Azam Pesa: Huduma mpya ya kifedha

Hii huduma ina makato yeyote kwenda kwa Mtandao host?

Mfano Tigo, nikiingia kwenye menu ya AzamPesa watanikata salio?
Hapana. Hakuna gharama yeyote utakayokatwa kwa ku'access' menu ya AzamPesa katika mtandao wowote. Ni bure.
Na je gharama za kutuma na kutoa Pesa zikoje?
Gharama za kutuma na kutoa pesa ni chini kulinganisha huduma nyinginezo za kifedha
Na kitu gani hasa nitanufaika nacho kwenye AzamPesa ambacho kwenye Mpesa sikipati? Hasa kama situmii King'amuzi cha Azam?
Gharama za kutuma na kupokea zipo chini na nafuu kuliko huduma zingine
 
Tofauti ya hii huduma na SARAFU ni nini?
Sarafu ni huduma ya kutuma na kupokea malipo ya huduma na bidhaa.

Sarafu inahitaji kuunganisha account zako za benki na mfumo wa Sarafu. AzamPesa haihitaji taarifa zako za kibenki.

Sarafu inakuhitaji uwe na Application maalum. AzamPesa inahitaji namba yako ya simu pekee na kuunganishwa.

Karibu!.
 
Weka makato yake tuone apa mfano kutuma laki moja na kutoa wanakata shs ngap?????.......na je tozo za serikali ipo umo kwenye azampesa.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Kwa mawakala nini wafanye ili waweze kusajiliwa kuwa mawakala wa AZAM PESA?.
Ili kuwa wakala wa AzamPesa, fika katika kibanda cha kusajili wateja wa kawaida wa AzamPesa.

Muombe akuelekeze kwa Wakala Mkuu wa AzamPesa. Ukifika, atakusajili kwanza kama mteja wa kawaida. Kisha atakupa form ya kujaza ukiambatanisha na vifuatavyo:
1. TIN NUMBER
2. LESENI YA BIASHARA
3.KITAMBULISHO CHA NIDA.

Ukishajaza na kusaini kukubaliana na vigezo na masharti, utamuachia Wakala Mkuu.

Naye atazikusanya na kuscan, zitatumwa kwetu. Tutakuandalia TILL number pamoja na vifaa vinginevyo.

Kisha, kumfikishia wakala Mkuu ambaye naye atakupigia simu ukafate documents zako tayari kama Wakala wa kawaida wa AzamPesa.

Karibu.
 
Kingine sio huduma inaanza baada ya muda inapotea tena.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Nikuhakikishie;

Ndiyo, huduma huanzishwa ili kuleta tija kwa jamii. Lakini pia, kampuni hujiwekea malengo kupitia utoaji wa huduma hiyo.

Kampuni itakapoona huduma hiyo haina tija na huleta hasara, basi huifunga na kuipotezea.

Lakini, wataalamu na washauri wa 'Bakhresa Group' wameshafanya tafiti na kujihakikishia kuwa AzamPesa italeta mapinduzi katika huduma za kifedha. Hivyo kwa namna yeyote, haitoweza kupotea.

Karibu kuwa mteja wa AzamPesa.
 
Weka makato yake tuone apa mfano kutuma laki moja na kutoa wanakata shs ngap?????.......na je tozo za serikali ipo umo kwenye azampesa.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Nitaweka 'sheet' yenye gharama za kutuma na kutoa pesa kwa wateja wa AzamPesa.

Ndiyo, tozo za serikali ni takwa la kisheria. Hivyo AzamPesa haina 'exception' ya kutojumuisha tozo za Kiserikali.
 
1.kuna mawakala wengine wapo mikoani tena vijijini mfano wakala yupo matombo morogoro vijijini.
2.kuna wakala ana namba ya nida ila kitambulisho bado hajapata.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Nitaweka 'sheet' yenye gharama za kutuma na kutoa pesa kwa wateja wa AzamPesa.

Ndiyo, tozo za serikali ni takwa la kisheria. Hivyo AzamPesa haina 'exception' ya kutojumuisha tozo za Kiserikali.
Pia unaweza kutuma pesa kwenda mtandao washindani????......mfano kutuma pesa kutoka azampesa kwenda Tigo pesa au airtel money

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Kwa style hii mtawapata wachache sana.maswali ni mengi kuliko majibu.kuna faida/uzuri gani wa kujiunga na hiyo azampesa badala ya kutumia tigo pesa ya kawaida? Au hii ni sawa na Nala ile yule mtoto wa Fenandes?

Maswali ni mengi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…