Azam TV haina uwezo wa kifedha kuonesha Kombe la Dunia?

Azam TV haina uwezo wa kifedha kuonesha Kombe la Dunia?

Nadhani uwezo wa kushindana na kununua wanao....nadhani wametathmini hali ya soko na ushindani na gharama za kununua alafu ni jambo la muda mfupi wameona halina faida.......


Ni mtizamo wangu tu......
Azam TV hana hela za kupata hizo haki, pia hana miundombinu nchi nyingi
 
hailipi mkuu kiupande wao, wabongo hatuwezi kulipia kifurushi bei kubwa, na pia soko lake ni dogo, DSTV wamejitawanya nchi nyingi sana na ndio mana kwao inawalipa.
Bongo tunaambiwa population yetu ni milion 60, ila walioweka Azam ndani yamajumba yao ni wangapi? wengi wetu tunaishi kwa mabanda umiza tu.
Asilimia 1
 
Iko hivi, ili kupata haki/zabuni/tenda ya kurusha matangazo ya kombe la dunia au kombe lolote tu hata ligi za mataifa mengine ni lazima inaendeshwa mchakato na wanazingatia vigezo vingi.Moja wapo ni vifuatavyo
1. Coverage/ TV yako inaangaliwa eneo au ukubwa gani?
2. Matangazo yao ambayo mataingia nao makubaliano katika mabunguzo ya mkataba huo yana faida gani kwao kulingana na eneo/Maeneo TV yako inapoonekana.
3. Ikiwa wazungumzaji wa eneo la coverage ya TV yako wanashabiana na lugha inayotumika kutanga ligi au kombe hilo
4. Ubora wa TV yako na record zako za nyuma?.
5. Idadi ya watu wanaotazamiwa kuangalia ligi hiyo
6. Political stability ya eneo husika(japo hiki kipengere ni cha zamani)
7. Record yako katika kuomesha mashindano mbali mbali
8. Gharama zao uweze kuzimudu.

Sasa here is the thing..
1. Azam ni mchanga zan kwa Mult choice (DSTV)
2. Dstv inakava Africa nzima wakati azam anafika Tz, uganda, kenya, Rwanda, Burundi, congo, na sasa naona anajipanua Sudani na central Africa
3. Katika nchi anazofik Azam wingi wa watazamaji sio kivile.
4. Dstv ni mkongwe na amekua akifanya vizuri kila wakati
5. Pia fedha wanayohitaji na mtaji wa Azam wameona kama bado hajakua sana.


Free ideas
Maelezo mazuri sana
 
Mmmh..bara zima la afrika hapo nakupinga....DSTV inafanya kazi nchi zinazoongea haswa kingereza..DSTV haipo nchi za kiarabu..wana BEIN SPORT na haipo nchi wanazoongea kifaransa..kuna CANAL SPORT
Uko sahihi,hata watu wa Cable Tv Tz hawatumii DStv..........mi mwenyewe naangalia kupia App Football Live,siyo mechi za world cup tu bali ligi zote 5 kubwa
 
Je, Azam TV hawana uwezo wa kifedha kuweza shinda kandarasi ya kuonesha Kombe la Dunia?
Suala wala siyo Fedha

Mfano Kuna Vituo vikubwa kama

Sky sports,
BT sports
CBS sports
NBC sports,
Vyoote hivi hakuna hata kimoja kilichopata idhini ya kurusha World cup. Je na vyenyewe havina hela?

Kuwa na hela ni kitu kingine na kupata haki za matangazo ni kitu Kingine.
 
Back
Top Bottom