Azam TV badilisheni Tamthilia zenye mlengo wa itikadi za kidini

Mkwawe

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2016
Posts
3,132
Reaction score
5,508
Jana nimerudi nimechoka nikafikia kujitupa tu kwenye kiti hakukuwa na mtu sebuleni ila TV ilikuwa inaonesha chaneli ya Azam 2

Macho yangu yakaona kipande kimoja kwenye tamthilia ya kituruki bila shaka inaitwa Alpasalani nadhani, Sasa Kuna Binti alikuwa Yuko kwenye mtego na viongozi wa utawala mwingine inaonesha huo utawala una Ukristu maana askari wake wana misalaba kwenye mavazi yao.

Sasa hawa askari aisee ni midebwedo vibaya mno yaani mwanamke moja anaua infidels (humo wanaita wadhalimu) zaidi ya 20 mbele ya kiongozi wao halafu Yuko pekeake na bado anaendelea kusurvive!? Duuuh ina maana hao ni wanyonge kiasi hiko? Halafu mule inaonesha waislamu ni watu wema sana na wakristu ni watu wenye Roho mbaya mno na hii chanel secular ila inabagua Imani moja na kuipendelea ingine.

Ututuki ni nchi ambayo raia wake wengi ni waislamu hivyo ni sawa kuwa na maudhui kama Yale, Sasa Tanzania hii ni multi religion county huwezi kuwa na maudhui hayo hayo tu kila siku ya kukandamiza Imani moja na kuipendelea ingine kulikuwa na;
  • Ertugrul
  • Ottoman
  • Barbarossa na Sasa ni hii
  • Alpasalani
Zote hizi maudhui ni yaleyale.

Azam tv badilikeni, hela tunalipa sisi lakini mnatutibua nyingi makusudi kabisa.

Na huu mwezi nitaacha kulipia hiki kisimbuzi kama ni ligi kuu nitaangalia bandani na kisimbuzi nitanunua cha startimes.

Azam tv mjifunze kwa wenzenu, mbona wao wanajua mipaka yao.

Mnakera bwana aah!
 
Hapana, azam ni wafanya biashara na tv lazima itafute content ambayo wanaimudu ki gharama na muendelezo imetokea kwamba wamiliki wa azam wanaukaribu na channel au kampuni fulani ya kituruki wasichangamkie fursa? Endapo kama hata bongo movie na tamthiliya za kiswahili zingekuwa na maudhui hayo hapo ingekuwa na hoja.

Pia mbona kuna tamthiliya za kikorea pia? Ni kweli waturuki ni waislam na si dhambi kwa mfanyabiashara wa dini fulani kupigia debe maudhui ya dini yake,
Afadhali ungelalamika azam tv kutumia nguvu nyingi kuinadi timu au bidhaa zao . Mimi naona wapo sahihi katika ulimwengu wa movie wamerekani na wazungu wasio waislam ndio wametawala sana ndio maana sinema zenye maudhui ya kiislam kutoka azam unaona kama zina ukakasi
 
Jana nimerudi nimechoka nikafikia kujitupa tu kwenye kiti hakukuwa na mtu sebuleni ila TV ilikuwa inaonesha chaneli ya Azam 2

Macho yangu yakaona kipande kimoja kwenye tamthilia ya kituruki bila shaka inaitwa Alpasalani nadhani, Sasa Kuna Binti alikuwa Yuko kwenye mtego na viongozi wa utawala mwingine inaonesha huo utawala una Ukristu maana askari wake wana misalaba kwenye mavazi yao.

Sasa hawa askari aisee ni midebwedo vibaya mno yaani mwanamke moja anaua infidels (humo wanaita wadhalimu) zaidi ya 20 mbele ya kiongozi wao halafu Yuko pekeake na bado anaendelea kusurvive!? Duuuh ina maana hao ni wanyonge kiasi hiko? Halafu mule inaonesha waislamu ni watu wema sana na wakristu ni watu wenye Roho mbaya mno na hii chanel secular ila inabagua Imani moja na kuipendelea ingine.

Ututuki ni nchi ambayo raia wake wengi ni waislamu hivyo ni sawa kuwa na maudhui kama Yale, Sasa Tanzania hii ni multi religion county huwezi kuwa na maudhui hayo hayo tu kila siku ya kukandamiza Imani moja na kuipendelea ingine kulikuwa na;
  • Ertugrul
  • Ottoman
  • Barbarossa na Sasa ni hii
  • Alpasalani
Zote hizi maudhui ni yaleyale.

Azam tv badilikeni acheni upumbavu wenu hela tunalipa sisi lakini mnatutibua nyingi makusudi kabisa. Na huu mwezi nitaacha kulipia hiki kisimbuzi kama ni ligi kuu nitaangalia bandani na kisimbuzi nitanunua cha startimes.

Azam tv mna mazoea sana aisée na kazi zenu, Imani hazilazimishwi kihivyo, mjifunze kwa wenzenu mbona wao wanajua mipaka yao.

Mnakera bwana aah!
lawama tu muda wote kama ndugu wa mke
 
Hapana, azam ni wafanya biashara na tv lazima itafute content ambayo wanaimudu ki gharama na muendelezo imetokea kwamba wamiliki wa azam wanaukaribu na channel au kampuni fulani ya kituruki wasichangamkie fursa? Endapo kama hata bongo movie na tamthiliya za kiswahili zingekuwa na maudhui hayo hapo ingekuwa na hoja.
Pia mbona kuna tamthiliya za kikorea pia? Ni kweli waturuki ni waislam na si dhambi kwa mfanyabiashara wa dini fulani kupigia debe maudhui ya dini yake,
Afadhali ungelalamika azam tv kutumia nguvu nyingi kuinadi timu au bidhaa zao . Mimi naona wapo sahihi katika ulimwengu wa movie wamerekani na wazungu wasio waislam ndio wametawala sana ndio maana sinema zenye maudhui ya kiislam kutoka azam unaona kama zina ukakasi
Ving'amuzi vyote Tz 90% vinarusha maudhui ya kituruki uyu jamaa ana lock mindset
 
We kama unaona AZAM TV inakukwaza achana nayo kaangalie ITV huko kila Jumapili mambo ya kanisani lakini Ijumaa hakuna mambo ya msikitini.Pia kaa angalie channel 10 yuko BULLDOZER Mwammposa ! Shida yako nini ??? Achana na AZAM
 
Back
Top Bottom