Azam Tv kutoonesha Ligi kuu Tz bara msimu ujao

wakijitoa wachunguzwe walivyouwa tembo na kukwepa kodi..watajuta kumfahamu jiwe
 
Naona vibarua vya kina Nyembera,kabombe,mpenja vinaenda kuota nyasi pale daah
 
 
Pombe no... Lakini Sport pesa michuano inayodhaminiwa na kampun la kamari yes... Hapana niacheni nadhani kuna kitu sijaelewa.....
 
Pombe no... Lakini Sport pesa michuano inayodhaminiwa na kampun la kamari yes... Hapana niacheni nadhani kuna kitu sijaelewa.....
Lini ulioona wanarusha michuano ya sportpesa? hawajawahi kurusha walikataa ndio maana ilirushwa na itv,star tv
 
Lile jini bado lina wafuatilia TFF na sasa linakwenda kwenye Ligi......Yajayo yanafurahisha[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Hahah imani na biashara buana, kuna watu imani kali kabisa, wanakwambia dini hairuhusu mikopo yenye riba, ila bodi ya mikopo ikifungua dirisha mzee ndio wa kwanza kufatilia form za kujaza😀😀😀😀😀, wakati mkopo huo pia unajumuisha riba.
 
nilitaka kulipia kingamuzi cha azam kesho,lakini kwa hali hii ngoja nitafute mteja kabla hakijanidodea
 
Kabla ya sportpesa Yanga ma Simba walikuwa wanadhaminiwa na Tbl kupitia bia yao ya Kilimanjaro. Je walikua hawonyeshi mechi zao?
 
Wachukue zabuni DSTV mambo yaendeleee ya kuonyesha live
 
Sidhani kama mleta mada ameleta taarifa ya ukweli, Simba SC wamekuwa na program ya Simba TV ndani ya Azam channel kwa zaidi ya miaka 2, na wakati kipindi kinaanza walikuwa nadhaminiwa na TBL kupitia brand ya Kilimanjaro Beer, lakini Azam walikuwa kimya katika hili, ukiingiza udini sana kwa nchi kama Tanzania unaweza filisika. Sidhani kama Azam wapo tayari kufunga biashara ya King'hamuzi cha Azam, kwani bila ligi kuuTZ biashara kwishney.
 
Wanaona Pombe Ni Dhambi Wakati Nao Ni Wadhambi Tu. Lini Walikuwa Ni Watakatifu Kama Si Unafiki? Wanaogopa Tope Wakati Wanakanyaga Udongo

Kila mtu ni mtenda dhambi sawa, ila kuzuia dhambi ya waziwazi ndio bora zaidi. Ndio maana mda wote tunaomba toba kwa Mola wetu mlezi ila si.kigezo cha kufanya dhambi hadharani
 
[HASHTAG]#OFFICIAL[/HASHTAG]
KAMPUNI ya Azam TV imesema kwamba itaendedelea kuuheshimu na kuutekeleza mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu ya Bara kulingana na mabukubaliano yao na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

>>Katika mahojiano maalum leo, Mkurugenzi wa Azam TV, Yussuf Bakhresa amesema kwamba wataendelea kuonyesha mechi za Ligi Kuu chini ya udhamini wa kampuni yoyote kulingana na makubaliano yao na TFF.

“Jukumu letu ni kuonyesha mechi za Ligi Kuu, hilo tutaendelea kulitekeleza kama ambavyo tumekuwa tukifanya miaka yote. Na zaidi ninachoweza kusema ni kwamba watazamaji wetu watarajie mambo mazuri zaidi,”amesema Bakhresa akizungumza kwa simu kutoka Dubai jioni hii.

>>Bakhresa amesema kwamba wamekuwa wakipokea maoni mbalimbali kutoka kwa wadau juu ya mapungufu kadhaa katika uonyeshaji wa mechi za Ligi Kuu na nyingine nyingi na wakati wote wamekuwa wakiyafanyia kazi.

“Hadi sasa tunaridhishwa na kiwango chetu, lakini tumekuwa tukipokea maoni juu ya mapungufu madogo madogo na tumekuwa tukiyafanyia kazi. Na tutaendelea kuyafanyia kazi kwa lengo la kuhakikisha tunawafikishia watazamaji wetu matangazo bora kabisa,”.

Katika hatua nyingine, Bakhresa pia amesema kwamba wamefurahishwa na mafanikio ya klabu ya Azam FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Bara kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo.

>>Bakhresa amesema kwamba hayo ni matunda ya uwekezaji wao mzuri katika timu, lakini pia kushiriki Ligi Kuu nzuri yenye ushindani. “Azam FC itakuwa na maandalizi mazuri kabla ya msimu mpya wa Ligi Kuu, lengo ni kuhakikisha inafanya vizuri na kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo,”amesema Bakhresa.

*PotiphaJonathan*
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…