Azam Pesa: Huduma mpya ya kifedha

Azam Pesa: Huduma mpya ya kifedha

ANZISHENI SIM CARD YENU ITAKAYOKUWA NA HUDUMA ZA DATA NA KIFEDHA PEKEE NA SI KUPIGA SIMU,FANYENI ACCESS KWA HUDUMA ZA KIFEDHA DUNIANI KOTE MKIONGEZEA NA HUDUMA YA PAYPAL, MTAKUWA SUPA GIANT KWA EAST AFRICA.
 
Kampuni kubwa na iliyoenea katika nchi ya Tanzania pamoja na nchi jirani 'Bakhresa Group' imeleta sokoni huduma mpya ya kifedha ijulikanayo kama 'Azam Pesa'.

Huduma hii ni kama zilivyo huduma nyinginezo za M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa and the like.

Ili kuielewa zaidi huduma hii, nitaenda katika mtindo wa Maswali na kisha majibu.

Je, Azam wameanzisha mtandao wao wa simu?
Hapana. Azam bado hawajaanzisha mtandao wao kama zilivyo kampuni kadhaa za mawasiliano hapa nchini.

Bali AzamPesa wameingia makubaliano na baadhi ya mitandao kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa huduma kupitia line za mitandao hiyo.

Mpaka sasa AzamPesa wameshakubaliana na Tigo, Airtel na Zantel. Hivyo huduma hii inapatikana katika line za mitandao tajwa.

Vodacom, Halotel na mitandao mingine bado wapo kwenye mazungumzo. Watakapokubaliana basi huduma hii itawezeshwa katika line hizo.

Je, huduma hi inahusika
na nini?
Kama ilivyo huduma zingine, huduma hii inahusika na;
1.Kutuma Pesa
2.Kutoa Pesa
3.Kulipia bili
4.Kulipia bidhaa za Azam

Je, huduma hii imeanza kufanya kazi?
Ndiyo, huduma hii imeshaanza kufanya kazi kwa wateja wote waliosajiliwa.

Je, najiungaje na huduma hii?
Fika katika duka la wakala na uweze kusajiliwa. Kinachohitajika ni namba yako ya simu pamoja na namba yako ya NIDA. Ndani ya dakika mbili tayari utakuwa umeshasajiliwa kuwa mteja wa AzamPesa.

Je, huduma naweza kupata vifurushi 'bundles' maalum vya Azam?
Hapana. Kama ambavyo nilijwishaeleza hapo juu kwamba Azam bado hawajaanzisha mtandao wao hivyo swala la vifurushi linabakia kuwa maamuzi ya mtandao husika.

Je, huduma hii naipata wapi?
Huduma hii inapatikana katika mikoa yote Tanzania. Ijapokuwa bado haijatapakaa kila mahali lakini upatikanaji wake katika maeneo mengi ya miji ni uhakika.

Je, menu 'ussd' ya AzamPesa ni ngapi?
Baada ya kusajiliwa, utabadili namba ya siri. Hivyo utabonyeza *150*08# na kuweza kupata huduma ya AzamPesa.

Kama una swali lolote kuhusiana na huduma za AzamPesa, basi karibu.

Wasalaam.
Kwa sasa hivi, naweza kupata huduma ya azam pesa kwa lain ya vodacom.?
 
Kwa sasa hivi, naweza kupata huduma ya azam pesa kwa lain ya vodacom.?
😁Najibu kama freelancer, ndio unaweza kwasasa, pia, huduma ya kujisajili na Azampesa ni rahisi zaid. Ili kujiunga unatakiwa kuwasiliana nao kupitia namba ya Whatsapp +255 677 099 908 then utachagua kujisajili.
Vitu muhimu.
1. Number ya NIDA
2. Namba simu ambayo ipo hewani
3. Taarifa zako za NIDA ulizojaza wakati wa kujiandikisha (taarifa mbili tu)

Kuhusu mawakala: kwasasa wapo sehemu kubwa ya Dar es salaam na mikoani
Jinsi ya kujua wakala aliyekaribu nawe tafadhali nenda kwenye page yao ya Facebook, Instagram then taja eneo ulipo mfano; nipo tandale naomba wakala wa Azampesa aliyekaribu nami.
Azampesa: Jj Shop 07877711** mpigie kwa mawasiliano zaid
 
Back
Top Bottom