Azam TV haina uwezo wa kifedha kuonesha Kombe la Dunia?

Azam TV haina uwezo wa kifedha kuonesha Kombe la Dunia?

Hawana hyo pesa

Dstv kanunua kwa ajili ya kuonesha kwenye bara zima la afrika

Wakati azam mitambo yake ipo east afrika tu
Mmmh..bara zima la afrika hapo nakupinga....DSTV inafanya kazi nchi zinazoongea haswa kingereza..DSTV haipo nchi za kiarabu..wana BEIN SPORT na haipo nchi wanazoongea kifaransa..kuna CANAL SPORT
 
Unaweza kuwa na hela lakini usipate hiyo nafasi.

Upande huu wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, mwenye haki za kuonyesha kombe la dunia ni Multi Choice ambayo ndiyo hao DsTv.
 
Azam mechi za ligi tu zimemshinda anaonyesha picha hafifu na kamera uwanjani anaweka chache Sasa nani wa kumpa tenda hiyo
Acha uchawi,Azam kibongobongo anajitahidi sana,hakuna TV station bongo inayoweza kuonyesha ligi yetu kwa viwango na weledi kama Azam.
Kuhusu kombe la dunia huonyeshi bila kuwa na haki,kupata hiyo haki ni kazi
 
hailipi mkuu kiupande wao, wabongo hatuwezi kulipia kifurushi bei kubwa, na pia soko lake ni dogo, DSTV wamejitawanya nchi nyingi sana na ndio mana kwao inawalipa.
Bongo tunaambiwa population yetu ni milion 60, ila walioweka Azam ndani yamajumba yao ni wangapi? wengi wetu tunaishi kwa mabanda umiza tu.
 
hailipi mkuu kiupande wao, wabongo hatuwezi kulipia kifurushi bei kubwa, na pia soko lake ni dogo, DSTV wamejitawanya nchi nyingi sana na ndio mana kwao inawalipa.
Bongo tunaambiwa population yetu ni milion 60, ila walioweka Azam ndani yamajumba yao ni wangapi? wengi wetu tunaishi kwa mabanda umiza tu.
Wenye Azam kwa data za TCRA hata milioni moja hawafiki..sasa Azam huo uthubutu wa kununua haki za mashindano haya makubwa atatoa wapi na hata akijaribu hawezi kushinda..Dstv wamekaba sana huku kusini mwa jangwa la sahara.
 
Je, Azam TV hawana uwezo wa kifedha kuweza shinda kandarasi ya kuonesha Kombe la Dunia?
Iko hivi, ili kupata haki/zabuni/tenda ya kurusha matangazo ya kombe la dunia au kombe lolote tu hata ligi za mataifa mengine ni lazima inaendeshwa mchakato na wanazingatia vigezo vingi.Moja wapo ni vifuatavyo
1. Coverage/ TV yako inaangaliwa eneo au ukubwa gani?
2. Matangazo yao ambayo mataingia nao makubaliano katika mabunguzo ya mkataba huo yana faida gani kwao kulingana na eneo/Maeneo TV yako inapoonekana.
3. Ikiwa wazungumzaji wa eneo la coverage ya TV yako wanashabiana na lugha inayotumika kutanga ligi au kombe hilo
4. Ubora wa TV yako na record zako za nyuma?.
5. Idadi ya watu wanaotazamiwa kuangalia ligi hiyo
6. Political stability ya eneo husika(japo hiki kipengere ni cha zamani)
7. Record yako katika kuomesha mashindano mbali mbali
8. Gharama zao uweze kuzimudu.

Sasa here is the thing..
1. Azam ni mchanga zan kwa Mult choice (DSTV)
2. Dstv inakava Africa nzima wakati azam anafika Tz, uganda, kenya, Rwanda, Burundi, congo, na sasa naona anajipanua Sudani na central Africa
3. Katika nchi anazofik Azam wingi wa watazamaji sio kivile.
4. Dstv ni mkongwe na amekua akifanya vizuri kila wakati
5. Pia fedha wanayohitaji na mtaji wa Azam wameona kama bado hajakua sana.


Free ideas
 
Back
Top Bottom