizo.
Je, huduma hi inahusika
na nini?
Kama ilivyo huduma zingine, huduma hii inahusika na;
1.Kutuma Pesa
2.Kutoa Pesa
3.Kulipia bili
4.Kulipia bidhaa za Azam
Je, huduma hii imeanza kufanya kazi?
Ndiyo, huduma hii imeshaanza kufanya kazi kwa wateja wote waliosajiliwa.
Je, najiungaje na huduma hii?
Fika katika duka la wakala na uweze kusajiliwa. Kinachohitajika ni namba yako ya simu pamoja na namba yako ya NIDA. Ndani ya dakika mbili tayari utakuwa umeshasajiliwa kuwa mteja wa AzamPesa.
Je, huduma naweza kupata vifurushi 'bundles' maalum vya Azam?
Hapana. Kama ambavyo nilijwishaeleza hapo juu kwamba Azam bado hawajaanzisha mtandao wao hivyo swala la vifurushi linabakia kuwa maamuzi ya mtandao husika.
Je, huduma hii naipata wapi?
Huduma hii inapatikana katika mikoa yote Tanzania. Ijapokuwa bado haijatapakaa kila mahali lakini upatikanaji wake katika maeneo mengi ya miji ni uhakika.
Je, menu 'ussd' ya AzamPesa ni ngapi?
Baada ya kusajiliwa, utabadili namba ya siri. Hivyo utabonyeza *150*08# na kuweza kupata huduma ya AzamPesa.
Kama una swali lolote kuhusiana na huduma za AzamPesa, basi karibu.
Wasalaam.